• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vivutio vya Kitalii

IFAHAMU HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSEGA NA FURSA MBALIMBALI ZA UWEKEZAJI

Ni furaha kubwa ndugu msomaji kukuletea fursa za uwekezaji zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Busega kwa lengo la kukuwezesha kuifahamu vyema wilaya ya Busega pamoja na kuzifahamu fursa hizo mbalimbali zilizopo katika wilaya hii, ambazo zinawezesha uwekezaji wa aina mbalimbali katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Halmashauri ya wilaya ya Busega imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi za asili ambazo hazijawekewa uwekezaji wa kutosha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mitaji ya uwekezaji mkubwa na wa ngazi ya kati. Kwa hali hiyo kumesababisha uwekezaji katika Halmashauri yetu kuwa ni wa chini lakini pia kwa upande mwingine ufinyu wa uwekezaji umesababishwa na wawekezaji wengi kutokuwa na taarifa sahihi au kutokuwa na taarifa kabisa juu ya fursa zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Busega. Uwekezaji ni moja ya njia madhubuti inayoweza kupunguza/kutokomeza umasikini na kufikia azma ya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega ni mojawapo ya halmashauri 6 zilizopo mkoa wa Simiyu ambapo mkoa huu una jumla ya wilaya 5. Halmashauri ya Wilaya ya Busega imeanzishwa mwaka 2013 ikiwa ina Tarafa 2, kata 15, vijiji 59 na vitongoji 362. Vyombo vya kiutendaji vinaendeshwa kupitia Halmashauri ya Wilaya ambayo ina jumla ya madiwani 21 ambapo madiwani 15 ni wa kuchaguliwa na madiwani 6 ni wa viti maalum.

Kijiografia wilaya ya Busega inapakana na wilaya ya Magu upande wa kusini, wilaya ya Bunda upande wa kaskazini, wilaya ya Bariadi upande wa mashariki na kwa upande wa magharibi imepakana na ziwa Viktoria. Wilaya ya Busega ina jumla ya ukubwa wa kilometa za mraba 2129, ambapo kilometa za mraba 1524 ni nchi kavu, na kilometa za mraba 605 ni maji, hivyo wilaya hii ni chachu ya fursa kubwa kwa wawekezaji kwa uwekezaji ikiwemo uwekezaji wa viwanda vikubwa na vidogo vya uzalishaji. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Busega ina jumla ya idadi ya watu 203,597.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega imejaliwa kuwa na hali nzuri ya hewa kwa uwekezaji mbalimbali. Ustawi na rutuba nzuri ya udongo uliopo Busega hustawisha mazao ya aina mbalimbali ya biashara na chakula ikiwemo pamba, mpunga, choroko, dengu, mahindi, mtama, mihogo na viazi.   

Mazingira rafiki pamoja na hali nzuri ya hewa inawezesha ustawi wa mifugo, hivyo kufanya ufugaji ni moja ya shughuli kubwa ya kiuchumi wilayani Busega. Mifugo aina mbalimbali inazalishwa na kufugwa ikiwemo ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega imejaliwa kuwa na sehemu ya ziwa Viktoria yenye ukubwa wa kilometa za mraba 605 upande wa magharibi kutoka kata ya Kiloleli mpaka kata ya Lamadi iliyopo kaskazini mwa wilaya hii. Ziwa Viktoria ndilo ziwa linalounganisha mikoa mingi nchini Tanzania na kati ya Halmashauri 6 zinazounda mkoa wa Simiyu, Halmashauri ya Wilaya ya Busega ndiye pekee imepakana na Ziwa Viktoria; hivyo shughuli za uvuvi na usafiri wa majini ni miongoni mwa shughuli kubwa za kiuchumi wilayani Busega. Samaki aina ya Sato na Sangara na dagaa hupatikana kwa wingi wilayani Busega, pia shughuli ya Ufugaji wa Samaki kwa kutumia Vizimba (Fish Cage) huchangia uchumi wa maendeleo kwa wananchi wa Halmashuri ya wilaya ya Busega. Kwa upande mwingine ziwa linasaidia kwa kiasi kikubwa kilimo cha umwagiliaji hivyo kufanya shughuli za kilimo wilayani Busega kuwa ni za mwaka mzima ambapo kilimo hicho ni pendekezwa katika dunia ya sasa.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega imejaliwa kuwa na pori la akiba la Kijereshi lenye ukubwa kilometa za mraba 65.72. Pori hili linapakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa Upande wa Kaskazini na Mashariki na jumla ya Vijiji sita Lukungu, Mwabayanda, Mwakiroba, Kijilishi, Nyamikoma na Senta kwa Upande wa Kusini na Magharibi. Wanyamapori kama vile Tembo, Nyati, Simba, Chui, Pundamilia, Nyumbu, Nyamera, Kuro, Ngiri, Nguruwe pori, Fisi, Bweha dhahabu, Bweha masikio, Swalapala, Swala tomi, Tohe, nyani,Tumbili, Sungura na wengine wengi wanapatikana kwenye pori la akiba Kijereshi.

Pori hili lipo karibu na Miji mikuu Mwanza (145km), Musoma (100km) na Bariadi (75Km), na Mji mdogo unaokaua kwa kasi wa Lamadi (3km) na hii inawezesha  wageni wanaoitembelea mji huu, Kukidhi shauku yao ya kuona wanyamapori kwa muda mfupi wanaoweza kuutenga katikati ya ratiba zao na kuweza kupata mahitaji kama malazi na chakula kwa gharama nafuu.

Pori la akiba Kijereshi linaweza kufikika kwa usafiri wa anga kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza. Na pia Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa eneo la Igegu- Bariadi (The Proposed Serengeti International Airport) Kunafungua fursa ya kukuza utalii wa Kanda ya Ziwa kwa kupata wageni wa kimataifa moja kwa moja kutoka nchi zao na kuwawezesha watanzania kutoka mikoa mingine ya nchi, kutembelea Pori kwa muda/siku chache hivyo kupunguza gharama za matumizi. Pia Halmashauri ya Wilaya ya Busega imepakana na lango la kuingia Hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa upande wa kaskazini mwa wilaya; hivyo hupokea wageni wengi wa ndani na nje ya Tanzania kwaajili ya Utalii.

Juhudi ya kukabiliana na changamoto ya miundombinu ya mawasiliano na nishati ni kubwa ambapo kwa sasa ni kipaumbele katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Mawasiliano ya barabara katika wilaya ni mazuri na sehemu zote zinafikika kwa wepesi na kwa wakati hivyo kufanya muingiliano wa watu kuwa ni mkubwa. Muingiliano huo pia huchangiwa na uwepo wa barabara kuu ya Mwanza-Musoma. Kwa upande wa nishati, karibu vijiji vyote 59 vipo kwenye mpango wa umeme vijjini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), huku huduma za mitandao ya mawasiliano ya simu zikiwa ni nzuri zinazotolewa na makampuni ya TTCL, Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel na Zantel mengineyo.

Kwa ujumla fursa za uwekezaji wilayani Busega ni kubwa hivyo hakuna haja ya wawekezaji kusita kuja kuwekeza kwenye Halmashauri yetu. Hivyo tunawakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza wilayani Busega ili kwa pamoja kuweza kuinua uchumi na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii nchini. Wawekezaji wenye ndoto na maendeleo wanayo nafasi ya kuchagua sehemu sahihi ya kufikia ndoto za maendeleo hawana shaka kukaribia kufanya uwekezaji Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Unakaribishwa Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Imeandaliwa na Kitengo cha TEHAMA-BUSEGA

Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Busega December 15, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili Mwaka 2022_Wilaya ya Busega January 04, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2022_Wilaya ya Busega January 29, 2023
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI BUSEGA LAITAKA RUWASA KUJIRIDHISHA NA TAKWIMU ZA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI

    November 18, 2022
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa