Kamati ya siasa mkoa wa Simiyu imefanya ziara wilayani Busega kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo. Katika ziara hiyo ambayo imeongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa mkoa wa Simiyu Ndg. Gungu Silanga, imeweza kutembelea miradi mitano katika sekta ya maji, barabara, mifugo na afya.
Katika ziara hiyo ambayo uongozi wa Wilaya ya Busega umepongezwa kwa kazi nzuri ya usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali, ambapo miradi iliyotembelewa inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.1.
“Tuendelee kusimamia miradi ya maendeleo vyema, ili wananchi wetu wapate huduma, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi”, aliongeza Silanga.
Akiongea kwa niaba ya viongozi wengine wa wilaya, Mkuu wa wilaya ya Busega Mhe. Anna Gidarya, amesema Wilaya ya Busega itaendelea kusimamia miradi, ili wananchi waone matunda ya Serikali yao.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa