• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Sheria Ndogo

                                              TANGAZO LA SERIKALI  NA. 206 la tarehe 29/05/2015

SHERIA YA FEDHA ZA SERIKALI ZA MITAA

SURA YA 290

______

SHERIA NDOGO

_____

Zimetungwa chini ya kifungu cha 7(1) na 16(1)

______

SHERIA NDOGO ZA (USHURU WA STENDI NA MAEGESHO YA MAGARI), ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSEGA   ZA  MWAKA, 2013

Jinan a mwanzo wa kutumika
1. Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Magari,2015 za Halmashauri ya  Wilaya ya Busega za Mwaka,2015 na zitaanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali.

Eneo la matumizi
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Tafsiri
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo;
“Afisa Muidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi.
“Ada” maana yake ni kiasi cha fedha kinacholipwa kwa Halmashauri na dereva au mwenye gari kama ada ya vituo vya mabasi, maeneo ya maegesho ya magari na vituo vya kuoshea magari
“Daladala” maana yake ni mabasi madogo ya jumuiya yanayosafirisha abiria au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya Halmashauri;
“Eneo la kuoshea magari” maana yake ni eneo  maalumu lililotengwa au kujengwa kwa ajili ya kuoshea magari na linalotambuliwa na Halmashauri
 “Halmashauri maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
“Kituo cha basi” maana yake ni stendi ya mabasi au eneo maalumu lilolotengwa kwa ajili ya mabasi ya abiria au chombo cha usafiri kwaajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.
“Kuegesha gari” maana yake ni kupaki gari au kusimamisha gari kwa muda kando ya barabara au gereji au eneo maalum lililotengwa kwa ajili hiyo.
“Magari ya biashara” maana yake ni magari au chombo cha usafiri kinachotumika kusafirisha abiria au mizigo kutoka sehemu moja hadi nyingine;
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi.
“Wakala” maana yake ni mtu, kikundi cha watu, kampuni au Taasisi aliyeteuliwa na Halmashauri kutekeleza majukumu ya kukusanya ushuru kwa niaba yake.
Usajili wa magari
4.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa magari yanayotumika kufanya shughuli ya kusafirisha abiria au mizigo katika eneo la Halmashauri kuhakikisha kwamba gari lake limesajiliwa na Halmashauri kabla ya kuanza kazi hiyo.
(2) Maombi ya usajiri wa magari au chombo chochote cha usafiri  yatatolewa kwa kujaza fomu maalumu kama itakavyoelekezwa na Halmashauri.
(3) Kila mwombaji wa usajili wa gari au chombo kingine cha usafiri atapaswa kulipa ada ya usajili kwa mwaka kwa viwango itakavyoainishwa na Halmashauri.



5.-(1) Vyombo vyote vya usafiri vinavyotumika kwa biashara ya usafirisha abiria na au mizigo vitapaswa;-
  • kuonyesha jina na anuani ya mmiliki
  • kupakwa rangi maalumu au alama maalumu iliyoidhinishwa na Halmashauri;

(2) Itakuwa ni wajibu wa kila dereva wa vyombo vya usafiri kuwasilisha picha aina ya passport size ofisi za Halmashauri ambazo zitatunzwa katika jalada   maaalum la vyombo vya usafiri.
Maeneo ya maegesho
6.-(1) Halmashauri itatenga maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.
(2) Itakuwa ni marufuku kuegesha gari kandokando ya barabara, njia za waenda kwa miguu au kwenye mitaa au mahali pengine ambapo hapakutengwa kama eneo la maegesho.
(3) Magari yote yatakayoegeshwa katika maeneo maalum yaliyotengwa kama maeneo ya maegesho ya magari yatalipa ada ya maegesho kama itakavyooneshwa katika jedwali la Sheria Ndogo hizi.


Udhibiti wa magari yenye uzito mkubwa
7.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuendesha gari lenye uzito wa zaidi ya tani kumi katika barabara za Halmashauri isipokuwa kwa kibali maalum kwa viwango vitakavyopangwa na Halmashauri.
8. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari nje ya maeneo yaliyotengwa kama maegesho.

Matumizi ya vituo vya mabasi
9.-(1) Mabasi na daladala zinazojishughulisha na shughuli za usafirishaji wa abiria ndani na nje ya Halmashauri yatatakiwa kuanza safari zake katika kituo kikuu cha mabasi au katika kituo cha daladala na si vinginevyo.
(2) Mabasi, daladala na magari mengine yote yataanza safari kwa utaratibu maalum na kwa kuzingatia muda uliowekwa ili kuzuia msongamano wa magari kwenye vituo vya mabasi.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa daladala kukatisha safari kabla ya kuwafikisha abiria katika kituo cha mwisho au kuanza safari katikati ya njia kinyume na leseni.


Karakana na uoshaji wa magari
10. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote au kikundi cha watu kutengeneza magari kwenye kituo cha mabasi, taxi, au eneo la hifadhi ya barabara au kando ya barabara au kufanya shughuli hiyo katika eneo ambalo halikutengwa kwaajili hiyo.
Ujazaji wa mafuta
11. Itakuwa ni marufuku kwa dereva wa chombo chochote cha moto kinachotumika kusafirisha abiria kuongeza mafuta wakati abiria wakiwa ndani ya chombo hicho.
Udhibiti wa wapiga debe kwenye vituo vya magari
12.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote;-
  • kupiga debe au kubughudhi wasafiri katika vituo vya mabasi.
  • kukaa standi bila ya shughuli yoyote.
(2) Itakuwa ni wajibu wa madereva wote wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha kwamba wanavaa sare zao na vitambulisho wakati wote wawapo kwenye vituo vya mabasi.

Uuzaji wa bidhaa kandokando ya barabara
13. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kubeba, kutembeza au kuweka bidhaa kandokando ya barabara kwa madhumuni ya kuuza.
Kukama-ta chombo cha usafiri
14.-(1) Endapo mmiliki au dereva wa chombo cha usafirishaji atakataa au kukaidi kulipa ada au faini anayodaiwa Halmashauri itakamata chombo hicho na kikitunza katika maegesho ya Halmashauri mpaka mwenye gari atakapolipa faini au ada anayodaiwa.
(2) Chombo chochote cha usafirishaji kitakachokamatwa na kutunzwa au kuegeshwa katika maegesho ya Halmashauri kitalipiwa shilingi elfu tano (5,000/=) kwa siku ikiwa ni gharama ya kutunza chombo hicho mpaka siku mmiliki au dereva atakapokikomboa kwa kulipa ada, faini anayodaiwa na gharama za kutunza chombo hicho.

Makosa na adhabu
15. Mtu yeyote atakayekataa au atakayedharau au kushindwa kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi 50,000 au kifungo cha miezi 3 jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo.
16. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kumtoza faini mtu yeyote isiyozidi shilingi elfu thelathini (30,000/=) iwapo mkosaji atakiri kwa maandishi kutenda kosa hilo kwa kujaza fomu maalum iliyopo kwenye jedwali la pili la Sheria Ndogo hizi na kukubali kulipa faini anayodaiwa.
Kufifili-sha kosa

JEDWALI LA NAMBA 1

  • ushuru wa kituo cha mabasi 
Na
Aina ya chombo cha usafirishaji
Kiasi cha ada 
Muda 
1
Basi kubwa(  abiria 31 na zaidi)
Tshs 5,000/=
Kwa siku
2
Mabasi madogo (chini ya abiria 30
Tshs 2000/=
Kwa siku
3
Daladala
Tshs.2000/==
Kwa siku
4
Magari mengine yanayoingia na kutoka isipokuwa Taxi zilizosajiliwa kwa biashara hiyo.
Tshs 1000/=
Kwa siku
  •  
  • Ushuru wa maegesho 
  •  
Na
Aina ya chombo cha usafirishaji
Kiasi cha ada 
Muda 
1.
Lori tani 10 na zaidi
5000/=
Kwa siku
5
Lori chini ya tani 10
3000/=
Kwa siku
6
Pick up
2000/=
Kwa siku
7
Tax au gari nyingine ndogo
2000/=
Kwa siku

JEDWALI NAMBA 2

FOMU YA KUFIFILISHA KOSA

(Chini ya kifungu cha16 cha Sheria Ndogo hizi)

Mimi ………………………………………………………………………………… wa SLB……………………………………………………….…… ninaefanya biashara ya ……………………………………………………………………………… katika eneo la ………………………………… lililopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Nakiri kuwa leo tarehe ………………………………………Nilikiuka kifungu cha …………………cha Sheria Ndogo za (Ushuru wa Stendi na Maegesho ya Magari) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega za mwaka 2013. Kwa hiyo, kwa hiari yangu mwenyewe na bila kushawishiwa na mtu yeyote, nakubali kulipa faini iliyoainishwa kwenye Sheria Ndogo hizi iwapo Mkurugenzi atatekeleza madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 16 cha Sheria Ndogo hizi

Saini ………………………………………………………………

Mbele yangu………………………………………………… (jina)

Saini …………………………..……………………………………

Wadhifa ……………………………………………………………


TANGAZO LA SERIKALI NA. 210  la tarehe 29/05/2015 

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA

______

 

 (MAMLAKA ZA WILAYA)

______ 

 

(SURA YA 287)

______

 

Zimetungwa chini ya Kifungu cha 153

______

 

SHERIA NDOGO ZA (MATUMIZI YA BARABARA) ZA HALMASHAURI  YA WILAYA YA BUSEGA, 2014

 

Jina na mwanzo wa kutumika
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Matumizi ya Barabara) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega za Mwaka ,2014 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
 
Eneo la matumizi
2. Sheria Ndogo hizi zitaanza kutumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
 
Tafsiri
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo;
“Afisa Muidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi.
“Eneo la kati” maana yake ni eneo la kata ya Shangani
“Gari” maana yake ni chombo chochote kile cha moto chenye matairi kuanzia matatu.
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
‘’Kituo”maana yake ni kituo kilichosajiiwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha teksi,pikipiki,gari na lori.
“Kituo cha teksi” maana yake ni kituo maalum kilichoainishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha teksi.
“Kituo cha Basi” maana yake ni Kituo maalum kilichoainishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha mabasi yanayoshusha na kupakia abiria.
“Lori” maana yake ni gari yeyote ile ya mzigo yenye uzito kuanzia tani 3½ na kuendelea.
“Maegesho” maana yake ni sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuegesha magari.
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi.
“Mtaa” maana yake ni eneo lolote ndani ya Halmashauri na inajumuisha barabara.
 “Mkokoteni” maana yake ni chombo chochote kile chenye matairi kinachotumika kubeba mizigo ambacho hutembea kwa kusukumwa na binadamu au kukokotwa na mnyama.
“Teksi” maana yake ni gari yeyote iliyosajiliwa yenye uwezo wa kubeba abiria wasiozidi watano inayotumika kufanya biashara ya kusafirisha watu,ikiwa ni pamoja na bajaji na pikipiki.
“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
“Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, Kampuni, Taasisi au Shirika atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kwa niaba yake.
Maegesho
4.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari sehemu yoyote isipokuwa katika eneo lililotengwa maalum kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.




Usajili wa teksi
5.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa teksi kuhakikisha kwamba:-
  • gari lake limekaguliwa na Polisi na amelipia kodi zote zinazotakiwa na Serikali ikiwa ni pamoja na Kodi, ada na ushuru wa Halmashauri kabla ya kusajiliwa.
  • teksi yake imesajiliwa na Halmashauri kabla ya kuanza kufanya biashara ya kusafirisha abiria.

(2) Baada ya kusajiliwa, Halmashauri itatoa namba itakayobandikwa ubavuni mwa gari na kuainisha kituo ambacho teksi iliyosajiliwa itaegeshwa.
Usajili wa vituo vya teksi
6.-(1) Halmashauri itatenga na kutangaza maeneo maalum yatakayotumika kama vituo vya teksi.
(2) Halmashauri itaainisha idadi ya teksi zitakazoruhusiwa kuegeshwa katika kituo kimoja kwa wakati mmoja kwa kuzingatia ukubwa wa eneo.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha teksi      mahali ambapo hapakutengwa kwa ajili ya matumizi hayo.


Mikokoteni
7.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa mkokoteni kuusajili mkokoteni wake kwenye Kata anayofanyia biashara ya kuendesha Mkokoteni.
(2) Baada ya kusajiliwa Afisa Mtendaji wa Kata ataupatia mkokoteni huo namba na kuupangia eneo ambalo utatakiwa kuegeshwa.
(3) Kila mkokoteni utalipiwa ada ya usajili kama itakavyopangwa na Halmashauri.


Malori
8.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa lori lolote kuingia eneo la kati la Halmashauri bila kupata kibali cha Maandishi cha Halmashauri.
(2) Eneo la kati la Biashara la Wilaya (Central Bussiness District) kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi na kata ya Mjini, Ibinzamata, Lubaga, Kambarage, Ngokolo Ndala,Kitangili,Ndabezi na eneo lingine lolote abalo Halmashauri itaamua kufanya hivyo.

(3) Kibali cha kuingiza lori eneo la kati kitalipiwa ada ya Shilingi 30,000/= kwa kila safari.Halmashauri inaewza kubadili kiwango endapo itaona inafaa kufanya hivyo.
   
(4) Kibali kilichotolewa kitatumika kwa safari moja na kwa siku iliyotajwa kwenye kibali kwa kupitia barabara zile tu zitakazoainishwa ndani ya kibali hicho.
(5) Kibali cha kuingiza lori eneo la kati la Halmashauri kitatolewa na Halmashuari baada ya kupokea maombi ya maandishi kutoka kwa muombaji akiainisha lengo la kuingiza lori eneo la kati na mahali linapokwenda.


Uoshaji na utengenezaji wa magari
9.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuosha na au kutengeneza gari katika eneo la barabara, hifadhi ya barabara au eneo la wazi ambalo halijatengwa kwa matumizi ya hayo.
(2) Gari litalokutwa linaoshwa au kutengenezwa katika maeneo yasiyoruhusiwa litavutwa na kupelekwa katika Ofisi za Halmashauri na mmiliki wa gari hilo atatakiwa kulipa faini isiyozidi Shilingi Elfu Hamsini (50,000/=).
(3) Pamoja na faini iliyoainishwa chini ya kifungu kidogo cha (2) mmiliki wa gari lililovutwa atatakiwa pia kulipa shilingi elfu arobaini (15,000/=) ikiwa ni gharama za kuvuta gari, na shilingi elfu kumi na tano (15,000/=) kwa siku ikiwa ni gharama ya kutunza gari hilo, iwapo litatunzwa kwenye eneo la Halmashauri au kiwango cha gharama kitakachobainishwa na mmiliki wa eneo la kuhifadhia gari.



(4) Iwapo gari lililokamatwa litakaa katika ofisi za Halmashauri kwa zaidi ya siku kumi na nne (14) Halmashauri itauza gari hilo kwa mnada baada ya kuomba na kupata kibali cha mahakama ili kufidia gharama zake na kiasi cha fedha kitakachobaki atarudishiwa mmiliki wa gari.
Ufungaji wa barabara
10.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kufunga barabara kwa ajili ya sherehe, msiba au shughuli nyingine yeyote ile bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri. Kibali cha kufunga barabara kwa siku kitalipiwa shilingi laki moja (20,000/=)
(2) Mtu yeyote ambaye atafunga barabara bila idhini ya Halmashauri atakua ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozodi shillingi elfu Hamsini(50,000/=)au kifungo cha miezi sita jela au vyote viwili yani faini na kifungo.
Uwekaji wa vifaa vya ujenzi barabarani
11. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuweka au kumwaga vifaa vya ujenzi kama kokoto, mchanga, mawe na vifaa vinginevyo vya ujenzi katika eneo la hifadhi ya barabara au eneo lisiloruhusiwa bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri.
12.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukata barabara kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji, nyaya za umeme, simu au shughuli nyingine yeyote ile bila ya kuwa na kibali cha maandishi kutoka Halmashauri.
(2) Mtu yeyote atakayetaka kukata barabara kwa ajili ya kupitisha miundo mbinu mingine atatakiwa kulipa ada ya shilingi elfu Hamsini (50,000/=) kwa barabara ya lami, Shiling elfu arobaini (40,000/=) kwa kila mita ya erefu, kwa barabara za Changarawe Shilingi eflfu ishirini (20,000/=) na atatakiwa kurejesha barabara inayohusika kwenye hali yake ya awali kwa muda utakaotengwa na Halmashauri.
Kukata barabara


(3) Kibali cha kukata barabara kitadumu kwa muda wa siku saba (7) tu, na baada ya hapo tozo la faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (50,000/=) itatozwa kila siku ambayo muombaji atashindwa kurekebisha eneo lililokatwa na kurejesha barabara katika hali yake ya awali.
Barabara na uzito wa magari
13.-(1) Kila barabara itakua na uzito wa magari yanayoruhusiwa kupitisha kataka barabara hiyo.Halmashauri itaweka katiak kila barabara bango lianaloonyesha uzito wa gari wa magari yanayoruhusiwa kupitishwa katika barabara hiyo.
(2) Hakuna gari lolote litakaroruhusiwa kupitishwa katika barabara yoyote iwapo uzito wa gari hilo utakuwa mkubwa kuliko uzito wa magari yaliyoruhusiwa kupitishwa katika barabara hiyo.
(3) Mtu yoyote atakayepitisha gari katika barabara yoyote kinyume na Kifungu cha 15(2) atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shillingi elfu hamsini(50,000/=) pamoja na gharama za uharibifu wa barabara zilizothaminiwa na Halmashauri au kifungo kisichiozidi miezi sita jela au vyote kwa pamoja yani faini na kifumgo.
Ujenzi kwenye eneo la Barabara
14.-(1) Mtu yoyote ambaye atakua amejenga au ameweka jengo lolote katika eneo la barabara mara baada ya Sheria Ndogo hii kuanza atatakiwa kupewa notisi ya kumi na nne.
(2) Iwapo baada ya kupewa notisi ya siku kumi na nne mtu huyo ameshindwa kutekeleza amri hiyo Halamashauri itabomoa na kimpelekea gharama za ubomoaji huo mhusika.
Uzibuaji wa mitaro
15.-(1) Pale ambapo njia ya kiuingilia kwenye nyumba imejengwa kwa namna ambayo inaweza kuziba mitaro iliyo kwenye barabara na kuzuia mtirirko wa maji kwenye mitaro hiyo,Mkurugenzi au Afisa Muidhiniwa anaweza kumtumia notisi mtu anayemiliki jengo hilo aweke culvert au bomba eneo hilo kama itakavyoelezwa kwenye notisi hiyo kwa lengo la kuondoa tatizo la uzibaji wa mitaro husika
(2) Endapo kuna njia ya kuingia kwenye makazi na pamewekewa culvert au bomba mwenye jengo husika au makazi kwenye jengo hilo atatakiwa kuliacha wazi eneo hilo bila kuliziba na kuzuia maji kupita na atahakikisha eneo hilo liko kwenye hali nzuri na endapo atakiuka masharti ya  fungu hili,Halmashauri itafanya kazi hiyo na kisha kimtaka mhusika alipie gharama ambazo Halmashauri itakua imetumia.
(3) Itakua ni jukumu la mwenye nyumba kuhakikisha mtaro unaozunguka au uliopo mbele ya nyumba au jengo lake la biashara unakua katika hali ya usafi wakati wote.  
 
Majengo yanayojitokeza
16. Hairuhusiwi kwa mtu yoyote, bila kupata kibali maalum kutoka Halmashauri, kujenga,kuning’iniza au kuweka jengo lolote au kusababisha jengo kuingia katika eneo la barabara.
Kufanya biashara
17.-(1) Hairuhusiwi kwa mtu yoyote kufanya biashara katika eneo la barabara.
 
(3) Iwapo Halmashauri itagundua mtu yoyote ameweka bidhaa zake katika eneo la hifadhi ya barabara,mtu huyo atapewa notisi ya siku kumi na nne uli kuondoa bidhaa zake na asipofanya hivyo,Halmashauri itaondoa bidhaa hizo na kumtaka alipe gharama za uondoaji wa bidhaa hizo.
   
Uteuzi wa wakala
18. Halmashauri itakuwa na uwezo wa kumteua Wakala kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kwa niaba yake.
Makosa
19. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi iwapo:-
ataegesha gari katika sehemu isiyoruhusiwa;
atafanya biashara ya teksi kwa kutumia gari isiyosajiliwa au kuegesha kwenye kituo cha teksi;
ataendesha mkokoteni bila ya kusajili katika Kata;
ataendesha mkokoteni katika barabara ambayo hajaruhusiwa;
ataendesha lori bila kibali katika eneo la kati la Halmashauri;
ataosha gari katika eneo la barabara, hifadhi ya barabara au eneo la wazi ambalo matumizi yake siyo ya kuegesha gari;
atafunga barabara kwa shughuli za sherehe, msiba au shughuli nyingine yoyote bila kibali cha maandishi cha Halmashauri;
atakata barabara bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri.
ataweka au kumwaga vifaa vya ujenzi kwenye barabara, hifadhi ya barabara au eneo lisiloruhusiwa.
atamzuia Afisa au Wakala wa Halmashauri kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hizi;
Adhabu
20. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi atatozwa faini ya isiyozidi shilingi elfu hamisni (50,000/=) au kifungo kisichozidi miezi mitatu Jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo.
Kufifilisha kosa
21. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kumtoza faini mtu yeyote isiyozidi elfu hamsini (50,000/=) iwapo mkosaji atakiri kwa maandishi kutenda kosa hilo kwa kujaza fomu maalum iliyopo kwenye jedwali la Sheria Ndogo hizi na kukubali kulipa faini anayodaiwa.

 

 

 

JEDWALI LA KWANZA

 

                     

Na.
Ada ya kukata barabara
Ada
1.
Lami
500,000/= kwa kibali
2.
Barabara ya changrawe
150,000/=kwa kibali
3.
Faini ya kila siku ya kuchelewa kurudishia barabara katika haliyake ya awali
50,000/=kwa kibali
4.
Kulaza Lori katika sehemu iliyotengwa
5,000/= kwa siku
5.
Kibali cha kufunga barabara kwa siku
30,000/= kwa siku

 

JEDWALI LA PILI

FOMU YA KUFIFILISHA KOSA

(Chini ya kifungu cha 16 cha Sheria Ndogo hizi)

Mimi ………………………………………………………………………………… wa SLP …………………………………………….…………………… ninaefanya biashara ya ………………………………………..……………………………… katika eneo la ………………………..…………………… lililopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Nakiri kuwa leo tarehe ………………………………………Nilikiuka kifungu cha …………………………………………………cha Sheria Ndogo za (Matumizi ya Barabara) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega za Mwaka 2014. Kwa hiyo, kwa hiari yangu mwenyewe na bila kushawishiwa na mtu yeyote, nakubali kulipa faini iliyoainishwa kwenye Sheria Ndogo hizi iwapo Mkurugenzi atatekeleza madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 16 cha Sheria Ndogo hizi.

Saini …………………………………………………………

Mbele yangu………………………………………………… (jina)

Saini ……………………………………….…………………

Wadhifa ………………………………….…………………


TANGAZO LA SERIKALI NA. 210  la tarehe 29/05/2015

 

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA

______

 

 (MAMLAKA ZA WILAYA)

______ 

 

(SURA YA 287)

______

 

Zimetungwa chini ya Kifungu cha 153

______

 

SHERIA NDOGO ZA (MATUMIZI YA BARABARA) ZA HALMASHAURI  YA WILAYA YA BUSEGA, 2014

 

Jina na mwanzo wa kutumika
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Matumizi ya Barabara) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega za Mwaka ,2014 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
 
Eneo la matumizi
2. Sheria Ndogo hizi zitaanza kutumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
 
Tafsiri
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo;
“Afisa Muidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi.
“Eneo la kati” maana yake ni eneo la kata ya Shangani
“Gari” maana yake ni chombo chochote kile cha moto chenye matairi kuanzia matatu.
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
‘’Kituo”maana yake ni kituo kilichosajiiwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha teksi,pikipiki,gari na lori.
“Kituo cha teksi” maana yake ni kituo maalum kilichoainishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha teksi.
“Kituo cha Basi” maana yake ni Kituo maalum kilichoainishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha mabasi yanayoshusha na kupakia abiria.
“Lori” maana yake ni gari yeyote ile ya mzigo yenye uzito kuanzia tani 3½ na kuendelea.
“Maegesho” maana yake ni sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuegesha magari.
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi.
“Mtaa” maana yake ni eneo lolote ndani ya Halmashauri na inajumuisha barabara.
 “Mkokoteni” maana yake ni chombo chochote kile chenye matairi kinachotumika kubeba mizigo ambacho hutembea kwa kusukumwa na binadamu au kukokotwa na mnyama.
“Teksi” maana yake ni gari yeyote iliyosajiliwa yenye uwezo wa kubeba abiria wasiozidi watano inayotumika kufanya biashara ya kusafirisha watu,ikiwa ni pamoja na bajaji na pikipiki.
“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
“Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, Kampuni, Taasisi au Shirika atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kwa niaba yake.
Maegesho
4.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha gari sehemu yoyote isipokuwa katika eneo lililotengwa maalum kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.




Usajili wa teksi
5.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa teksi kuhakikisha kwamba:-
  • gari lake limekaguliwa na Polisi na amelipia kodi zote zinazotakiwa na Serikali ikiwa ni pamoja na Kodi, ada na ushuru wa Halmashauri kabla ya kusajiliwa.
  • teksi yake imesajiliwa na Halmashauri kabla ya kuanza kufanya biashara ya kusafirisha abiria.

(2) Baada ya kusajiliwa, Halmashauri itatoa namba itakayobandikwa ubavuni mwa gari na kuainisha kituo ambacho teksi iliyosajiliwa itaegeshwa.
Usajili wa vituo vya teksi
6.-(1) Halmashauri itatenga na kutangaza maeneo maalum yatakayotumika kama vituo vya teksi.
(2) Halmashauri itaainisha idadi ya teksi zitakazoruhusiwa kuegeshwa katika kituo kimoja kwa wakati mmoja kwa kuzingatia ukubwa wa eneo.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuegesha teksi      mahali ambapo hapakutengwa kwa ajili ya matumizi hayo.


Mikokoteni
7.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa mkokoteni kuusajili mkokoteni wake kwenye Kata anayofanyia biashara ya kuendesha Mkokoteni.
(2) Baada ya kusajiliwa Afisa Mtendaji wa Kata ataupatia mkokoteni huo namba na kuupangia eneo ambalo utatakiwa kuegeshwa.
(3) Kila mkokoteni utalipiwa ada ya usajili kama itakavyopangwa na Halmashauri.


Malori
8.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa lori lolote kuingia eneo la kati la Halmashauri bila kupata kibali cha Maandishi cha Halmashauri.
(2) Eneo la kati la Biashara la Wilaya (Central Bussiness District) kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi na kata ya Mjini, Ibinzamata, Lubaga, Kambarage, Ngokolo Ndala,Kitangili,Ndabezi na eneo lingine lolote abalo Halmashauri itaamua kufanya hivyo.

(3) Kibali cha kuingiza lori eneo la kati kitalipiwa ada ya Shilingi 30,000/= kwa kila safari.Halmashauri inaewza kubadili kiwango endapo itaona inafaa kufanya hivyo.
   
(4) Kibali kilichotolewa kitatumika kwa safari moja na kwa siku iliyotajwa kwenye kibali kwa kupitia barabara zile tu zitakazoainishwa ndani ya kibali hicho.
(5) Kibali cha kuingiza lori eneo la kati la Halmashauri kitatolewa na Halmashuari baada ya kupokea maombi ya maandishi kutoka kwa muombaji akiainisha lengo la kuingiza lori eneo la kati na mahali linapokwenda.


Uoshaji na utengenezaji wa magari
9.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuosha na au kutengeneza gari katika eneo la barabara, hifadhi ya barabara au eneo la wazi ambalo halijatengwa kwa matumizi ya hayo.
(2) Gari litalokutwa linaoshwa au kutengenezwa katika maeneo yasiyoruhusiwa litavutwa na kupelekwa katika Ofisi za Halmashauri na mmiliki wa gari hilo atatakiwa kulipa faini isiyozidi Shilingi Elfu Hamsini (50,000/=).
(3) Pamoja na faini iliyoainishwa chini ya kifungu kidogo cha (2) mmiliki wa gari lililovutwa atatakiwa pia kulipa shilingi elfu arobaini (15,000/=) ikiwa ni gharama za kuvuta gari, na shilingi elfu kumi na tano (15,000/=) kwa siku ikiwa ni gharama ya kutunza gari hilo, iwapo litatunzwa kwenye eneo la Halmashauri au kiwango cha gharama kitakachobainishwa na mmiliki wa eneo la kuhifadhia gari.



(4) Iwapo gari lililokamatwa litakaa katika ofisi za Halmashauri kwa zaidi ya siku kumi na nne (14) Halmashauri itauza gari hilo kwa mnada baada ya kuomba na kupata kibali cha mahakama ili kufidia gharama zake na kiasi cha fedha kitakachobaki atarudishiwa mmiliki wa gari.
Ufungaji wa barabara
10.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kufunga barabara kwa ajili ya sherehe, msiba au shughuli nyingine yeyote ile bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri. Kibali cha kufunga barabara kwa siku kitalipiwa shilingi laki moja (20,000/=)
(2) Mtu yeyote ambaye atafunga barabara bila idhini ya Halmashauri atakua ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozodi shillingi elfu Hamsini(50,000/=)au kifungo cha miezi sita jela au vyote viwili yani faini na kifungo.
Uwekaji wa vifaa vya ujenzi barabarani
11. Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuweka au kumwaga vifaa vya ujenzi kama kokoto, mchanga, mawe na vifaa vinginevyo vya ujenzi katika eneo la hifadhi ya barabara au eneo lisiloruhusiwa bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri.
12.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukata barabara kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji, nyaya za umeme, simu au shughuli nyingine yeyote ile bila ya kuwa na kibali cha maandishi kutoka Halmashauri.
(2) Mtu yeyote atakayetaka kukata barabara kwa ajili ya kupitisha miundo mbinu mingine atatakiwa kulipa ada ya shilingi elfu Hamsini (50,000/=) kwa barabara ya lami, Shiling elfu arobaini (40,000/=) kwa kila mita ya erefu, kwa barabara za Changarawe Shilingi eflfu ishirini (20,000/=) na atatakiwa kurejesha barabara inayohusika kwenye hali yake ya awali kwa muda utakaotengwa na Halmashauri.
Kukata barabara


(3) Kibali cha kukata barabara kitadumu kwa muda wa siku saba (7) tu, na baada ya hapo tozo la faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (50,000/=) itatozwa kila siku ambayo muombaji atashindwa kurekebisha eneo lililokatwa na kurejesha barabara katika hali yake ya awali.
Barabara na uzito wa magari
13.-(1) Kila barabara itakua na uzito wa magari yanayoruhusiwa kupitisha kataka barabara hiyo.Halmashauri itaweka katiak kila barabara bango lianaloonyesha uzito wa gari wa magari yanayoruhusiwa kupitishwa katika barabara hiyo.
(2) Hakuna gari lolote litakaroruhusiwa kupitishwa katika barabara yoyote iwapo uzito wa gari hilo utakuwa mkubwa kuliko uzito wa magari yaliyoruhusiwa kupitishwa katika barabara hiyo.
(3) Mtu yoyote atakayepitisha gari katika barabara yoyote kinyume na Kifungu cha 15(2) atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shillingi elfu hamsini(50,000/=) pamoja na gharama za uharibifu wa barabara zilizothaminiwa na Halmashauri au kifungo kisichiozidi miezi sita jela au vyote kwa pamoja yani faini na kifumgo.
Ujenzi kwenye eneo la Barabara
14.-(1) Mtu yoyote ambaye atakua amejenga au ameweka jengo lolote katika eneo la barabara mara baada ya Sheria Ndogo hii kuanza atatakiwa kupewa notisi ya kumi na nne.
(2) Iwapo baada ya kupewa notisi ya siku kumi na nne mtu huyo ameshindwa kutekeleza amri hiyo Halamashauri itabomoa na kimpelekea gharama za ubomoaji huo mhusika.
Uzibuaji wa mitaro
15.-(1) Pale ambapo njia ya kiuingilia kwenye nyumba imejengwa kwa namna ambayo inaweza kuziba mitaro iliyo kwenye barabara na kuzuia mtirirko wa maji kwenye mitaro hiyo,Mkurugenzi au Afisa Muidhiniwa anaweza kumtumia notisi mtu anayemiliki jengo hilo aweke culvert au bomba eneo hilo kama itakavyoelezwa kwenye notisi hiyo kwa lengo la kuondoa tatizo la uzibaji wa mitaro husika
(2) Endapo kuna njia ya kuingia kwenye makazi na pamewekewa culvert au bomba mwenye jengo husika au makazi kwenye jengo hilo atatakiwa kuliacha wazi eneo hilo bila kuliziba na kuzuia maji kupita na atahakikisha eneo hilo liko kwenye hali nzuri na endapo atakiuka masharti ya  fungu hili,Halmashauri itafanya kazi hiyo na kisha kimtaka mhusika alipie gharama ambazo Halmashauri itakua imetumia.
(3) Itakua ni jukumu la mwenye nyumba kuhakikisha mtaro unaozunguka au uliopo mbele ya nyumba au jengo lake la biashara unakua katika hali ya usafi wakati wote.  
 
Majengo yanayojitokeza
16. Hairuhusiwi kwa mtu yoyote, bila kupata kibali maalum kutoka Halmashauri, kujenga,kuning’iniza au kuweka jengo lolote au kusababisha jengo kuingia katika eneo la barabara.
Kufanya biashara
17.-(1) Hairuhusiwi kwa mtu yoyote kufanya biashara katika eneo la barabara.
 
(3) Iwapo Halmashauri itagundua mtu yoyote ameweka bidhaa zake katika eneo la hifadhi ya barabara,mtu huyo atapewa notisi ya siku kumi na nne uli kuondoa bidhaa zake na asipofanya hivyo,Halmashauri itaondoa bidhaa hizo na kumtaka alipe gharama za uondoaji wa bidhaa hizo.
   
Uteuzi wa wakala
18. Halmashauri itakuwa na uwezo wa kumteua Wakala kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kwa niaba yake.
Makosa
19. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi iwapo:-
ataegesha gari katika sehemu isiyoruhusiwa;
atafanya biashara ya teksi kwa kutumia gari isiyosajiliwa au kuegesha kwenye kituo cha teksi;
ataendesha mkokoteni bila ya kusajili katika Kata;
ataendesha mkokoteni katika barabara ambayo hajaruhusiwa;
ataendesha lori bila kibali katika eneo la kati la Halmashauri;
ataosha gari katika eneo la barabara, hifadhi ya barabara au eneo la wazi ambalo matumizi yake siyo ya kuegesha gari;
atafunga barabara kwa shughuli za sherehe, msiba au shughuli nyingine yoyote bila kibali cha maandishi cha Halmashauri;
atakata barabara bila kibali cha maandishi kutoka Halmashauri.
ataweka au kumwaga vifaa vya ujenzi kwenye barabara, hifadhi ya barabara au eneo lisiloruhusiwa.
atamzuia Afisa au Wakala wa Halmashauri kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hizi;
Adhabu
20. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi atatozwa faini ya isiyozidi shilingi elfu hamisni (50,000/=) au kifungo kisichozidi miezi mitatu Jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo.
Kufifilisha kosa
21. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kumtoza faini mtu yeyote isiyozidi elfu hamsini (50,000/=) iwapo mkosaji atakiri kwa maandishi kutenda kosa hilo kwa kujaza fomu maalum iliyopo kwenye jedwali la Sheria Ndogo hizi na kukubali kulipa faini anayodaiwa.

 

 

 

JEDWALI LA KWANZA

 

                     

Na.
Ada ya kukata barabara
Ada
1.
Lami
500,000/= kwa kibali
2.
Barabara ya changrawe
150,000/=kwa kibali
3.
Faini ya kila siku ya kuchelewa kurudishia barabara katika haliyake ya awali
50,000/=kwa kibali
4.
Kulaza Lori katika sehemu iliyotengwa
5,000/= kwa siku
5.
Kibali cha kufunga barabara kwa siku
30,000/= kwa siku

 

JEDWALI LA PILI

FOMU YA KUFIFILISHA KOSA

(Chini ya kifungu cha 16 cha Sheria Ndogo hizi)

Mimi ………………………………………………………………………………… wa SLP …………………………………………….…………………… ninaefanya biashara ya ………………………………………..……………………………… katika eneo la ………………………..…………………… lililopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Nakiri kuwa leo tarehe ………………………………………Nilikiuka kifungu cha …………………………………………………cha Sheria Ndogo za (Matumizi ya Barabara) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega za Mwaka 2014. Kwa hiyo, kwa hiari yangu mwenyewe na bila kushawishiwa na mtu yeyote, nakubali kulipa faini iliyoainishwa kwenye Sheria Ndogo hizi iwapo Mkurugenzi atatekeleza madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 16 cha Sheria Ndogo hizi.

Saini …………………………………………………………

Mbele yangu………………………………………………… (jina)

Saini ……………………………………….…………………

Wadhifa ………………………………….…………………


Tangazo la Serikali Na. 211 la Tarehe 29/05/2015 

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)

________

(SURA YA 287)

________

 

SHERIA NDOGO

_________

 

(Zimetungwa chini ya  kifungu  cha 153)

_________ 

 

SHERIA NDOGO YA (ULAZIMA WA KULIMA EKARI MBILI YA MAZAO YANAOSTAHIMILI UKAME) YA HAKMASHAURI YA WILAYA YA BUSEGA MWAKA, 2015



  • Jina na Tarehe ya kuanza kutumika


    Sheria ndogo hizi ziitwe Sheria Ndogo za (ulazima wa Kulima ekari mbili ya mazao yanayostahimili ukame) za Halmashauri ya wilaya ya Busega za Mwaka ,2014.


    Matumizi


    Sheria  Ndogo hizi  zitatumika  katika eneo lote  lililo katika eneo la mamlaka ya Halmashauri  ya Wilaya wa  Busega.


    Tafsiri


    Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa itakavyofafanuliwa au kuelezwa vinginevyo na Sheria yoyote andishi.

    ‘’Afisa  Mwidhinishwa’’ maana yake  ni Mkurugenzi, Afisa Mtendaji  wa Kata au mtumishi  yeyote  wa Halmashauri  ambaye anatekeleza  kazi na majukumu  ya Mkurugenzi au Afisa  Mtendaji  wa Kata

    ‘’Afisa  Mtendaji” maana yake ni Afisa  Mtendaji  wa Kata, kijiji au  mtumishi  yeyote  wa  Halmashauri  ambaye  atakuwa  anakaimu  kwa  ajili ya kutekeleza  majukumu   na madaraka ya Afisa Mtendaji  wa Kata husika.

    ‘’Kamati ya Kata’’ maana yake ni Kamati ya Maendeleo ya Kata husika

    ‘’Katibu‘’ maana yake ni Katibu  wa Baraza la Kata aliyeteuliwa na kuidhinishwa na Halmashauri  kwa ajili ya kufanya  shughuli  za Katibu  katika  Baraza la Kata.

    “Mazao ya chakula” maana yake ni Mtama, Uwele, Mahindi, Mpunga, karanga, Viazi vitamu, Muhogo na mazao mengine yanayoliwa wilayani kwa madhumuni ya chakula

    . “Mazao ya chakula” maana yake ni Mtama, Uwele, Mahindi, Mpunga, karanga, Viazi vitamu, Muhogo na mazao mengine yanayoliwa wilayani kwa madhumuni ya chakula

    ”Mazao yanayovumilia ukame” Maana yake ni Mtama, Uwele, Dengu, viazi vitamu, na Mhogo

    ”Magonjwa ya mimea “ maana yake ni ugonjwa au magonjwa yoyote yanayodhuru mimea na kuidhoofisha, kuinuwa au kuifanya isizae au kutoa mazao au matunda kwa ukamilifu.

    Mkazi” maana yake ni mkulima yeyote aliye na makazi  na anayeishi katika eneo lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya wilaya ya Busega kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja isipokuwa si:

    • Mtu aliyechini ya umri wa miaka 18,
    • Mtu asiyeweza kufanyakazi kwa sababu  ya uzee ugonjwa na ulemavu.
    • Mtu aliye na kazi ya kudumu ya kuajiriwa,
    • Mwanafunzi wa shule ya msingi, Sekondari au Chuo.
  • ‘’Mkurugenzi’’maana yake ni Mkurugenzi Halmshauri ya Wilaya ya  Busega.

    ‘’Halmashauri ‘’ maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

    “Wadudu waharibifu” maana yake ni wadudu wanaodhuru au kuambukiza magonjwa kwa mazao shambani/ghalani na hivyo kupunguza uzalishaji, ubora na thamani ya mazao.



    • Wajibu wa kila kaya au mkazi


      Kila kaya ya mkazi ni lazima kulima mazao ya chakula,yanayo stahamili    ukame ekali zisizopungua mbili na kutunza kitaalam shamba hilo,  


      • Mkulima kufuata kanuni bora za kilimo


        Kila mkulima anapaswa kutunza shamba lake la mazao ya biashara au chakula kwa kulipalilia, kutumia madawa na mbolea za asili au za viwandani, kuuvuna mazao mapema yawapo tayari na kuyatunza au kuyahifadhi kwa mujibu wa kanuni bora za kilimo.


        • Kujiwekea chakula kila mwaka


          Kila Kaya inawajibika kujiwekea chakula cha kutosha hadi msimu unaofuata wa mavuno ya chakula na ni makosa kuuza, kutumia kwa kupikia pombe au kwa shughuli ya ngoma sehemu kubwa ya chakula na kuiacha familia katika njaa.


          • Ukaguzi wa shamba


            Afisa mwenye mamlaka aweze kuingia katika shamba lolote la mkulima wakati wowote kati ya saa 12:00 asubuhi na saa 12:00 jioni kwa ajili ya ukaguzi wa madhumuni ya utekelezaji wa sheria ndogo hizi.


            • Adhabu


               Mtu yeyote atakayekataa au kushindwa kutekeleza sheria ndogo hizi, atakuwa ametenda kosa na akifikishwa mahakamani na kupatikana na hatia adhabu yake itakuwa faini isiyopungua shilingi thelathini na isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungu kisichopungua miezi miwili na kisichozidi miezi sita au adhabu zote mbili yaani faini na kifungo kwa pamoja


Tangazo la Serikali Na. 213 la Tarehe 29/05/2015

 

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)

______

 

(SURA YA 287)

______

SHERIA NDOGO

______

Zimetungwa chini ya kifungu cha 153

______

SHERIA NDOGO ZA (UANZISHAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSEGA ZA MWAKA 2011

 

      

Jina na mwanzo wa kuanza kutumika
Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega 2011 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
 
Matumizi
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
 
 Tafsiri
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo:-
“Ada ya Mtumiaji” maana yake ni ada inayotozwa na Hospitali, kituo cha afya au zahanati, kwa ajili ya huduma ya afya inayotolewa kwa mtumiaji;
“Asasi” maana yake ni pamoja na shule, vyuo, vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria au asasi yoyote itakayokuwa imekubaliwa na kuidhinishwa na Bodi;
Sura ya
    287
“Bodi’’ maana yake ni Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri iliyoundwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287;
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega;
“Huduma za afya” maana yake ni huduma zote za afya zinazotolewa na hospitali za Serikali  na watu binafsi, na zinajumuisha huduma nyingine za afya zilizoanzishwa kwa madhumuni ya kutoa huduma za afya ikiwa ni pamoja na vituo vya afya na Zahanati;
“Kadi” maana yake ni kadi itakayotolewa na Bodi kwa mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii.
“Kaya” maana yake ni :
  • mama, baba, watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane;
  • mwanachama yeyote aliyefikisha umri wa miaka kumi na nane au zaidi na awe na motto au bila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nane;
  • Taasisi au asasi yoyote.
“Kituo cha huduma kilichoteuliwa” maana yake ni kituo kinachotoa huduma za afya na ni pamoja na kituo chochote kilichoanzishwa au kinachoendeshwa kwa malengo ya kutoa huduma za afya kiwe kinamilikiwa na Halmashauri, Serikali, asasi ya kidini, mtu au watu binafsi ambacho kinahusika na mfuko wa Afya ya Jamii.
“Malipo ya huduma” maana yake ni malipo yanayotozwa na kituo cha tiba, kilichoteuliwa kwa watu ambao sio wanachama, wanapopatiwa huduma za afya katika kituo hicho;
“Mchango au ada ya mwanachama” maana yake ni mchango wa hiari utakaotolewa na wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii;
“Mfuko au Mfuko wa Afya ya Jamii”(CHF) maana yake ni mfuko wa afya ya jamii wa tiba kwa kadi ulioanzishwa chini ya Sheria Ndogo hizi.
“Mganga Mkuu wa Wilaya” maana yake ni daktari ambaye ni msimamizi mkuu wa shughuli za huduma za afya katika Halmashauri.
“Mwanachama” maana yake ni kaya inayochangia kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii;
“Tele kwa Tele” maana yake ni mkataba unaoeleza wajibu wa Halmashauri na wajibu wa Wizara unaoeleza wajibu wa Halmashauri na wajibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii.
“Wizara” maana yake ni Wizara yenye dhamana ya masuala ya afya.

Mfuko wa Afya ya Jamii  wa Tiba kwa Kadi
4.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa  Afya wa Jamii ambao ni mfuko wa hiari wenye lengo la kutoa huduma za afya, ambapo kaya zitakuwa zikilipia huduma hizo na Serikali itatoa mchango wake wa fedha kama jazilio kwa mchango kutoka kwenye kaya; (Tele kwa Tele).
 

 
(2) Matumizi ya fedha yatafanywa na kusimamiwa na Bodi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.
 

Madhu-muni ya Mfuko
5. Madhumuni ya Mfuko yatakuwa ni:
kutafuta vyanzo vya fedha kutoka katika jamii kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya kwa wanachama;
kutoa huduma bora za afya zinazopatikana kwa kutumia mipango endelevu; na
kuboresha huduma za afya katika jamii kwa kugawanya madaraka na kuzipa nguvu jamii katika kufanya maamuzi na kuchangia katika masuala yanayohusu afya zao.

Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii
6.-(1) Kutakuwa na Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii wa Halmashauri atakayeteuliwa na Mkurugenzi baada ya kupokea mapendekezo kutoka Timu ya Wataalam wa Afya wa Halmashauri (CHMT).
(2) Majukumu ya Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii yatakuwa kama ifuatavyo;-




kufuatilia, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya ya Jamii kwa kiwango kati ya Halmashauri, Jamii na wadau mbalimbali kwa ushirikiano na mhasibu wa Mfuko; na
kuandaa taarifa za Mfuko wa Afya ya Jamii za robo mwaka na mwaka kwa kushirikiana na mhasibu wa Mfuko, pamoja na majukumu mengine atakayopangiwa na Halmashauri.

Muundo wa Bodi
7.-(1) Bodi itakuwa na wajumbe wafuatao;-
Wawakilishi wanne wa watumiaji huduma za afya kati yao wawili ni lazima wawe ni wanawake.
Mwakilishi mmoja kutoka watoa huduma za Afya binafsi bila faida na
Mwakilishi mmoja kutoka watoa huduma za Afya kwa faida waliochaguliwa na Halmashauri kutoka vituo vya kutolea huduma za afya binafsi kwa faida waliochaguliwa miongoni mwao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji.
Afisa Mipango wa Halmashauri
Mganga Mkuu wa Halmashauri ambaye atakuwa Katibu wa Bodi.
Mwakilishi mmoja kutoka Hospitali na Mwakilishi mmoja kutoka Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Mkoa.


(2) Mwenyekiti wa Bodi atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika aya (a)-(c) hapo juu.
(3) Wajumbe waliotajwa katika aya (a)-(d) mbali na wajumbe waliotajwa katika aya (e)- (g) za kifungu kidogo cha (1) watakuwa  na haki ya kupiga kura katika maamuzi ya Bodi.



Kazi za Bodi
8. Ili kufanikisha malengo yake makuu, Bodi itakuwa na kazi zifuatazo:-
  • itasimamia masuala na shughuli zote zinazohusu Mfuko wa Afya ya Jamii;
itafanya kazi kwa kushauriana na Timu ya Uendeshaji ya Huduma za Afya  ya Halmashauri na kuhakikisha kuwa huduma ya afya inayotolewa ni bora na ya kitaalamu;
kukusanya na kusimamia mapato ya Mfuko wa Afya ya Jamii.
kupendekeza kwa Halmashauri watu wanaostahili kusamehewa kutoa mchango kwenye Mfuko
kuweka malengo ya Mfuko.
kupitia ripoti na taarifa kutoka Kamati ya Afya ya Kata au chanzo kingine chochote.
kuratibu makusanyo, matumizi na kudhibiti mapato na;
kupanga mipango ya afya ya mwaka kwa ajili ya kuthibitishwa na Halmashauri.
kupanua na kuongeza utoaji  wa huduma za afya kwa wanachama kulingana na mapato ya mfuko;
Bodi katika kutekeleza majukumu yake, itapokea na kutekeleza maagizo ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu

Sifa za wajumbe wa bodi
9. Mjumbe wa Bodi atakuwa na sifa zifuatazo;-
  • awe Raia wa Tanzania isipokuwa kwa wawakilishi kutoka katika Taasisi zisizo za kiserikali.
awe na umri si chini ya miaka ishirini na tano na si zaidi ya  miaka sabini;
awe amehitimu elimu ya sekondari na kuendelea;
awe na uzoefu na amewahi kuonyesha uwezo wake wa kuongoza katika shughuli za huduma jamii;
awe na sifa za uongozi; na
asiwe na wadhifa wowote wa kisiasa kupitia chama chochote cha siasa.
awe mwanachama hai wa Mfuko wa Afya ya Jamii au Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Muda wa kukaa madara-kani
10.-(1) Mjumbe wa Bodi atakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe aliyochaguliwa na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitatu tu.
(2) Endapo nafasi yeyote ya mjumbe wa Bodi itaachwa wazi kwa sababu ya kifo, kujiuzulu kukiuka maadili ya kazi au ulemavu utakaomfanya ashindwe kushiriki kikamilifu kama mjumbe au kwa sababu nyingine yeyote ile, mjumbe mwingine atachaguliwa kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2), haitaruhusiwa kuchagua mjumbe mwingine iwapo kipindi kilichobaki ni chini ya miezi sita.





Mikuta-no ya Bodi
11.-(1) Mikutano ya kawaida ya Bodi itaitishwa na Mwenyekiti kila robo mwaka.
(2) Ikiwa kuna umuhimu, mwenyekiti anaweza akaitisha kikao cha dharula kulingana na mahitaji maalumu.



Uwajibi-kaji wa Bodi.
12. Bodi itawajibika kwa Halmashauri kupitia Kamati husika.

Vyanzo vya Mapato
13. Vyanzo vya mapato ya Mfuko vitatokana na:-
fedha zote zitakazopokelewa kutokana na  michango ya wanachama;
ruzuku kutoka kwenye Halmashauri, Serikali Kuu, na wahisani mbalimbali toka ndani na nje ya Halmashauri;
michango ya watu binafsi wanaoishi ndani na nje ya Halmashauri
malipo ya fedha ya wasiokuwa wanachama wa Mfuko kwa kupata huduma ya afya.
  • ushuru utakaotozwa na Halmshauri kutoka vyanzo mbalimbali na kutengwa kwa ajili ya Mfuko; na
  • fedha zozote halali ambazo Mfuko unaweza kupata toka   mahali pengine popote.
  • Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
  • fedha zozote halali ambazo mfuko unaweza kupata kutoka mahali pengine popote
 

Akaunti ya mfuko wa Bodi na watiaji saini
14.-(1) Kutakuwepo na akaunti maalumu itakayotumika na Halmashauri ambayo fedha zote zitakazokusanywa kwa ajili ya Mfuko zitahifadhiwa na kutolewa.
(2) Malipo yataidhinishwa na Mkurugenzi kwa kufuata taratibu za kanuni za fedha za Halmashauri.
(3) Watia saini wa akaunti  ya Mfuko watachaguliwa na Bodi na watakuwa ni mmoja kutoka kundi “A” na “B” na kwa namna yoyote  hakuna pesa zitakazotolewa kwenye akaunti ya mfuko bila saini ya mmojawapo kutoka kundi “A” na “B”.
(4) Watia saini kwenye hundi za Mfuko watakuwa kama ifuatavyo:-
  • Mwenyekiti wa Bodi na mjumbe mmoja wa Bodi ambao watakuwa Kundi “A”
  • Katibu wa Bodi (Mganga mkuu) na Mweka Hazina wa Halmashauri watakuwa Kundi “B”
(5) Kila baada ya miezi mitatu, Bodi itakuwa inatoa taarifa ya akaunti ya Mfuko kwa Halmashauri;
(6) Akaunti ya Mfuko itakaguliwa na wakaguzi waliochaguiliwa kwa mujibu wa kanuni za fedha za Serikali za Mitaa.
 



 

 

 

 

Taarifa ya fedha ya mwaka
15. Mwezi mmoja baada ya mwaka wa fedha wa Halmashauri, Bodi itatakiwa kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha ya mwaka na kuwasilisha kwa Halmashauri.
 

Mipango na Matumi-zi
16.-(1) Miezi miwili kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha wa Halmashauri, Bodi itaandaa mipango na bajeti ya mwaka kwa kuonyesha kiwango kinachotarajiwa kupatikana na mgawanyo wa fedha kwa ajili ya utoaji huduma za afya na maendeleo katika maeneo ya Halmashauri.
(2) Bodi inaweza kuandaa bajeti ya nyongeza kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo na kama mazingira yataruhusu.
(3) Mipango ya bajeti ya Mfuko itaandaliwa kulingana na utaratibu kama ilivyoainishwa katika vifungu vidogo vya (1) na (2) hapo juu, ambayo ni lazima iwasilishwe kwa Halmashauri kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi.
 



 

 
(4) Matumizi yatazingatia mipango shirikishi ya maeneohusika ambayoitakuwa sehemu ya Mpango kabambe wa afya wa Halmashauri. Pia mipango hii itazingatia maelezo yaliyomo ndani ya Mkataba wa Tele kwa Tele.

Usima-mizi wa Mfuko
17. Usimamizi  na uendeshaji wa Mfuko utakuwa chini ya :-
Halmashauri kupitia Bodi ya huduma za Afya ya Halmashauri katika ngazi ya Halmashauri.
kamati ya Maendeleo ya Kata kupitia Kamati ya afya ya Kata, katika ngazi ya Kata; na
Serikali ya Kijiji kupitia Kamati ya Huduma za Jamii katika ngazi ya Kijiji.

Kamati ya Afya ya kata
 
18. Kutakuwa na Kamati ya Afya ya Kata.

Wajum-be wa Kamati ya Afya ya Kata
19.-(1) Kamati ya Afya ya Kata itakuwa na wajumbe wafuatao:-
Diwani anayewakilisha Kata husika.
Afisa Mtendaji wa Kata;
Mwalimu Mkuu mmoja kutoka shule ya msingi na mmoja kutoka shule ya Sekondari ambayo ipo kwenye Kata husika;
Wajumbe wawili wanawakilisha jamii husika ambapo mmoja wao ni lazima awe mwanamke.
Mganga au Mganga Msaidizi wa Kituo cha Afya, ambaye atakuwa Katibu wa Kamati.
Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kutokana na watu waliopendekezwa na Serikali za Mitaa zilizomo ndani ya eneo la Kata; na
Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kutoka kwenye vyama vya kijamii kutoka kwenye Kata.
 

 
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Kata atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe.
Endapo Kamati ya Afya ya Kata itashindwa kutekeleza kazi zake, Halmashauri itatoa onyo au kuivunja na kufanya utaratibu wa uchaguzi wa wajumbe wengine katika muda usiozidi miezi mitatu.
 

 

Kazi na Majukumu ya Kamati ya Afya ya Kata
20.-(1) Kamati ya Afya ya Kata itakuwa na majukumu yafuatayo:-
kuwahamasisha na kuandaa jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.
kuandaa orodha na kuratibu idadi ya wajumbe wa Mfuko wa Jamii.
kusimamia ukusanyaji wa michango ya Mfuko.
kuratibu viwango vya  uchangiaji kwenye huduma za afya;
kupitia utendaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii na kutoa mapendekeo ya ufumbuzi;
kuanzisha na kuratibu mipango ya Afya  ya Jamii na;
kuendesha mikutano ya wajumbe wa Mfuko wa Afya ya Jamii

 
(2) Kamati ya Afya ya Kata, itakaa kila baada ya miezi mitatu, na Katibu atatoa taarifa ya maandishi wiki moja kabla ya siku ya Kikao.
(3) Baada ya kikao katibu atawasilisha muhtasari wa kikao hicho kwa Katibu wa Mfuko wa Wilaya.
 

 

Matumi-zi ya fedha za Mfuko
21. Fedha zitakazokusanywa na Mfuko zitatumika kwa madhumuni yafuatayo:-
  • masuala yanayohusiana na afya yaliyotajwa katika mpango wa afya na kuidhinishiwa na Wizara; na
  • suala au shughuli yoyote muhimu ya afya kama itakavyoonekana inafaa na kama itaidhinishwa na Bodi

Utoaji wa Kadi kwa wanachama
22.-(1) Kila mwanachama wa Mfuko na wategemezi wake, atapewa Kadi baada ya kulipa mchango wake wa mwaka kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 24(1) cha sheria ndogo hizi.
(2) Kwa kuzingatia kanuni za mfuko wa afya ya jamii za mwaka 2004, kila mwanachama atakayepewa msamaha ni lazima atapewa kadi ya uanachama na Halmashauri itaweka utaratibu wa kulipia kadi hiyo.
 

 

Haki za mwana-chama na Utoaji wa Huduma za afya
23. Kila mwanachama na wategemezi wake watakuwa na haki zifuatazo:
  • kupata huduma ya afya aliyolipia anapougua ndani ya eneo la Halmashauri husika au katika kituo cha Afya kwenye Halmashauri nyingine ambayo itaingia makubaliano maalum na Halmashauri husika.
  • kupata huduma ya afya kwa baba, mama na watoto wao wenye umri chini ya miaka kumi na nane;
  • kutoa mapendekezo kuhusu huduma za afya kupitia kituo chake cha tiba ambayo yatafanyiwa kazi na Bodi; na
  • kushirikishwa kikamilifu katika uandaaji na utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa huduma za afya, katika eneo la Halmashauri

Kiwango cha mchango au ada ya mwana-chama
24.-(1) (a) Mtu yeyote atakayetaka kuwa mwanachama wa mfuko wa afya ya jamii atapaswa kutoa kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000) kila mwaka.
(b) Mchango huo utalipwa na kila mtu anayetaka kuwa mwanachama wa mfuko mwanzoni mwa mwaka au kila mwaka wa fedha unapoanza au kama Bodi itakavyoelekeza.
(c) Mtu yeyote ana hiari ya kulipa mchango wake wa uanachama kwa zaidi ya mwaka mmoja;
(2) Bila kuathiri kifungu cha 21 (c) hapo juu mtu yeyote anayelipa mchango wa uanachama kwa zaidi ya mwaka mmoja, pale inapotokea mabadiliko ya kiwango cha mchango atawajibika kulipa tofauti ya kiwango kilichozidi kile cha awali.
(3) Halmashauri itaandaa utaratibu wa kupanga kaya maalum zilizoko katika Taasisi/shule mbaimbali zilizo ndani ya Halmashauri ili kuziwezesha kupata huduma ya Tiba kwa kadi.

 

 

Muda wa uanachama
25. (a) Mtu yeyote atabaki kuwa mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii wa Tiba kwa Kadi kila atakapolipa ada yake ya mwaka.
  • (b) Kila mwaka unapoisha uanachama wa mtu utafikia mwisho hadi pale atakapotimiza masharti ya kifungu (a) hapo juu.

Malipo ya papo kwa papo
26.-(1) Mtu yeyote ambaye hatakuwa mwanachama wa mfuko huu, atalipa mchango au malipo ya papo kwa kila atakapoenda kupata matibabu katika kituo cha kutolea huduma za Afya.
(2) Malipo ya papo kwa papo yatalipwa kama ifuatavyo;
shilingi elfu moja (1,000/=) katika huduma za afya zinazotolewa na Zahanati katika eneo lolote la Halmashauri.
shilingi elfu moja mia tano (1,500) kwa huduma za Afya zinazotolewa na kituo cha Afya kilichopo ndani ya Halmashauri.
huduma za Hospitali za aina zote kulingana na Sera ya uchangiaji.
 



Misamaha kwa wasioji-weza
27.Misamaha kwa wasioweza kulipa gharama za matibabu itatolewa na kulipwa na Halmashauri baada ya kuzingatia utaratibu ufuatao;-
uongozi wa Kitongoji utawatambua, kuwaorodhesha na kuwasilisha majina ya wasio na uwezo wa kulipa gharama za matibabu katika Serikali ya Kijiji;
Serikali ya Kijiji katika vikao vyake itapokea, itajadili na kuwasilisha orodha sahihi kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
Kamati ya Maendeleo ya Kata itapokea,itajadili na kuwasilisha orodha sahihi ya wasioweza kulipa gharama za matibabu kwa Bodi ya Afya ya Halmashauri; na
Bodi ya Afya itapokea, na kujadili mapendekezo husika na kuyawasilisha pamoja na gharama zake kwa Halmashauri kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi.

Makosa
28. Mtu yeyote ambaye:-
  • atakwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi; au
 atafanya kitendo chochote ambacho kitazuia Bodi kufanya kazi zake kwa ufanisi; au
atatumia vibaya mali na rasilimali za Mfuko na kusababisha kutofikia malengo ya Bodi; au
atatumia vibaya madaraka aliyonayo kumzuia afisa wa Bodi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria hii;
atashindwa kwa uzembe kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi.

Atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi Shilingi elfu hamsini (50,000/=) na isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kifungo jela kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo.






TANGAZO LA SERIKALI NA. 209 la tarehe 29/05/2015

 

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)

 

(SURA 287)

_____

SHERIA NDOGO

_____

 

Zimetungwa chini ya kifungu cha 153

_____

SHERIA NDOGO ZA (HIFADHI YA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSEGA ZA MWAKA, 2015

Jina na mwanzo wa kutumika
  • Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega, 2015 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali
Eneo la matumizi
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
Tafsiri
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo:
“Afisa mwidhinishwa” maana yake ni Afisa Maliasili, Afisa Kilimo na Mifugo na Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi;
“Eneo la Hifadhi” ni maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi;
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
“Hifadhi ya Mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa mwidhiniwa chini ya Sheria Ndogo hizi au Sheria nyingine yeyote;
“Kiwanda” maana yake ni jengo au kundi la majengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa;
“Kuvuna misitu” maana yake ni pamoja na kufyeka, kukata au kung’oa miti, visiki;
“Maeneo ya malisho” maana yake ni pamoja na sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri;
“Maji” kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya usimamizi Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 ni pamoja na maji ya kunywa, ya mito, vijito, maji yanayotiririka, yaliyohifadhiwa, yaliyo katika visima, mabwawa, mifereji, madimbwi, maziwa, maji yaliyoko chini ya ardhi na maji yaliyoko katika mkondo.
“Mazao ya misitu” maana yake kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 chini ya kifungu Na, 2 ni kitu chochote kinachopatikana au kuzalishwa kutokana na miti, mazao yanayoota au kupatikana msituni, ambayo ni pamoja na mianzi, magamba, mkaa, kuni, miti, fito, mbao, mbegu za miti, nta, asali, utaa, matunda, upapi, majani ya kulalia wanyama, majani, mizizi, gundi, utomvu, maranda matete, kamba, makuti mawale), nyuzi za wanyama, mimea (miti) na kitu chochote chenye uhai au kisicho na uhai kitakachotangazwa katika gazeti la Serikali kuwa ni zao la msitu..
“Mazingira”kama ilivyotafsiriwa katika sheria ya usimamizi wa mazingira na.20 ya mwaka 2004 yanahusisha maumbile halisi ya wazungukao Binadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji, tabia ya nchi, sauti, mwanga, harufu, ladha, viumbe hali za kibiolojia za wanyama na mimea.rasilimali za kitamaduni na masuala ya uchumi jamii na inahusisha mazingira asilia na yaliyoundwa binadamu na jinsi yanavyoingiliana ;
“Mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halimashauri
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi mtendaji wa Halimashuri ya wilaya ya Busega na ni pamoja na Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi;
  • “Mifugo” maana yake ni mnyama yeyote anayefugwa na binadamu;
“Misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asilia au iliyopandwa, au asilimia 50 au zaidi, ya vichaka na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifahi ambayo itatangazwa chini ya sheria ya misitu Na. 14 ya mwaka 2002 na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri;
“Uchafu hatari” kama ilivyotafsiriwa katika sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004.Maana yake ni kitu chochote kigumu, chenye majimaji, gesi au taka zitokazo viwandani, au mafuta machafu,ambayo yanaleta athari za kikemia,kwa binadamu, au mazingira;
“Uchafuzi wa Mazingira” kama ilivyo katika sheria ya usimamizi wa mazingira Na.20 ya mwaka 2004 ni mabadiliko ya hali ya hewa ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja, joto, kemikali, biolojia, au zana za mionzi katika mazingira ambayo zana hizo zinafanyia kazi au kutoa harufu mbaya, mrundikano wa taka ambazo unaathiri watumiaji, au unaosababisha hali hatari kwa afya ya jamii, usalama, au ustawi, au hatari kwa wanyama, ndege, wanyama pori, samaki, au viumbe vyote vya baharini, mimea au kusababisha hali mbaya ya hewa, upungufu au kizuizi ambacho ni sehemu katika sheria hizi;
“Udongo” kama ilivyo katika sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 maana yake ni pamoja na dunia, mchanga, miamba, miamba tope, madini, uoto wa mimea, mimea na wanyama iliyoko chini ya udongo pamoja na vumbi;
“Vitu hatari” maana yake kama ilivyotafsiriwa katika sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004, ni kemikali yoyote, taka gesi, madawa, vidonge, mimea wanyama au viumbe hai visivyoonekana ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu, maisha au mazingira;
“Waziri” maana yake ni waziri mwenye dhamana ya serikari za mitaa.
                                                                                                                                                                           



SEHEMU YA PILI

MASHARTI YA UFUGAJI

Wajibu wa mfugaji
4.-(1) Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hizi;-
atatakiwa kufuga idadi ya mifugo kama itakavyoainishwa katika kibali chake kitakachomruhusu kufuga kwa kuzingatia ukubwa wa eneo na kuridhika kwamba ufugaji huo hautakuwa kero kwa majirani.
atatakiwa kufuga ndani ya eneo lake (zero grazing) bila ya kuleta usumbufu kwa jirani zake na jamii kwa ujumla na kuhakikisha sehemu ya kufugia wanyama hao inakuwa safi wakati wote na ana chombo cha kuhifadhi samadi inayotokana na mifugo hiyo.
anayeishi pembezoni mwa Mji atatakiwa kupitisha mifugo yao katika njia zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri
atatakiwa kuwa na kadi ya mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo;
atatakiwa kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoagizwa na Halmashauri;
atatakiwa kupeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamuriwa na Halmashauri na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo;
Masharti ya mfugaji
5. Ni marufuku kwa mfugaji yeyote;
kuchunga, kulisha na kunywesha maji mifugo katika maeneo ya mipango miji pamoja na maeneo yote ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo;
kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani;
kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi jingine bila kibali kutoka kwa Halmashauri;
kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri;
kufuga mifugo mingi katika eneo dogo la Halmashauri
Ni marufuku kwa mfugaji yeyote kupitisha mifugo katika maeneo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri kupitisha mifugo;
Kudhibiti mifugo inayodhurura ovyo
6.-(1) Halmashauri itakamata mifugo au mfugo wowote utakaoonekana unazurura hovyo katika eneo la Halmashauri ambapo hapajaruhusiwa kuchungia mifugo.

(2) Mfugo wowote utakaokamatwa utalipiwa faini kama itakavyopangwa na Halmashauri na baada ya kulipia gharama hizo mfugaji atarudishiwa mifugo yake.
(3) Endapo mwenye mifugo au mfugo hatatokea ndani ya siku saba (7) tangu kukamatwa kwa mifugo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo au mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama.
(4) Baada ya mauzo, Mkurugenzi atakata fedha za faini, gharama za mnada na gharama za ulinzi na fedha zitakazobaki atapewa mwenye mifugo na kama hataonekana ndani ya siku kumi na nne (14) fedha hizo zitaingizwa katika vyanzo vya mapato ya Halmashauri.
(5) Endapo mwenye mifugo hiyo atakuwa na sababu za msingi za kutofika kwake katika muda wa siku kumi na nne (14) Halmashauri itarudisha fedha zake                                                                                                                                  
(6) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote.




Ukaguzi wa mifugo
7.-(1) Itakuwa halali kwa Afisa Kilimo na Mifugo, Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, na Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kuingia katika nyumba au jengo lolote wakati wowote kwa madhumuni ya kukagua na kuhesabu idadi ya mifugo iliyomo katika nyumba hiyo..

(2) Mtu yeyote atakayemzuia Afisa Muidhiniwa kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa.
Wajibu wa Halmashauri
8.-(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za malisho kwa kuzingatia idadi ya mifugo ndani ya eneo la Halmashauri na kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Sura ya 113 na 114 pamoja na Sheria ya usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004.

(2) Halmashauri itatenga njia maalum ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani.
  •                                                                     
(3) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa kadi ya mifugo na elimu ya ufugaji bora kwa jamii

Taratibu za ufugaji
9.-(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyo katika Sheria Ndogo hizi au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(2) Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mfugo au mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinjia nyama mahali pengine popote.
(3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo lolote la Halmashauri isipokuwa kwenye minada ya magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo.
                                                                                                                                                                                             





SEHEMU YA TATU

KILIMO NA HIFADHI YA ARDHI

Taratibu za kilimo
10.-(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo kama zitakavyotolewa na Halmashauri kwa kuzingatia sheria ya Ardhi sura ya 113 na 114 na Sheria nyingine zitakazotungwa na Bunge.

(2) Itakuwa halali kwa Afisa Kilimo kuingia katika shamba lolote kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi.
Masharti kwa mkulima
11.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira bila kuzingatia ushauri wa Afisa Kilimo.Michango ya jamii.
(2)  Ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia kinyume ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kilimo kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri.
(3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa Halmashauri.
(4) Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi kitakuwa cha maandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto.
(5) Muda unaotakiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hizi ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi.
(6) Ni wajibu wa Halmashauri kusimamia shughuli za kilimo na kuhakikisha kuwa wanazuia kilimo cha kuhamahama na kuhimiza kilimo cha mzunguko (crops roration).
 





Uhifadhi wa uoto wa asili
12. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha kuwa wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti au kutoendelea kuharibu mazingira na kuwezesha uoto urudi katika hali yake.
Uchimbaji mchanga na kokoto
13. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa kando kando ya barabara, mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa katikati ya barabara.

14. Ni marufuku kwa mtu yeyote kujenga nyumba au jengo lolote katika eneo la hifadhi.



SEHEMU YA NNE

HIFADHI YA VYANZO VYA MAJI

Wajibu wa kulinda vyanzo vya maji
15.-(1) Halmashauri itawajibika kuanzisha, kusimamia na kulinda vyanzo vya maji.
(2) Maeneo yaliyotajwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hizi yamehifadhiwa.
(3) Halmashauri itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila sababu ya msingi.


Kulinda eneo la hifadhi
16.-(1) Ni marufuku wa mtu yeyote kulima, kukata miti, kufuga mifugo katika umbali wa mita 60 toka vyanzo vya maji au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira.
(2) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu.  
                                                     
(3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki eneo la chanzo cha maji isipokuwa Halmashauri.
       


Uchafuzi wa vyanzo vya maji
17.-(1) Ni marufuku mtu yeyote, kiwanda, taasisi, shirika kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye mito, mabwawa, ziwa, visima, mifereji, chemichemi au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai.
(2) Ni marufuku mtu yeyote kuweka kituo chochote chenye sumu ndani ya maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe chochote hai.




SEHEMU YA TANO

HIFADHI YA MISITU

Kuchoma au kusababisha moto
18.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma misitu kwa namna yoyote ile katika misitu iliyoko eneo la Halmashauri

(2) Iwapo moto utatokea katika eneo la Halmashauri, kiongozi wa eneo husika atawajibika kutoa ishara ya hatari kwa kutumia njia iliyozoeleka kuamuru wakazi wa eneo hilo kwenda kuzima moto huo unapoonekana kuwa na madhara kwa maisha, mali za watu na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo.
(3) Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuzima moto huo endapo atatakiwa kufanya hivyo, kama atashindwa kushiriki katika kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa ametenda kosa.

Kibali cha kuchoma moto
19. Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa ya siku saba (7) kabla ya kuchoma moto kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma na ataweka njia za kuzuia moto.
Ukataji miti
20. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri.
(2) Halmashauri itatakiwa kuhakiki kama miti inayovunwa imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi.
(3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe maalum ambao ni rasilimali kwa Taifa.
(4) Watu wanao vuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa watatakiwa kuwa na eneo maalum lililoidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa.



Wajibu wa kupanda miti
21. Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika;-
  • kupanda na kutunza miti katika eneo lake
  • kupanda na kutunza miti katika shamba au mashamba anayomiliki.

22. Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kila kijiji;
  • kitawajibika kutenga eneo la hifadhi ya misitu wa asili kwa  ajili ya matumizi ya baadae;
  • kitalazimika kutunza miti yote inayopandwa katika eneo la kijiji;
  • kitahakikisha ya kuwa kila kaya inapanda miti isiyopungua kumi kwenye eneo la nyumba yake;
  • mtu yeyote anayetaka kukata miti au mti wa matumizi yakuchonga vifaa, kujenga nyumba, kutengeneza zizi na shughuli nyinginezo, inabidi apate kibali cha maandishi toka kwa mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kijiji  na kibali cha Afisa Maliasili wa wilaya au wasaidizi wake kwa miti iliyopanda na kuhifadhiwa na Halmashauri ya wilaya;
  • kinapaswa kutenga na kupanda shamba la miti ekari 2 kila mwaka na kulitunza;
  • kila shule au taasisi nyingineyo wilayani itapaswa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yake na kuwa na shamba lisilopungua miti hekta2;
  • Kijiji kitapaswa kutunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, makorongo na vyanzo vya maji ili kuzuia mmomonyoko wa udongo;
  • Kijiji kitahakikisha kuwa kila anayeandaa shamba kwa ajili ya kilimo hatumii moto na anapanda miti kwenye mipaka ya shamba lake kama kinga upepo;
  • Kila mtu mwenye nyumba kwenye mji mdogo atawajibika kupanda miti kando ya barabara inayopita mbele ya nyumba yake na kuitunza;
  • Kila Mwenyekiti wa kitongoji, Mtendaji wa kijiji, Mkuu wa taasisi yoyote Wilayani atahakikisha kuwa kijiji au taasisi ina msitu wa hifadhi wa miti ya kupandwa au ya asili iliyotengwa kwa madhumuni ya kuhifadhi ardhi, mazingira na matumizi ya baadaye.
  • SEHEMU YA SITA
  • MAKOSA NA ADHABU
  •  
Makosa yanayohusu mifugo
23. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa:
  • ataingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali;
  • atasafirisha mifugo nila kuwa na kibali;
  • atalisha mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa;
  • atafuga mifugo zaidi ya idadi iliyoruhusiwa;
  • atavua samaki kwa kutumia sumu au nyavu zenye matundu madogo (kokoro)
Makosa yanayohusu kilimo
24. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kilimo, kuchimba mchanga, kokoto, madini katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri atakuwa ametenda kosa.
Makosa yanayohusu kuhifdhi ardhi
25. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kuhifadhi ardhi atakuwa ametenda kosa.
Makosa yanayohusu vyanzo vya maji
26.-(1) Mtu yeyote atakayeharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji atakuwa ametenda kosa.
(2) Mtu yeyote atakayebainika kuwa ameweka sumu ya aina yoyote kwa namna yoyote ambayo inaathiri maisha ya binadamu na viumbe wengine ambao ni rasilimali ya Taifa atakuwa ametenda kosa.

Makosa yanayohusu kuharibu misitu
24. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa:
  • atachoma au kusababisha moto katika msitu bila kibali, au
  • atashindwa kushiriki katika kuzima moto, au
  • atavuna mazao ya misitu katika misitu iliyohifadhiwa isiyohifadhiwa bila kibali; au
  • atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali; au
  • atafyeka nyasi, kung’oa vichaka na kung’oa visiki kwenye eneo bila kibali; au
  • atachunga mifugo kwenye eneo lolote lililopandwa miti iliyohifadhiwa kama bustani ya miti;
  • atakata miti, au kuchungia mifugo kwenye miti iliyopandwa kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa udongo au kinga upepo
  • atabandua magome ya miti kwa ajili ya kutengenza vilindo, mzinga na vitu vingine bila ya kuwa na kibali
  • atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, milima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zinazohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo.
adhabu
25. Mtu yeyote atakayevunja masharti yaliyowekwa na Sheria    Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (Tshs.300, 000) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo.
 

 

JEDWALI

S/NA

AINA YA MIFUGO

ADHABU(TSHS)KWA KILA MFUGO

1

Ng”ombe

5,000/=

2

Mbuzi

2,000/=

3

Kondoo

2,000/=

4

Nguruwe

2,000/=

5

Mifugo mingine

2,000/=s


Tangazo la Serikali Na. 208  la Tarehe 29/05/2015

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA),

(SURA YA 287)

________

SHERIA NDOGO

______

Zimetungwa chini ya Kifungu cha. 153

_______

SHERIA NDOGO ZA (UANZISHAJI WA BODI YA MFUKO WA ELIMU) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSEGA, 2015

Jina na tarehe ya kuanza kutumika
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana Kama Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu) za Halmashauri ya Wilaya ya Busega, 2013 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama itatamkwa vinginevyo;
“Afisa Elimu wa Halmashauri” maana yake ni Mtumishi wa Umma ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa utoaji wa huduma za elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
“Bodi” maana yake ni Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Wilaya iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 4(1) cha Sheria Ndogo hizi.
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
“Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri” maana yake ni Kamati ambayo imeanzishwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya).
“Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu” maana yake ni Kamati iliyoteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 30 cha Sheria Ndogo hizi.
“Katibu Mtendaji” maana yake ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri aliyeajiriwa na Bodi ya Mfuko wa Elimu kwa mujibu wa Kifungu cha 22 cha Sheria Ndogo hizi.
“Mfuko wa Elimu” maana yake ni Mfuko wa Elimu ulioanzishwa kwenye Halmashauri kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi
“Mkuu wa Wilaya” maana yake ni Mkuu wa Wilaya ya Busega aliyeteuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997.

Matumizi

Tafsiri
 Sura ya 287
Sheria Na. 19 ya Mwaka 1997

SheriaNa 8/2002
Na 5/1992
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi.
“Timu ya uendeshaji Mfuko” maana yake ni timu ya Wataalam inayoshughulikia shughuli za kila siku za Mfuko.
“Viwango vya Elimu” maana yake ni viwango vya elimu ya Awali na Msingi, Elimu ya Sekondari na Ufundi vilivyowekwa kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo
“Wadhifa kwenye Chama Cha Siasa” maana yake ni kuwa na madaraka ya kuteuliwa au kuchaguliwa kwenye Chama chochote cha Siasa kilichoandikishwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992.

Kamati ya Elimu ya Kata
Wajumbe wa Kamati ya Elimu ya Kata
Bodi ya Mfuko wa Elimu
4.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Elimu ya Kata, ambayo itafanya kazi kwa kushirikiana na Bodi ya Mfuko wa Elimu
  • Fedha za kuendeshea Kamati ya Elimu ya Kata zitatokana na chanzo namba (1) katika Jedwali la Sheria Ndogo hizi, na zitatumika kwa mujibu wa bajeti iliyopitishwa na Kamati ya Maendeleo yaa Kata na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri
  • Mkurugenzi atakuwa na mamlaka ya kumuagiza mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya Kamati ya Elimu ya Kata wakati wowote au angalau mara mbili kwa kila mwaka wa fedha.
  • Posho, marupurupu na mishahara kwa watendaji wa Kamati ya Elimu ya Kata vitapendekezwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata na zitaanza kutolewa mara baada ya kuidhinishwa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri
(2) Kamati ya Elimu ya Kata itaundwa na wajumbe wafuatao:-                                                                                  
  • Diwani wa Kata, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati
  • Mratibu wa Elimu katika Kata husika, ambaye atakuwa Katibu
  • Wajumbe watatu (3) watakaochaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata, angalau mmoja wao atakuwa mwanamke
  • Mjumbe mmoja kutoka Shirika lisilo la kiserikali ambalo hujishughulisha na utoaji wa elimu katika Wilaya
  • Mjumbe mmoja ambaye atateuliwa na Mwenyekiti wa Kamati na kuridhiwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata
  • Ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za Kamati utafanywa na Afisa Mtendaji Kata
5. Kutakuwa na Bodi itakayojulikana kama Bodi ya Mfuko wa    Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Wajumbe wa Bodi
(1) Bodi itaundwa na Wajumbe wafuatao:-
Mwenyekiti ambaye atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mfuko kutoka miongoni mwa watu wenye uzoefu na masuala ya elimu
Katibu Tawala wa Wilaya
Wawakilishi wawili watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu ambapo mmoja kati yao sharti awe mwanamke.
Mwakilishi mmoja kutoka miongoni mwa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali katika Halmashauri.
Mwakilishi mmoja kutoka Wamiliki wa Shule za binafsi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Baraza la Halmashauri.
Wawakilishi wawili kutoka miongoni mwa walimu wakuu wa Shule za Msingi.
Mwakilishi mmoja kutoka miongoni mwa makatibu tarafa
           


(2) Bila kuathiri masharti ya Kifungu cha 4(2) cha Sheria Ndogo hizi Bodi pia itakuwa na Wataalamu wafuatao:
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
Afisa Elimu wa  Halmashauri
Mweka Hazina wa Halmashauri.

Ofisi za Bodi
6. Ofisi za Bodi zitakuwa katika eneo la Halmashauri au sehemu nyingine kama Bodi itakavyoamua.

Bodi kualika watu wengine
7. Bodi inaweza kualika watu wengine kwenye vikao vyake kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo lakini hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
Uchaguzi wa Mwenye-kiti wa Bodi
8. Mwenyekiti wa Bodi atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mfuko baada ya nafasi hiyo kutangazwa katika magazeti yanayosomwa katika eneo la Halmashauri.
Kipindi cha kushika madaraka
9.-(1) Wajumbe wa Bodi watashika madaraka kwa kipindi cha miaka mitatu, lakini mjumbe anaweza kuchaguliwa tena na kuendelea kuwa madarakani kwa kipindi kingine cha mika mitatu.
(2) Ufikapo wakati wa uchaguzi wa wajumbe wapya au baada ya Kipindi cha muda wa Bodi kuisha, Mkurugenzi Mtendaji atatangaza nafasi wazi na watu wenye sifa hizo watajaza fomu maalum za maombi na kuzirudisha kwenye Halmashauri ndani ya kipindi kitakachowekwa.



Utaratibu wa kujaza nafasi wazi
10.-(1) Pale ambapo nafasi katika Bodi zitakuwa wazi aidha kwa kifo, kujiuzulu, ugonjwa, au kwa sababu nyingine yoyote ile mjumbe mwingine atachaguliwa kujaza nafasi hiyo kwa kipindi kilichobaki.


(2) Hakuna uchaguzi utakaofanywa endapo kipindi kilichobaki ni chini ya miezi sita.


(3) Mjumbe atakayechaguliwa kutokana na Sheria Ndogo ya 9(1) hapo juu ataweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Uteuzi wa mwisho wa Bodi kuthibitishwa  na Baraza la Madiwani
11.-(1) Uteuzi wa wajumbe utathibitishwa na Baraza la Madiwani baada ya kupendekezwa na Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu.

Uzinduzi wa Bodi
(2) Bodi itazinduliwa rasmi kwa kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya baada ya kuidhinishwa na Baraza la madiwani.

Bodi kuvunjwa kwa kuzembea kazi
12.-(1) Endapo Bodi itazembea kazi au itashindwa kutekeleza kazi zake, Halmashauri itaionya Bodi mara mbili kwa maandishi au kuivunja Bodi na kuandaa uchaguzi mpya ndani ya miezi miwili.
(2) Endapo Bodi itavunjwa, wajumbe wote wa kuchaguliwa watapoteza nafasi zao na hawatachaguliwa tena kuwa Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Elimu.
(3) Wakati Bodi imevunjwa, Timu ya Uendeshaji ya Mfuko wa Elimu itatekeleza majukumu ya Bodi hadi hapo Bodi mpya itakapochaguliwa.

 

 

Vikao vya Bodi
13.-(1) Bodi itafanya Vikao vyake vya Kawaida kila baada ya miezi mitatu, na Vikao vyote vya Bodi vitaendeshwa na Mwenyekiti na endapo Mwenyekiti hatakuwepo, Mjumbe mmoja atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe kuwa Mwenyekiti wa Kikao.
(2) Vikao vya dharura vitafanywa pale tu Mwenyekiti atakapoomba au kuombwa kufanya hivyo kwa maandishi na kupata idhini ya Wajumbe wasiopungua theluthi moja ya Wajumbe wote wanaopiga kura.
(3) Mjumbe yeyote ambaye bila taarifa au sababu ya msingi atashindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bodi atakuwa amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mjumbe wa Bodi na nafasi yake itatangazwa kuwa wazi.





Kumbu-kumbu za mikutano ya Bodi
14. Bodi itahakikisha kumbukumbu za Mikutano yake yote zinaandikwa na kuhifadhiwa, pia kumbukumbu za kila Mkutano zitathibitishwa na Bodi kwenye mkutano unaofuata na zitatiwa saini na Mwenyekiti wa Mkutano pamoja na Katibu.

Akidi ya kikao na uwezo wa kuamua
15.-(1) Nusu ya Wajumbe wote ndiyo itakuwa akidi kamili katika Vikao vyote vya Bodi.

 
(2) Uamuzi wa Bodi utakuwa ni ule unaoungwa mkono na Wajumbe zaidi ya nusu ya Wajumbe kamili wa Bodi.
(3) Wajumbe wa kuchaguliwa wa Bodi ndio watakaokuwa na uwezo wa kupiga kura na kupitisha uamuzi wa Bodi.
(4) Wataalamu na waalikwa hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
(5) Kila Mjumbe wa Bodi atakuwa na kura moja na iwapo itatokea kura kufungana Mwenyekiti wa Bodi atakuwa na kura ya ziada mbali na kura yake ya kawaida.







Sifa za kuwa mjumbe wa bodi
16.-(1) Mtu anaweza kushika nafasi ya ujumbe wa Bodi kama atakuwa na sifa zifuatazo;
awe raia wa Tanzania
awe na umri usiopungua miaka ishirini na  mitano na asizidi miaka sabini
awe na akili timamu
awe na elimu ya sekondari, yaani kidato cha nne na kuendelea, isipokuwa endapo hakuna mtu mwenye elimu ya Sekondari basi Halmashauri itatoa idhini kuajiri bila kujali elimu yake, na
asiwe na madaraka yoyote kwenye chama cha Siasa.






(2) Mfanyakazi wa Halmashauri hataruhusiwa kuwa Mjumbe wa Bodi.
Majukumu na Kazi za Bodi
17. Majukumu na kazi za Bodi zitakuwa kama ifuatavyo:-
  • kubuni Mipango na Mikakati kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika Halmashauri.
  • kusimamia mgawanyo wa misaada ya fedha kwa Shule kufuatana na Bajeti iliyoidhinishwa na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Bodi.
  • kusimamia utekelezaji na kutathmini Mipango ya Elimu katika Halmashauri.
  • kujadili na kurekebisha Mipango na Bajeti ya Elimu na kuiwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Utendaji kwa ajili ya kuidhinishwa;
  • kupokea, kuchambua na kuidhinisha Taarifa za Utekelezaji wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri;
  • kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato na rasilimali za kutosha kuendesha Mfuko wa Elimu wa Halmashauri;
  • kushirikiana na Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri;
  • kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya Elimu katika Halmashauri kulingana na programu za kitaifa.
  • kupitisha Kanuni za Utengaji na Utumiaji wa Fedha kutoka kwenye Mfuko kwa ajili ya kuendeleza madhumuni ya Mfuko.
  • kusimamia ujenzi wa Shule za Sekondari katika Halmashauri.
  • kufanya jambo lolote litakalofanikisha maendeleo ya Elimu katika Halmashauri.
Mamlaka ya Bodi
18. Bodi itakuwa na mamlaka yafuatayo:
  • kusimamia mgawanyo wa fedha zinazoingizwa kwenye Mfuko wa Elimu wa Halmashauri.
kuajiri na kuachisha kazi watumishi wa Bodi.
Maagizo na maelekezo
19. Maagizo, maelekezo, taarifa au hati nyingine zilizotengenezwa au kutolewa kwa niaba ya Bodi zitatiwa saini na;
Mwenyekiti wa Bodi au
Katibu Mtendaji au Afisa mwingine ye yote aliyeidhinishwa kwa maandishi na Katibu Mtendaji wa Bodi kwa ajili hiyo
Uhusiano wa Bodi na wadau na mamlaka nyingine
20.-(1) Uhusiano wa Bodi na Jamii, wadau na mamlaka nyingine utakuwa kama ifuatavyo:
Bodi itahakikisha kuwa jamii inashirikishwa kikamilifu katika kutambua matatizo, kuweka kipaumbele, kupanga, kuchangia, kufuatilia na kutathmini utoaji wa huduma za elimu;
Bodi itawajibika mbele ya Halmashauri ambapo mipango ya elimu ya robo mwaka na ile ya mwaka pamoja na taarifa za kiutaalam za fedha zinapitiwa na Kamati ya Huduma za Jamii na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango na baadaye kuthibitshwa na Baraza la Halmashauri.
Bodi itaendesha shughuli zake kwa utaratibu wa uwazi na ambao utakuwa na ufanisi kwa Halmashauri na vyombo vyake vingine vya utendaji bila ya Halmashauri kuingilia uhuru wa Bodi.

(2) Bila ya kuathiri maelezo yaliyomo katika Sheria Ndogo ya (1) ya Sheria Ndogo hizi Bodi inaweza kukasimu baadhi ya madaraka yake pale inapoona inafaa.
20. Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri itafanya kazi zifuatazo;
itapokea Mipango yote ya Maendeleo ya Mfuko.
itapokea taarifa za Ukaguzi wa Hesabu za Mfuko na kupitia hoja za Ukaguzi na baadaye kuziwasilisha kwenye Halmashauri ambayo itaijadili na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kamati ya Huduma za Jamii ya Halma-shauri
Jukumu la Wizara na Mamlaka ya Elimu
21. Jukumu la Wizara zinazoshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Elimu pamoja na Mamlaka ya Elimu itakuwa ni kuandaa Sera, kupanga viwango, kufuatilia na kusimamia shughuli za Bodi kwa mujibu wa sheria zilizopo.
22. Bodi kwa idhini ya Mkutano Mkuu wa mwaka, itamteua Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri.
23.-(1) Nafasi ya Katibu Mtendaji itatangazwa katika magazeti yanayosomwa zaidi nchini na Bodi itamteua mtu ambaye atakidhi vigezo vya uteuzi na ambaye atakuwa na sifa zinazofaa.
Katibu Mtendaji
Uteuzi wa Katibu Mtendaji
 
(2) Bodi itaamua sifa za watu ambao wataomba nafasi ya Katibu Mtendaji.


(3)
Katibu Mtendaji atakuwa na muda maalum wa kushika madaraka kama itakavyopangwa na Bodi:
Isipokuwa tu kwamba kipindi kimoja cha madaraka kisizidi miaka mitatu na mtu aliyeko madarakani anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.
Kazi za Katibu Mtendaji
24. Kazi za Katibu Mtendaji wa Bodi zitakuwa:
kuwa Mtendaji Mkuu wa shughuli zote za Mfuko na Katibu wa Vikao vyote vya Bodi.
kuongoza, kupanga na kuratibu utendaji wa shughuli za Mfuko.
kubuni, kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Mfuko.
kubuni na kushauri vyanzo mbalimbali vya mapato vya Mfuko wa Elimu wa Halmashauri.
kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Elimu wa Halmashauri.
kubuni na kushauri mbinu mbalimbali za kukuza na kuendeleza Mfuko wa Elimu wa Halmashauri.
Vyanzo vya mapato
25. Vyanzo vya mapato vya Mfuko wa Elimu vitakuwa kama ifuatavyo:-
Mchango wa asilimia sio chini ya tatu (3%) kutoka mapato ya mwaka ya Halmashauri.
Michango ya kila mwaka ya kila Mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi anayeishi katika eneo la Halmashauri kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali la Sheria Ndogo hizi;
Ruzuku mbalimbali
Misaada mbalimbali kutoka Nchi mbalimbali, taasisi za kimataifa na kitaifa, Mashirika ya watu binafsi na kiserikali, Makampuni binafsi, na madhehebu ya Dini.
 
 
 
 
 
Mikopo; na
Vyanzo vingine halali vya mapato
Fedha za Mifuko kulipwa kwenye Akaunti
26. Fedha zote zitakazokusanywa kama fedha za Elimu zitalipwa kwenye akaunti za Benki kama Bodi itakavyoona inafaa au kuagiza
Akaunti maalum ya Mfuko wa Elimu
27.-(1) Kutakuwa na Akaunti Maalum ya Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ambapo fedha zote zitawekwa na kutunzwa.
(2) Wawekaji saini wa akaunti ya Mfuko wa Elimu pamoja na taratibu nyingine za mfuko huo zitakuwa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya mwaka 2001.


(3) Bodi itaajiri Mweka Hazina atakayesimamia Akaunti za Mfuko wa Elimu na kutunza mahesabu yote ya mapato na matumizi.
Matumizi ya Fedha
28. Fedha zitakazowekwa kwenye Mfuko wa Elimu zitatumika kwa madhumuni ya kuendeleza, kukuza na kuboresha Elimu kama itakavyokuwa katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu wa Halmashauri.
29. Bodi inaweza kuidhinisha malipo ya fedha kutoka kwenye mfuko kwa madhumuni ya kulipia gharama za;
ujenzi wa Shule za Sekondari na Msingi katika Halmashauri.
uendeshaji wa Bodi na Kamati ya Utendaji.
miradi na programu zinazogharimiwa na Mfuko.
udhamini wa masomo kwa wanafunzi yatima na wale wasio na uwezo wa kulipia masomo yao.
Shughuli nyingine yoyote au zozote ambazo kwa maoni ya Bodi zina manufaa kulingana na malengo na madhumuni ya Mfuko.
Bodi kuidhinisha malipo
Kamati Tendaji
30.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu wa Bodi.
(2) Kamati Tendaji itakuwa na Wajumbe wafuatao:-
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambaye atakuwa Mwenyekiti.
Katibu Mtendaji wa Bodi ambaye atakuwa Katibu.
Afisa Elimu wa Halmashauri ambaye atakuwa Mjumbe.
Mweka Hazina wa Bodi ambaye atakuwa Mjumbe.
Mchumi wa Halmashauri ambaye atakuwa Mjumbe.

Kazi za Kamati
31. Kazi za Kamati Tendaji zitakuwa kama ifuatavyo:
kuandaa mipango kabambe ya elimu ya Halmashauri ambayo itatilia mkazo mahitaji yote ya Elimu ya Halmashauri kwa kuzingatia Mwongozo wa Kitaifa wa Mpango wa Elimu;
kuwezesha na kuratibu Vikao vya Bodi ya Mfuko wa Elimu pamoja na Mkutano Mkuu wa mwaka.
kuchambua na kubainisha maeneo ya kipaumbele kwa masuala ya Elimu katika Halmashauri;
kuweka taratibu na vigezo vya ufadhili wa wanafunzi na utoaji ruzuku kwa miradi ya Elimu katika Halmashauri.
kuandaa taarifa za utekelezaji za Mfuko wa Elimu na maendeleo ya elimu katika Halmashauri.
Mkutano Mkuu wa mwaka
32.-(1) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mfuko wa Elimu utakaokuwa na wajumbe wafuatao:-
wajumbe wote wa Bodi ya Mfuko wa Elimu.
kamati Tendaji ya Mfuko wa Elimu
wawakilishi toka madhehebu ya Dini.
wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii.

Majukumu ya Mkutano Mkuu
33. Bila kuathiri uwezo wa Bodi, Mkutano Mkuu wa Mwaka kitakuwa ndicho chombo cha;
kupokea taarifa za Ukaguzi wa Mahesabu na Utendaji wa Mfuko za mwaka.
kumteua Mwenyekiti wa Bodi na Wakaguzi wa Hesabu za Mfuko.
kuchagua wawakilishi wawili wa Bodi kutoka miongoni na Wadau wa Elimu.

Taarifa za mapato na matumizi
34.-(1) Katibu Mtendaji atatayarisha na kuwasilisha kwenye Bodi kila miezi mitatu taarifa iliyo na;
viashiria vya utendaji na taarifa nyingine zinazohusiana na shughuli za Bodi.
kazi zilizofanyika na mafanikio yaliyopatikana.
taarifa nyingine kwa kadri Bodi itakavyoona inafaa.

Taarifa za ukaguzi wa hesabu za mwaka
35.-(1) Katibu Mtendaji atatunza hesabu na kumbukumbu za shughuli zake, na atahakikisha kuwa fedha zote zilizopokelewa zinaingizwa kwenye Akaunti na kwamba malipo yote kutoka kwenye Mfuko yanafanywa kwa usahihi baada ya kuidhinishwa na ataweka udhibiti wa kutosha wa mali zake pamoja na madeni.

Sheria Na. 33 ya mwaka 1972
(2) Hesabu za mwaka za Mfuko wa Elimu wa Halmashauri zitakaguliwa na Mkaguzi na mtaalamu mwenye sifa ya ukaguzi aliyesajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Wahasibu na Wakaguzi ya mwaka 1972 na ambaye ameteuliwa na Mkutano Mkuu.
(3) Ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya mwisho wa kila mwaka wa fedha Bodi itatayarisha na kuwasilisha kwa Halmashauri Taarifa ya Fedha ya mwaka huo ambayo itajumuisha;
taarifa za Fedha
viashiria vya utendaji na taarifa nyingine zinazohusiana nazo.
taarifa ya utekelezaji ya Mfuko wa Elimu wa Halmashauri
 
Mkuu wa Wilaya kuwasilisha Taarifa ya Mwaka.
36. Mkuu wa Wilaya atawasilisha nakala ya Taarifa ya kila mwaka kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mfuko.
Bodi kuwa na uwezo wa kukagua
37. Bodi itakuwa na madaraka ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa hesabu za Mfuko wa Elimu.
38. Mtu yeyote ambaye;
atakwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi au;
atakayefanya kitendo chochote ambacho kitazuia Bodi au Kamati Tendaji kufanya kazi zake kwa ufanisi, au;
atatumia vibaya mali na rasilimali za Mfuko wa Elimu na kusababisha kutofikiwa kwa malengo yaliyowekwa, au
kwa uzembe, atashindwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi;
Atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atalipa faini isiyozidi shilingi Mia tatu Elfu (300,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili (12) au vyote faini na kifungo kwa pamoja.
Adhabu


                          Tangazo la Serikali Na. 207 la tarehe 29/05/2015

SHERIA YA FEDHA ZA SERIKALI   ZA    MITAA

_________

 

(SURA YA 290)

________

 

SHERIA NDOGO

_________

(Zimetungwa chin ya Kifungu cha 7 (1) na 16 (1)).

________

SHERIA NDOGO (ADA NA USHURU) ZA HALMASHURI YA  WILAYA YA  BUSEGA ZA MWAKA 2013



Jina na tarehe ya kutumika


Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo (Ada na Ushuru) za Halmashauri wilaya ya Busega za mwaka 2013 na zitaanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali.                                                           

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                   



Eneo la matumizi


Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililio chini ya malmaka ya Halmashauri ya wilaya ya Busega.                                                                                                             

                                                                                      



Tafsiri


Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapo elezwa au kufafanuliwa vinginevyo:-                         

 

“Ada” maana yake ni tozo, kodi, ushuru au malipo yatakayolipwa na mtu yeyote kwa Halmashauri kwa ajili ya kupata kibali,  huduma ya leseni, ukaguzi wa ramani  na majengo, ukaguzi wa viwanja, upimaji wa viwanja, uhamishaji miliki ya viwanja,  uchapishaji stakabadhi, zabuni, kodi ya pango na huduma nyinginezo,

“Afisa Mwidhiniwa” maana yake Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri au Mkurugenzi kwa ajili ya kutekeleza sheria Ndogo hizi pamoja na Mhandisi Ujenzi, Afisa ardhi Mteule, Afisa Afya, Afisa Biashara, Afisa Mipango Miji wa Halmashauri,

“Bidhaa” maana yake ni zao au kitu chochote kilichotengwa au   kuwekwa katika eneo lililotengwa au kuamriwa na Halmashauri  kuwa soko au eneo la kuuzia bidhaa,

“Barabara” maana yake ni barabara zote zilizo katika eneo la mamlaka ya Halmashauri zinazo milikiwa na kuhudumiwa na Halmashauri au Serikali Kuu,

“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya wilaya ya Busega,

“Machinjio” maana yake ni machinjio yanayo milikiwa na Halmashauri au sehemu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuchinja wanyama au kuanikia ngozi za wanyama waliochinjwa,

“Kibali” maana yake ni kibali chochote cha maandishi kilichotolewa na Mkurugenzi kwa mtu yeyote anayepata huduma yoyote au mtu anayepata huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi,

 

“Kodi ya pango” maana yake ni kodi ya pango itakayolipwa na mtu yeyote aliyepanga katika kibanda cha biashara, meza za soko, eneo au jengo lolote la Halmashauri pamoja na vibanda vya biashara vilivyojengwa na watu binafsi katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri,

“Jengo” maana yake ni jengo lolote lililojengwa kwa kutumia vifaa vya aina yoyote ile na ni pamoja na jengo liliojengwa kwa kutumia udongo, nyasi na miti, jengo la biashara, makazi, kibanda, konteina, mwavuli uliosimikwa kwa ajili ya shughuli za biashara katika eneo lolote ambalo limeruhusiwa kutumiwa na mtu kibiashara katika eneo la mamlaka ya Halmashauri,

“Kibanda” maana yake ni kibanda chochote cha biashara kilichojegwa katika eneo linalomikiwa na Halmashauri au mtu binafsi,

“Mazao” au “zao” maana yake ni mazao ya kilimo au misitu, pamoja na nafaka, ndizi mbivu, ndizi za kupika,miwa, matunda aina ya nanasi, machungwa, palachichi, tikiti-maji, maembe na mengineyo yenye asili hiyo,

“Mfanyabiashara” maana yake ni mfanya biashara yeyote anayeuza bidhaa katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri ni pamoja na mfanyabiashara ndogo-ndogo au machinga,

“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashsuri ya  wilaya ya  Busega pamoja na Afisa yeyote wa Halmashauri atakaye kuwa anatekeleza  majukumu ya Mkurugenzi kwa Mujibu wa Sheria Ngogo hizi,

“Mtu” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, taasisi, kampuni ambayo inafanya biashara ya aina yoyote katika eneo la Halmashauri,

 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Fedha za Serikali za Serikali za Mitaa, Sura ya 290,

 

“Stakabadhi” maana yake ni stakabadhi yenye nembo ya Halmashauri (HW 5) itakayotolewa na Halmashauri kama uthibitisho wa malipo ya ada,

“Soko” maana yake ni eneo au soko liliotengwa na linalomikiwa na Halmashauri kama soko kwa ajili ya huduma ya umma,

“Takataka” maana yake ni taka ngumu, taka maji au kimimnika, taka laini,

“Wakala” maana yake ni mtu aliyeteuliwa au kuingia mkataba na Halmashauri kwa ajili ya kukusanya ushuru au ada kwa niaba ya Halmashauri,

 



Mamlaka ya Halmashauri
 kutoza Ada.


4.— (1)   Kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi Halmashauri ndiyo yenye mamlaka pekee ya kutoza  ada ya huduma mbalimbali zitolewazo katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri. 

 

 

       (2)   Katika kutekeleza Sheria Ndogo hizi Halmashauri itatoza ada kwa kuzingatia viwango vya ada au ushuru vilivyo ainishwa katka Jedwali la Kwanza la Sheria dogo hizi.

      (3)   Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi utatozwa na kulipwa kabla ya kupata huduma.



Wajibu kila Mtu kulipa Ushuru


      (4)    Itakuwa ni wajibu wa kila mtu anayetakiwa kulipa ada au ushuru unaotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kulipa Ada au ushuru anaotakiwa kulipa.                                                   



Wajibu wa kila mtu kutunza stakabadhi



      (5)   Mtu yeyote atakaye lipa ada chini ya Sheria Ndogo hizi atapewa stakabadhi na kwa ajili ya ukaguzi wa malipo ya ada kila mtu kutunza stakabadhi aliyopewa kwa kipindi chote.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                           

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                    

      (6) Haitakuwa ni utetezi kwa mtu yeyote kudai kwamba amelipa ada stakabadhi lakini imepotea, ameisahau nyumbani au hajui alipoiweka.

                                                                                           



Ada na Ushuru kulipwa Halmashauri


      5.– (1) Ada inaotozwa chini ya  sheria Ndogo hizi utalipwa kwa Halmahauri au wakala aliyeteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kukusanya ada.

      (2)  Wakala atakayeteuliwa kukusanya ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi atawajibika kuzingatia Sheria Ndogo hizi.



Wajibu wa Mfanya biashara


6.—(1) Itakuwa ni wajibu kwa wa kila mtu chini ya Sheria Ndogo hizi kuhakikisha kwamba:-          

     

      Anafanyia biashara katika maeneo au masoko yaliyotengwa na kuruhusiwa na Halmashauri tu.

  



Bidhaa za nyumbani kutolipiwa Ushuru


      (2)   Bila ya kuathiri masharti ya Sheria Ndogo hizi bidhaa zote zenye uzani usiozidi kilo 50 zitakazoingizwa sokoni na mtu yeyote kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hazitatozwa ushuru au ada.                                                                               

(3)  Endapo bidhaa zilizotajwa katika kifungu cha 6 (2) cha Sheria Ndogo hizi zitawekwa au kutunzwa sokoni kwa muda unaozidi masaa 12 zitatozwa kodi kama bidhaa za biashara ya kawaida.                                                                                                              



Muda wa kulipa Ada au Ushuru



7. Ada au ushuru wowote unaolipwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi utalipwa kwa Halmashauri au wakala kabla ya kutoa au kupokea huduma, kibali au leseni isipokuwa kwa yale malipo ya ada au ushuru yanayolipwa kwa muda maalum. 

 



Ukusanyaji wa madeni ya ada.


8.   Endapo mtu yeyote anayetakiwa kulipa ada au ushuru atakataa au kushindwa kulipa ada au ushuru ndani ya muda unaotakiwa, Halmashauri inaweza kukusanya ada au ushuru unaodaiwa kwa njia ya kufungua shauri mahakamani kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha Sheria Ndogo hizi.                                                                                                                                                                                                                   

                       



Halmashauri kukusanya madeni kwa mujibu wa Amri ya XXXV  Sura ya 33


9.—(1) Bila  kuathiri  kifungu chochote  cha  Sheria Ndogo hizi, endapo  mtu, mmiliki  au mtumiaji  atakataa, atashindwa  au atapuuza  kulipa  ada, tozo  au  Ushuru  kwa muda  unaotakiwa, Halmashauri  itakuwa na mamlaka  na uwezo  wa kukusanya  ada yoyote  inayodaiwa kwa njia ya Mkato (summary procedure) Mahakamani.

      (2)   Kwa ajili  ya kutekeleza  kifungu cha  9  (1) cha Sheria Ndogo  hizi, bila kujali kama mali hiyo inaharibika haraka au haiwezi kuharibika, baada ya mahakama kutoa amri ya kukamta au kushikilia mali Halmashauri  itakuwa na uwezo wa kuuza  mali kwa njia  ya  mnada baada ya kupata kibali kibali cha mahakama.



Taarifa  au notisi  ya kuuza mali


–(1) Bila ya Kuathiri kifingu cha 9 (2)  cha Sheria Ndogo hizi Mkurugenzi anaweza kuiomba mahakama kutoa amri ya kukaamata na kuuza  mali  iliyokamatwa kwa njia ya mnada wa kawaida.

(2)  Utekeleza amri ya mahakama kwa mujibu wa kifungu cha 10 (1) utakuwa halali endapo  Mkurugenzi, kabla  ya  kuuza  mali  hiyo atatoa  notisi  au taarifa  ya siku 14 kwa maandishi  akimtaarifu  mmiliki, mtumiaji  au mtu yeyote  ambaye  mali yake  inatarajiwa kuuzwa  na Halmashauri.

 

(3)  Endapo  mwenye mali  atashindwa  kulipa  ada anayodaiwa ndani  ya  kipindi cha  muda  ulioelezwa katika notisi iliyotolewa kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) mali hiyo itauzwa na Mkurugenzi kwa mnada kwa kuzingatia Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hizi.

(4) Endapo mali yoyote itauzwa kwa mnada, Mkurugenzi atawajibika:-

 Kukata  gharama  zote za mnada,  ulinzi, usafiri endapo  mali itasafirishwa  kwa gari au gharama za  Halmashauri , ada, na deni linalodaiwa kutoka katika mauzo  ya mali na kuzikatia stakabadhi  ya mapato  ya Halmashauri.

 

Atarejesha  salio  lote  la mauzo  baada ya kutekeleza  kifungu  cha  10  (4) (a) cha Sheria  Ndog hizi kwa mmiliki  au mtumiaji.



Halmashauri  kutowajibika kwa hasara.


(5)  Halmashauri  haitawajibika  kwa namna  yoyote kwa hasara itakayotokana na  uharibifu wa mali utakaotokea  wakati wa kukusanya  madeni, ada, kukamtata au   kuhifadhi mali  zilizokatwa  na Halmashauri.  

Bila  kuathiri, kifungu chochote  cha Sheria  Ndogo hizi,  Afisa  Mwidhinishwa  au Mkurugenzi  anaweza kuingia  katika jengo, eneo  au mahali  popote  wakati wowote  wa saa za kazi za Umma  kwa ajili ya  kukagua  au kukusanya  mapato  yatokanayo  na ada au Ushuru.

  

 

 

 



Kila Mtu kusajiriwa Katika Rejista


11.—(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mtu katika eneo la mamlaka ya Halmashauri kuhakikisha kuwa amesajiriwa katika rejesta maalum ya Halmashauri, amelipa ada na kupata kibali kabla ya kuanza shughuli yoyote ya biashara.                   

      (2)   Mtu ayeyote atakayekiuka kifungu cha 11 (1) atakuwa ametenda kosa na endapo atapatikana na hatia atalipa faini ya tshs. 50, 000/=, ada ya kibali pamoja na ada au ushuru huika.



Mamlaka ya Wakala, Mkurugenzi na Afisa Mwidhiniwa.


12.   Bila ya kuathiri masharti yoyote yaliyowekwa na Sheria Ndogo hizi, Afisa Mwidhiniwa, Mkurugenzi au Wakala atakuwa na mamlaka ya kuingia katika jengo lolote kwa nia ya kukagua au kusanya ada au ushuru.                                        

                                                                                                                            

 

 

 



Makosa na Adhabu


13.—(1)   Itakuwa ni kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi endapo mtu yeyote atatenda kosa lolote lililoainishwa katika kifungu cha 13 (2) (a) hadi (i) cha Sheria Ndogo hizi.

(2)  Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kosa lolote lilioainishwa katika kifungu cha cha 13 (1) (a) hadi (i) cha Sheria Ndogo hizi atalipa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini(50,000/=) kwa kila kosa atakalokuwa ametenda pamoja na kulipa ada anayodaiwa, endapo:

Atafanya biashara katika eneo la mamlaka ya Halmashauri bila kupata kibali.

Atakataa au kushindwa kutii agizo lolote atakalopewa na Mkurugenzi au   Afisa Mwidhiniwa.

Atashawishi watu au kikundi cha watu kukataa, kugoma au kukwepa kulipa ishuru au ada.

Atamzuia afisa mwidhiniwa, wakala au Mkurugenzi kutekeleza majukumu yake ya kisheria.

Atafanyia biashara nje ya jengo, kibanda, soko, barabarani, kando au katika maeneo ya hifadhi ya barabara au katika maeneo yalisiyoruhusiwa.

Atashushia au kuuzia bidhaa au mazao kando kando ya barabara, nje ya soko au nje ya eneo la kushushi mizigo bila kibali cha Halmashauri.

Atatupa au kuacha uchafu au takataka katika eneo la biashara.

Atashushia mizigo katika maeneo yasioruhusiwa ikiwa ni maeneo yasiyokuwa soko.

Atajenga au kufanya maendelezo yoyote ya kiwanja bila kibali

Mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kutenda kosa lolote lililoanishwa katika kifungu cha 13 (2) (a) hadi (i) atahukumiwa kutalipa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) au kutumikia kifungo jela kwa muda mwaka mmoja au kifungo na faini vyote pamoja.



Tangazo la Serikali Na. 242 la 2004


Kwa ajili ya kuondoa shaka soko maana yake ni soko au eneo lolote lililo tengwa na kutangazwa na Halmashauri kuwa soko la Halmashauri.  

Ni marufuku kwa mtu yeyote au kikundi chochote kumiliki au kuendesha soko au masoko katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri bila kibali cha Halmashauri.

                       



Mkosaji kuwajibika kulipa gharama Halmashauri



14. Endapo Halmashauri itaamua kutekeleza Sheria Ndogo hizi kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika kifungu cha 9 (1) cha Sheria Ndogo hizi mtu yeyote atakayebainika kuwa ametenda atawajibika kuilipa Halmashauri gharama zozote zitakazojitokeza kutokana na utekelezaji wa amri ya Mahakama kulingana gharama itakayo kadiriwa na Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa.



Wajibu wa mlipa
ada kudai stakabadhi


15.  Itakuwa ni wajibu wa kila mtu anayetakiwa kulipa ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kudai na kuhakiksha amepewa stakabadhi yenye nembo ya halmashauri kwa kila ushuru au ada atakayolipa.

                                                                                                                                                                                                                                                                                                         



Mamlaka ya Halmashauri kuasamehe ada.


16.  Kwa kuzingatia Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290, Halmashauri kwa mujibu Sheria Ndogo hizi inaweza kufuta au  kusamehe ushuru, ada au mapato yoyote yaliyotakiwa kulipwa na mtu yeyote endapo itathibitika bila shaka kuwa shughuli anayofanya haina faida.                                                                                                             



Halmashauri kuteua wakala


17.  Kwa kuzingatia Sheria, Sura ya 290 na Sheria ya Manunuzi ya 2011, Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru au ada katika eneo lote au sehemu ya eneo katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri kwa ajili ya kukusanya madeni au ada inayotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.   



Wajibu wa Wakala.



     18.—(1) Wakala aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 17 cha Sheria Ndogo hizi, atakuwa na wajibu wa:-

  Kutoa taarifa ya maandishi kuhusu majina na orodha ya watu waliolipa au wanaotakiwa kulipa ada au ushuru ndani au sehemu ya eneo ambalo ameteuliwa kukusanya ada au ushuru.

 Kukusanya na kupokea ushuru au ada kutoka kwa kila mtu anayetakiwa kulipa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hizi

 Kuwasilisha kwa Halmashauri fedha zot alizokusanya kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi au mkataba wa uwakala

Kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa kuhusu majina au jina la yeyote aliyekataa au kushindwa kulipa kiasi cha deni analodaiwa.



Makosa ya Wakala.



      (2)  Wakala yeyote atakuwa ametenda makosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi endapo:-                                                                                                 

 Atashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri kiasi chochote cha fedha ya ada aliyokusanya

Atatoza kiwango cha ada kwa mtu yeyote kinyume na viwango vilivoainishwa  katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi

 

 Atatoa taarifa za uongo kwa sababu au njia yoyote kuhusu idadi ya waliolipa au wanaostahil kulipa, ada au kiasi cha ada aliokusanya.

Atashindwa kutekeleza wajibu wake kama wakala chini ya Sheria Ndogo hizi.

Atakusanya ada katika maeneo ambayo hayakuainishwa katika mkataba wake wa uwakala.

  Wakala yeyote atakayekiuka Sheria Ndogo hizi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na:-

 Kufungiwa kufanya kazi au biashara na Halmashauri kwa

          kipindi cha muda wa miaka isiyopungua au kuzidi mitano (5).

 Kulipa fidia kama itavyoamriwa na Halmashauri.

 



Uwezo wa Mkurugenzi kufifilisha makosa.


        19. Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, Mkurugenzi atakuwa na uwezo na mamlaka ya kufifilisha kosa lolote kwa  mtu yeyote kwa mkutoza faini isiyozidi shilingi elfu hamsini (50,000/=) endapo mtu huyo kwa hiari yake mwenyewe atakiri kosa lake kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum  kwa mujibu wa Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. na kukubali  kulipa kiasi cha  ushuru au ada anaodaiwa kulipa.  

20.  Kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi mtu yeyote atakaye ingiza gari la mizigo kwa ajili kushusha mazao yoyote nje ya soko la Halmashauri:-

Atalipa faini ya shiligi elfu hamsini (50, 000/=), na

 

Atalipa ushuru wa kushusha mazao (landing fees) kwa kiwango cha shilingi 100, 000/=kwa gari lenye uzito wowte, na

Atalipa ushuru wa mazao kwa kuzingatia kiwango cha ushuru   kilichoainishwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi.

d. Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumkamata mmiliki au dereva na gari au chombo kilichotumika kusafirishia mazao hayo na kumchukulia hatua za kisheria.

21.–(1) Hakuna mtu au mmiliki yeyote wa ardhi atakayejenga au kuendeleza kiwanja bila kibali cha ujenzi.

 (2) Maombi ya kibali cha ujenzi yaliyowasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa yataambatanishwa:-

(a) Ramani ya jengo ikionyesha pande zote za jengo, mwezeko wa jengo na kila hatua ya ujenzi unaokusudiwa kujengwa katika jengo.

(b) Stakabadhi ya malipo ya kiwanja na ada ya ukaguzi wa ramani

(c) Kivuli cha hati ya kiwanja kilichothibitishwa (legally certified or notarized copy)

(3)  Ni marufuku kwa mtu yeyote kujenga jengo, ukuta au sehemu yoyote ya jengo iliyobomoka au kubomolewa kwa makusudi kwa ajili ya ukarabati au marekebisho ya jengo bila kibali cha Halmashauri

(4)  Ni marufuku kwa mtu yeyote kubadili matumizi ya kiwanja au jengo kutoka matumizi au sura ya jengo kwenda kwenye sura nyingine au kwa ajili ya matumizi mengine bila kibali.



Tangazo la Serikali Na. 242 la 2004


(5)  Hakuna ujenzi wowote wa jengo utakaofanywa na mtu yeyote kinyume na Sheria Ndogo hizi pamoja Kanuni za Serikali za Mitaa (Mamlaka za wilaya) (Udhibiti wa Uendelezaji) yaani The Local Government (district Authorities) (development Control) regulations, 

Maombi ya kibali cha ujenzi yatawsilishwa na kwa Halmashauri kwa kutumia fomu maalum iliyotolewa kwa mujibu wa jedwali la Sita la Sheria Ndogo hizi

Endapo ujenzi utakao fanywa utakiuka masharti yaliyoanishwa katika kifungu cha 21 (4) cha Sheria Ndogo hizi au kinyume na vipimo au ramani ya jengo iliyoidhinishwa:-

Afisa Mwidhinishwa atakuwa na mamlaka na uwezo kisheria kumwamru mmiliki au mjenzi avunje jengo hilo kwa gharama zake mwenyewe.

 Afisa Mwidhinishwa anaweza kuchukua hatua za kisheria dhaidi ya mmiliki

Atasimamisha ujenzi unaofanywa au kuendelea.

JEDWALI LA KWANZA

 (Chini ya kifungu cha 4(1))

A.Ushuru wa Mazao

   Na.         Aina ya Mazao                               Kiwango cha Ushuru (Tshs)

Pamba…………………………………5%   ya bei ya mauzo sokoni

Mahindi……………………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Choroko na dengu…………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Karanga……………………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Maharage…………………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Matunda /ndizi …………………………………5% ya bei kwa tenga

Miwa………………………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Mchele……………………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Mpunga  na mazao mengine ya nafaka……5% ya bei ya mauzo sokoni.

Ushuru wa samaki na Dagaa……………….5% ya bei ya mauzo sokoni

Ushuru wa mabondo………………………5% ya bei ya mauzo sokoni

Mazao mengine ya samaki………………..5% ya bei ya mauzo sokoni

 

                  

 

Ushuru wa Mifugo (Mnadani)

Na.     Aina ya Mifugo                                   Kiasi cha Ushuru kwa Mfugo

Ng’ombe………………………………………………………5,000/=

Mbuzi………………………………………….........................3,000/=

Kondoo………………………………………………………  3,000/=

Nguruwe………………………………………………………3,000/=

 

 

 

C.Ushuru  wa Ukaguzi wa Nyama Machinjioni

Na.  Aina ya Mifugo                                         Kiasi cha Ada kwa mnyama (Tshs)

Ng’ombe…………………………………       3,000/=kila mmoja kila mmoja

Mbuzi…………………………………………2,000//=    kila mmoja

Kondoo……………………………………….2,000/=     kila mmoja

Nguruwe…………………………………….2.000/=    kila mmoja.

 

D.Ushuru wa masoko

Ushuru wa Kushusha Mizigo katika Eneo au Soko lolote liliotengwa na Halmashauri

Na.         Aina ya Mizigo na uzani                                      Kiwango cha Ushuru (Tshs)

Lori lililobeba Ndizi lenye  uzani wa tani 4  hadi 50……Tshs 20, 000/=

Lori  lililobeba Miwa, Machunga, Parachichi nyanya au Nanasi lenye

          uzani wa tani 4 hadi 50………………………………………Tshs 20, 000/=

Lori  lililobeba mbao, nguzo, milunda au magogo  lenye uzani wa

         tani  4 hadi 50……………………………………………………Tshs 40, 000/=

Tenga  au gunia la dagaa, Samaki ………………………………Tshs   1,000/=

Gunia  la Mahindi, Maharage ,Karanga, Mpunga  mchele, Ulezi ,           Kunde………………………………………………………..........Tshs 20,000/=

Tenga la Machungwa, Parachichi, Nanasi,

Papai au Nyanya………………………………………………Tshs  1, 000/=

E.Ushuru wa bidhaa mbalimbali katika masoko, minada,  magulio na maeneo mbalimbali yaliyotengwa na Halmashauri :

 

  Na.     Aina ya Bidhaa                 Kiwango cha Ushuru kwa siku (Tshs)

 

Ndizi za kupika…………………………………………Tshs. 1,000/= kwa siku,

Ndizi mbivu………………………… ………..Tshs.  1,000/=  kwa siku,

Nanasi……………………………………………Tshs. 1,000/= kwa siku,

Maparachici………………………………………Tshs. 1,000/= kwa siku,

Mboga-mboga……………………………………Tshs  1,000/=  kwa siku,

Nyanya/ nyanya mshumaa………………................Tshs. 1,000/= kwa siku,

Machungwa………………………………………Tshs. 1,000/= kwa siku,

Nguo za mitumba…………………………………Tshs. 1, 000/= kwa siku,

Nguo za madukani………………………………... Tshs. 1,000/= kwa siku,

Viatu vya mitumba……………………………… Tshs.  1, 000/= kwa siku,

Biashara ya Mama au Baba lishe…………………Tshs.  1, 00/= kwa siku,

Vileo………………………………………………Tshs.  1,000/= kwa siku,

Nyama au nyama choma…………………………Tshs.  2,000/= kwa siku,

Vyombo vya ndani……………………………      Tshs.  1,000/= kwa siku,

Urembo……………………………………...............Tshs. 1,00/= kwa siku,

Samani (furniture)……………………………       Tshs.  2, 000/= kwa siku,

Bidhaa mchanganyiko…………………………Tshs.  1,000/=kwa siku

Ushuru wa Samaki…………………………………Tshs.  500/= kwa siku,

Unga……………………………………………………Tshs.  100/=

Viazi mviringo/ viazi vya kawaida…………………Tshs.  1 00 kwa siku

 

 

F.Ada ya Kibali cha Kuvuna Mazao ya Misitu

Na.    Aina ya kibali            Kiwango cha Ada au Ushuru wa maombi ya kibali (Tshs)

Kibali cha Uchomaji mkaa………………………Tshs. 15, 000/=kwa mwaka

Usajiri wa biashara ya mazao ya misitu………………shs. 1,000. 000/= kwa mwaka.

 

 

      G.Ada ya Kibali cha Biashara mbalimbali zisizohitaji leseni.

               Na.  Aina ya kibali                  Kiwango cha Ada ya maombi ya kibali (Tshs)

Biashara ya mitumba nje ya maeneo ya magulio, soko na    minada  Tshs. 5000/= kwa  mwaka

Fundi viatu, cherehani, dobi, baiskeli…………….........……….…. Tshs. 3000/=kwa mwaka

Fundi  radio, TV, saa, kinyozi, saluni za wanawake/ wanaume ….Tshs. 5,000/= kwa mwaka

Mikokoteni, matoroli yenye magurudumu Mawili ……………….. Tshs. 1,0000/= kwa mwaka

Kibali cha biashara nyinginezo   zisizohitaji leseni ………………Tshs. 2, 000/=kwa mwaka

            H.Ada ya Kibali cha Ujenzi.

Na.   Aina ya kibali                                                Kiwango cha  Ada ya Kibali (tshs).

Ujenzi wa Nyumba ya makazi……………………                   Tshs  30, 000/=

Ujenzi wa minara …………………………………….              Tsh. 1,000,000/=

Ujenzi wa Ghala, Karakana, gereji  au karakana za magari          Tshs 200,000/=

Ujenzi wa kituo cha mafuta         …………………….…           Tsh 250,000/=

ujenzi wa Viwanda vidogo vidogo,  mashine  za kukoboa 

                         au kusaga   nafaka  (mchele, mahindi)…………………        Tshs 100,000/=

Ujenzi wa Nyumba ya ghorofa moja ……………………       Tshs 120,000/=

Ujenzi wa Kibanda  chochote  cha biashara……………….    Tshs 10,000/=

Ujenzi wa uzio wakati wa kujenga jengo lolote………………Tshs. 50, 000/=

I.Ada ya ukaguzi wa Ramani    

                                  

Na.         Aina ya Kibali                                       Kiwango cha Ada

Kukagua ramani ya jengo la  Nyumba ya makazi …………………Tshs. 40, 000/=

Kukagua ramani ya  Ujenzi wa Gorofa ……. Tshs. 15,000/=kwa kila hatua ya ujenzi.

Kuendelea na hatua ya ujenzi inayoendelea  baada ya kibali cha awali Tshs.5, 000/=

Ramani za maghala………………………………………………Tshs, 15, 000/=

Ramani za Makanisa na misikiti………………………Tshs. 15, 000/=

J.Ada ya kubadili matumizi ya Majengo na Ukaguzi wa Majengo.   

Kibali cha idhini  ya kubadilisha matumizi ya Ardhi/ viwanja kutoka:-

Makazi  kwenda biashara………….........................Tshs 50,000/=

Makazi kwenda  kwenda  viwanda…………………Tshs. 100, 000/=

Biashara Kwenda Makazi……………………………40, 000/=

Biashara/ makazi/ viwanda Kwenda matumizi Mengine…………………………………………….Tshs 100,000/=

Kibali cha idhini ya  kuhamisha  miliki

                                 ya Ardhi…………………Tsh 40, 000/=

K.   Ada ya Kuchangiaji  gharama za Upimaji na Usafishaji wa Viwanja

Na.      Aina ya Kiwanja                                        Kiwango cha Ada

  Kiwanja chenye Ujazo wa Msongamano Mkubwa (HD)…………Tshs. 40, 000/=

Kiwanja chenye Ujazo wa Msongamano wa Kati (MD)……………Tshs. 50, 000/=

Kiwanja chenye Ujazo wa Msongamano  Mdogo (LD)……………Tshs. 60, 000/=

Viwanja vya Taasisi za watu Binafsi/dini………………………Tshs    100,000/=

Mashamba…………………………………Tshs. 100, 000/= kwa kila ekari moja.

Kurudia upimaji upya baada ya mipaka kufutika 50% ya ada ya upimaji wa kiwanja au eneo husika.

Kurudia kuonyeshwa kiwanja baada ya ugavi wa awali kufanyika Tshs. 10, 000/=

.

L.Ada ya Leseni mbalimbali 

Na.  Aina ya Leseni au Kibali                                          Kiwango cha Ada         (Tshs).

Leseni ya pombe za kigeni……………………………Tshs 60,000 kwa miezi Sita

Leseni ya Pombe za Kienyeji…………………………..Tshs 20,000.kwa miezi sita

Ada ya leseni za Magobore ………………………………  Tsh. 10,000 kwa mwaka

 Ada ya zabuni

Na.  Aina ya Zabuni                                                Kiwango cha Ada  (Tshs)

Zabuni ya ujenzi wa majengo,

                                 barabara na miundo mbini mingine………………………………….100,000/=

Zabuni za uwakala mbalimbali ………………………………………100,000/=

Zabuni za ugavi wa huduma mbalimbali…………………………….100,000/=

N.Ada ya Uthamini wa Ardhi na Viwanja vya taasisi binafsi na watu binafsi

Na.     Aina ya Uthamini                       kiwango cha Ada (Tshs)

Kiwanja cha Ukubwa wowote………………10 % ya kiwango cha thamani ya kiwanja

Shamba lenye ukubwa wowote………………10% ya kiwango cha thamani ya shamba

               

O.Ada ya kibali cha kusafirisha ngozi

Na.  Aina ya Ngozi                                                                 Kiwango cha Ada (Tshs)

Ngozi za ng’ombe……………………………………….tshs. 10, 000/=

Ngozi za mbuzi………………………………………….Tshs. 10, 000/=

Ngozi za Kondoo………………………………………Tshs. 10, 000/=

P.Kodi , Ushuru  na Ada  ya kukodi  vifaa, mali  ukumbi na mitambo  ya Halmashauri.

Na.            Aina ya kibali                                                 Ada ya Kibali

Mitambo ya Halmashauri lori tani  7 hadi  10……………………Tshs  1500 kwa kilometa

Gari aina ya Landcruiser  au gari lolote…………………………Tshs  1300/=kwa kilometa

Ukumbi wa Mkutano wa Halmashauri:

Ukumbi mdogo  …………………… Tshs   100,000/ kwa siku moja

Ukumbi mkubwa…………………… Tshs.  200,000/ kwa sikumoja.

Vifaa/Mali za Halmashauri kiti au meza za ukumbi wa  mkutano  wa Halmashauri………………Tshs  300@kiti  Kwa siku

Maeneo ya wazi/ barabara  kwa ajili ya  shughuli  za promosheni na  matangazo  ya biashara………………Tshs  10,000/ kwa siku

Q.Ada na Ushuru  mbalimbali unaotozwa na Halmashauri

Ushuru unaotokana na mauzo ya bidhaa na huduma mbalimbali

Na.    Aina ya Bidhaa/ huduma                                    Kiwango cha Ada (Tshs).

Ushuru  wa michango  ya uchapishai wa vitabu  Vya  kukusanyia  mapato (HM5)…………………………………………..Tshs20, 000 kwa kila vitabu 20

  Ushuru  Huduma ya choo cha Halmashauri  … Tshs 300/= kwa haja ya ndogo au kubwa

Ada ya kibali cha kuendesha huduma ya  soko la binafsi/ taasisi Tshs. 500, 000/=

R.Ushuru wa maegesho standi na maeneo mengine

                                                                                

S/NO
AINA YA GARI
USHURU 
IDADI 
1
Mabasi /malori
Tsh, 3000/=
Kwa siku
2
Hice
Tsh, 2,000/=
Kwa siku
3
Taxi
Tsh 1000/=
Kwa siku
4
Bajaji
Tsh,1000/=
Kwa siku
5
Magari ya watu binafsi
Tsh. 500.-
Kwa siku

S.Ada ya ukaguzi wa Afya

S/NO
 
USHURU 
Idadi
\1
Ada ya kuandikishwa na usajili wa wahudumu kwa mtu mmoja
Tshs 12,000/=
Kwa mwaka
2
Ada ya kupima Afya kwa mtu mmoja
Tshs. 10,000/=
Kila baada ya miezi sita

 

T.Ushuru wa mbao za matangazo.

S/NO 
AINA YA TANGAZO 
USHURU 
UKUBWA 
MUDA
1
Matangazo yatakayobandikwa kwenye vibao na kuwekwa kando ya barabara kuu
Tsh.5,000/=
Kila ft1 ya mraba
Kwa mwaka
2
Matangazo ya biashara yanayobandikwa kwenye nyumba ya biashara
Tsh.2,000/=
Kila ft. 1ya mraba
Kwa mwaka
3
Matangazo ya biashara yatakayobandikwa kwenye nyumba za makazi
Tsh. 1,000
Kila ft 1 ya mraba
Kwa mwaka
4
Matangazo ya biashara kwa njia ya kipaza sauti
Tsh 50,000/=
Kwa siku moja
Kwa siku

 

 

 

U.Ushuru wa madini ya ujenzi

S/NO
AINA YA MADINI
USHURU                                UJAZO
1
CHANGARAWE / KOKOTO /MAWE/ KIFUSI
Tsh. 500/=  kwa kila tani  inayochimbwa au kusafirishwa

 

V.Kodi ya pango na majengo mengine ya Halmashauri.

S/No
Aina ya Jengo
Kodi ya Pango
Muda
1
Vibanda ndani ya soko
 Tsh.7, 000/=
Kwa mwezi

Vibanda nje ya soko
Tsh.5,000/=
Kwa mwezi
3
Vibanda ndani ya stendi
Tsh. 10,000/=
Kwa mwezi
4
Vibanda nje ya stendi
Tsh.5,000/=
Kwa mwezi
5
Nyumba ya makazi ya Halmashauri
Tsh.15,000/=
Kwa kila mpangaji kwa mwezi.

JEDWALI LA PILI

_________

Chini ya kifungu cha 19

_________

HALMASHAURI YA  WILAYA YA   BUSEGA

HATI YAKUFIFILISHA MASHITAKA/ KOSA.

Mimi …………………………………………….mwenye  umri wa miaka …………ambaye

Anuani yangu  imeandikwa hapo juu NAKIRI  kwa hiari yangu kwamba  nimekiuka kifungu cha …………………cha  Sheria Ndogo  za Ada  na Ushuru kwa kutenda makosa  yafuatayo;  (a) ………………….…………………(b) ………………………………………

( c )  ………………………………..……………(e ) ………………………..………………

Kwa hiyo naomba  na kukubali  Mkurugenzi wa Mji  Busega  afifilishe kosa/makosa hayo kwa mujibu

……………………………………….

Sahihi/Jina  la Mharifu /Mkosaji

Kwa matumizi ya Ofisi tu.

Mimi ……………………………………ambaye ni………………………….nikiwa afisa  Mwidhinishwa kwa mujibu  wa Sheria  Ndogo hizi kutokana  na  madaraka  niliyopewa  na  Mkurugenzi  wa Mji  Busega  kwa mujibu  wa kifungu cha  19  cha Sheria Ndogo za Ada na Ushuru, 2013)  NAFIFILISHA  KOSA lililotajwa hapa juu na kuamuru BW/MS ……………….. kulipa  Tshs…………………….kama faini  na zaidi ya  hapo

………………………………….

Jina  la Mhalifu/Mkosaji

Tarehe……………………

…………………………………………

Sahihi  ya Afisa  aliyefifilisha  kosa

Kwa  matumizi ya Idara ya Fedha.

Malipo  ya jumla  ya Tshs ………………….…………yamefanyiuka  kwa HW/ERV/Stakabadhi No……………………….ya tarehe  ……………………………………….iliyotolewa  kwa Mhasibu.

……………………………………

Sahihi ya Mhasibu

____

Fomu Na. BDC/CO/2

HALMASHAURI YA  WILAYA YA   BUSEGA

KIBALI CHA BIASHARA  ISIYOHITAJI LESENI

KIBALI HIKI  kinatolewa  kwa Mtajwa  hapo juu kwa ajili ya  kufanya biashara  ya ………………………………….. katika eneo  la  ………………………ambalo  liko  chini ya  mamlaka  ya Halmashauri  kuanzia  tarehe………………………..…………..hadi………………

Kwa  mujibu  wa kibali  na Sheria  Ndogo za Ada  na Ushuru  kibali  hiki kitakuwa  na masharti 

yafuatayo:

Kitakuwa  cha muda wa mwaka  mmoja tu.

Unatakiwa  kuzingatia  taratibu  na kanuni  za Afya.

Hutagawa  eneo au kibali  kwa mtu yeyote.

Utalipa ada  ya kibali  jumla  ya Tshs  …………………ambazo  hazitarejeshwa.

Kibali hiki kinaweza kufutwa  au kubatilishwa na Halmashauri  wakati wowote  kwa sababu maalum.

KIBALI  hiki  kimetolwea  na Mkurugenzi Mtendaji

…………………………………….

Mkurugenzi Mtendaji  /Afisa Mwidhinishwa

JEDWALI  la ………….

_________

(Chini ya kifungu cha 6 (1) (b) )

_________

KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA  BUSEGA.

HATI YA KUKAMATA MALI ZA KUIUZA.

KWA: 

          DALALI WA MAHAKAMA

M/S……………………………………….

……………………………………….

……………………………………….

Jina na aina  ya  mali…………………………..

Mahali malipo………………………………….

Jina la mmiliki wa mali………………………..

HII NI KUAMURU  kukamata na kutunza  mali inayoondosheka/isiyoondosheka  ya M/s………………………….ambayo  imeonyeshwa  katika Jedwali  mpaka hapo juu atakapolipaTshs ………zikiwa ni deni kwa kiwango  cha  2% kwa kila siku kuanzia 

tarehe …………mwezi……………mwaka  …………hadi tarehe………mwezi…………mwaka ………pamoja  na gharama  za kukamata  mali hiyo.

 

Na  baada ya  kutoa taarifa  (notice)  ya siku  kumi na nne (14)  ambayo itabandikwa  katika jengo  la Mahakama  na baada ya kumalizika kwa  taarifa  hiyo, mauzo  ya mali hiyo  yatafanywa  kwa mnada  wa hadhara  ili kupata  Tshs  ………pamoja  na gharama 

za kukamata  mali hiyo.

UNAAMRIWA kurudisha  hati  hii mnamo  au kabla  ya tarehe ……………..mwezi………………...mwaka…………pamoja  na maelezo  ya namna  ulivyotekeleza  amri hiyo au sababu  kwa nini  hukutekeleza  (kama ndivyo

IMETOLEWA na Mimi KWA MKONO WA AMRI  WANGU  na kugongwa  MUHURI  wa Mahakama  leo tarehe…………………mwezi…………………mwaka………………

………………………………….

HAKIMU

JEDWALI……..

________

(Chini ya kifungu cha  15 (5) )

_________

HALMASHAURI YA WILAYA YA  BUSEGA

Form Na…………………….

Kwa: Mkurugenzi (W),

           Halmashauri ya wilaya,

           S.L.P 190, BUSEGA

BPF . Na.BDC/………………                                                                   Tarehe………………

KIBALI CHA  UJENZI

(Kimetolewa chini ya kifungu  cha  15 (5) )

KIBALI  HIKI cha ujenzi  kimetolewa /kinakataliwa leo hii tarehe………..………………..…mwezi

……………………………mwaka…………………………………..…….kwa MS…………………..

Wa S.L.P …………………………kwa ajili  ya  kiwanja  Na……………Kitalu ………… eneo la ………………Katika  eneo la  mamlaka  ya Halmashauri.

 Kwa sababu  Mwombaji  ameambatanisha /hakuambatanisha  maombi  yake  ya kibali  cha     ujenzi na hati au  vielelezo  vifuatavyo

Stakabadhi  ya malipo  ya ada  ya kibali

Stakabadhi  ya malipo  ya ada ya ukaguzi  wa ramani

Ramani  ya  majengo

Nyaraka zozote zinazohusu  kiwanja  anachotaka kujenga

Stakabadhi  ya  malipo  ya ada ya upimaji (HW 5)

Stakabadhi  ya malipo  mengine  ya Serikali

Mkataba  wa mauzo  ya plot  (kama upo);

Nakubali/ Nakataa kuwa ramani  ya majengo  inakidhi / haikidhi  masharti ya kiafya au  matumizi

ya kiwanja  na hivyo aendelee/ asitishae ujenzi  na kurkebisha ramani..

                                                       ………………………………………

Mhandisi  Ujenzi  /Mkurugenzi (W).

*Futa  isiyohusika

Tarehe………………………

 

 

Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Busega December 15, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili Mwaka 2022_Wilaya ya Busega January 04, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2022_Wilaya ya Busega January 29, 2023
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI BUSEGA LAITAKA RUWASA KUJIRIDHISHA NA TAKWIMU ZA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI

    November 18, 2022
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa