Utekelezaji Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji;
Idara ya mipango na takwimu inajumuisha wataalamu wa mipango na takwimu ambao kwa ujumla wanasimamiwa na Afisa mipango wa wilaya. Idara ya mipango ndiyo inayoratibu shughuli zote za miradi ya maendeleo pamoja na kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi hiyo mfano taarifa za robo mwaka, taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, uratibu wa uandaaji wa bajeti na utekelezaji wake, n.k. Taarifa hizi hupelekwa ngazi za juu kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.
Majukumu ya idara hii kiutawala yameainishwa kuonesha majukumu ya mtakwimu na majukumu ya wachumi/mipango ila katika utekelezaji majukumu haya hutekelezwa kwa pamoja. Pamoja na kuahinishwa kwa majukumu hayo, pia Idara kwa mujibu wa waraka mpya wa muundo wa Idara za Halmashauri, Idara ina sehemu kuu tatu;
Majukumu ya Mipango (Sera na Mipango & Tathmini na Ukaguzi wa Miradi)
Kuratibu masuala yote ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kuandaa mpango na taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha tawala kwa kipindi cha miaka mitano,mwaka mmoja na nusu mwaka.
Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini ubora wa mradi na thamani ya fedha iliyotolewa (value for money)
Kuratibu miradi iliyofadhiliwa na Wahisani wilayani.
Kuratibu Mipango na Bajeti ikiwemo Mpango Mkakati na Mipango kazi ya wilaya.
Kuunganisha, kuratibu na kufuatilia Mipango na Bajeti za Serikali za mitaa.
Kushiriki katika kufuatilia, kukagua na kutoa tathmini kwenye miradi ya maendeleo wilayani ili kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa kazi za serikali.
Kushiriki katika kuandaa taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kuratibu shughuli za tafiti zote wilayani, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya mapato vya Halmashauri.
Kuchapisha machapisho mbalimbali ya kiucumi na kijamii wilayani.
Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja.
Idara ya Mipango ndiyo Sekretarieti katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC).
Kuratibu masuala ya Maafa katika wilaya.
Kazi Za Mtakwimu Wa Halmashauri
Mtakwimu wa Halmashauri anashiriki katika kazi zote za kitakwimu zinazofanyika katika halmashauri. Mtakwimu anafanya kazi chini ya usimamizi wa Afisa Mipango Wilaya. Kazi za mtakwimu wa wilaya ni kama ifuatavyo;
Kushirikiana na idara zote za kisekta (kwa mafano Afya, Elimu, Kilimo, n.k) ndani ya Halmashauri ili kuwa na mfumo mzuri wa kitakwimu.
Kuandaa mkusanyiko wa takwimu za kiuchumi na kijamiiā(Socio economic profile),
Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa zoezi la Sensa ya idadi ya watu na Makazi.
Mtakwimu pia ni mwenyekiti wa kikundi kazi cha ukusanyaji wa takwimu ndani ya Halmashauri (District Statistics Working Group).
Kufuatilia mwenendo wa mfumo wa utunzaji wa takwimu katika ngazi ya serikali za mitaa(LGMD) na kushirikiana na idara nyingine zenye mifumo mingine ya utunzajia wa takwimu za kisekta kwa mfano;
Maliasili - NAFOBEDA, Afya - MTUHA na Elimu - BEST.
LGMD - Local Government Monitoring database, BEST-Basic Education Statistics na NAFOBEDA - National Forestry and Beekeeping Database
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa