Majukumu ya Idara ya maji
Kutafsiri na kusimamia sera za Wizara ya Maji katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya.
Kusimamia, kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayorudisha nyuma huduma ya upatikanaji wa maji.
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Halmashauri ya Wilaya, mashirika yasiyo ya kiserikali, binafsi na kidini kuhusu namna ya kushirikiana kukabili tatizo la upatikanji wa huduma ya maji ndani ya Wilaya.
Kusimamia na kuratibu miradi yote ya maji ndani ya wilaya,
Kuandaa Bajeti ya mwaka ya Mishahara, shughuli za uendeshaji na Miradi ya Maendeleo kwa upande wa Idara ya maji,
Kutoa ushauri kwa serikali kuhusu Sera ya Sekta ya Maji na kudurusu sera, sheria na kanuni zake, na
Kuratibu na kushauri mfumo wa matumizi bora ya miradi ya maji ili iwe endelevu.
Kupata taarifa zaidi za Wizara ya Maji, tembelea tovuti hii: http://www.maji.go.tz/
Kupata taarifa na Takwimu Mbalimbali za Maji, bonyeza kwenye kiunganishi hiki: http://water.opendata.go.tz
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa