Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega imetembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Busega. Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Daudi Ng’hindi imefanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Juni, 2021. Katika ziara hiyo Kamati ya Siasa imeweza kutembelea miradi ya sekta ya elimu, maji, afya, na kwa sehemu kubwa imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Katika ziara hiyo, Kamati ya Siasa imeweza kutoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi kwa lengo la kuleta ufanisi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali. Katika ziara hiyo Kamati ya Siasa imetaka kuwepo kwa mambo muhimu yafuatayo;
Elimu
Miradi liyotembelewa katika sekta ya elimu ni mradi wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi 1 Shule ya Msingi Mirambi kwa gharama ya TZS Milioni 30, ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa Shule ya Msingi Mwanangi kwa gharama ya TZS Milioni 60, madarasa yamekamilika na yanatumika, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Sekondari Nyaruhande kwa gharama ya TZS Milioni 21.3, ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari Gininiga kwa gharama ya TZS Milioni 13, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Msingi Fogofogo na matundu 7 ya vyoo kwa gharama ya TZS Milioni 47.7, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Sekondari Kabita kwa gharama ya TZS Milioni 40, ujenzi umekamilika, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 7 ya vyoo Shule ya Msingi Itongo kwa gharama ya TZS Milioni 47.7 ujenzi umekalika, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 7 ya vyoo Shule ya Msingi Mwamajashi kwa gharama ya TZS milioni 47.7, ujenzi umekamilika.
Afya
Ujenzi wa wodi tatu za wanaume, wanawake na watoto Hospitali ya Wilaya ya Busega, ambapo Serikali imetoa kiasi cha TZS Milioni 500. Ujenzi wa majengo hayo unaendelea. Ujenzi, ukarabati wa vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji Kituo cha Afya kiloleli kwa gharama ya t TZS Milioni 27, ujenzi, ukarabati wa miundombinu ya vyoo vya Watumishi na uwekaji wa miundombinu ya maji Zahanati ya Badugu kwa gharama ya TZS Milioni 20, ujenzi wa vyoo vya wagonjwa na watumishi na uwekaji wa miundombinu ya maji kwa gharama ya TZS Milioni 20 Zahanati ya Ngasamo, ujenzi wa vyoo vya watumishi na uwekaji wa miundombinu ya maji Zahanati ya Shigala kwa gharama ya TZS Milioni 20, ujenzi wa vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji kwa gharama yaTZS Milioni 25, ujenzi wa miundombinu ya vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji Zahanati ya Kijesrishi kwa gharama ya TZS Milioni 20.
Maji
Ujenzi mradi wa tanki la maji Mkula wenye thamani ya TZS Bilioni 2.1 ambapo tanki hilo lina ukubwa wa lita 300,000. Ujenzi unaendelea na mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 60, ukamilikaji wa mradi huu utahudumia watu 16,108 ambapo vituo 33 vitajengwa kwaajili ya huduma ya maji Wakazi wa Mkula, Lutubiga na Kijerishi.
Pia kamati hiyo imeweza kutembelea ujenzi wa mradi wa maji Mwamanyili ambao tahamani yake ni TZS Milioni 227.7 ambapo utekelezaji wa mradi huu ni asilimia 45 mpaka sasa. Ujenzi wa tanki wa mradi huo wenye ukubwa wa lita 225,000 umekamilika hatua iliyobaki ni kuanza usambazaji maji kwa watumiaji.
Miradi Mingine
Mradi mwingine ambao ulitenmbelewa na ziara hiyo, ni mradi wa ujenzi wa soko la Masanza Kata ya Kiloleli, ambapo kamati ilifika kukagua ujenzi wa choo cha Soko ambacho kimegharimu TZS Milioni 6. Katika ukaguzi wa choo hicho kamati imeagiza Ofisi ya Mkurugenzi kuendelea na jitihada za kuweka miundombinu katika choo hicho ikiwemo maji na umeme ili kuweka mazingira bora pale kitakapoanza kutumika.
Aidha, kamati ya siasa Wilaya ya Busega imeweza kufika katika Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS), ambapo walitembelea AMCOS ya Bushigwamh’ala iliyopo Kata ya Kalemela na AMCOS ya Kijerishi iliyopo Kata ya Mkula, kukagua na kujionea hali ya ununuzi wa Pamba. Kamati hiyo ikiwa katika AMCOS hizo imeweza kupata taarifa kutoka kwa viongozi lakini pia kusikiliza changamoto wanazokutana nazo, hasa wauzaji wa Pamba ili kuzifanyia kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Anderson Kabuko amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo na kuahidi kutekeleza mambo yote yaliyoelekezwa na kamati hiyo ili kuendelea kuboresha huduma Wilayani Busega kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega Mhe. Daudi Ng’hindi, amesema ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kikamilifu ni muhimu kuwa na ushirikiano katika kutekeleza miradi hiyo, na kuzingatia maelekezo yanayotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa