Katika matokeo ya Mitihani ya Elimu ya Msingi, Wilaya ya Busega imeng’ara kwa ufaulu wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga kidato cha kwanza katika Shule mbalimbali za serikali kwa ngazi ya elimu ya sekondari nchini. Mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi iliyofanyika tarehe 11 na 12 mwezi septemba 2019, takwimu zinaonesha ufaulu katika Wilaya ya Busega umeweza kuongezeka kwa 8.28% ukilinganisha na mwaka jana; ambapo ufaulu mwaka huu 2019 ni 90.2% ikilinganishwa na mwaka jana 2018 ambapo ufaulu ulikuwa ni 81.99%.
Jumla ya wanafunzi wapatao 5513 walifanya mitihani ya kuhitimu elimu ya Msingi, kati yao wasichana walikuwa 2806 na idadi ya wavulana ilikuwa 2707, waliofaulu ni 4973 ambapo wasichana jumla yao ni 2470 na wavulana ni 2503. Kati ya waliofaulu jumla ya wanafunzi 3220 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye Shule mbalimbali za Sekondari. Kwenye idadi hiyo ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kati yao wasichana ni 1614 na wavulana ni1606. Kwa upande mwingine jumla ya wanafunzi 1754 ikiwa wasichana ni 855 na wavulana ni 899 hawakuchaguliwa kujiunga licha ya kufaulu mitihani yao kutokana na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na idadi ya Shule zilizopo.
Kwa upande wa ufaulu ngazi ya mkoa, Wilaya ya Busega imeweza kushika nafasi ya pili ikiwa na kiwango cha ufaulu wa 90.27% ikitanguliwa na Wilaya ya Bariadi iliyoshika nafasi ya kwanza, Mkoa wa Simiyu. Licha ya kushika nafasi ya pili kwa ngazi ya Mkoa, Wilaya ya Busega imeweza kutoa wanafunzi bora kimkoa katika nafasi ya kwanza mpaka ya nne.
Wanafunzi waliofanya vizuri kwa ngazi ya Wilaya ni Busumba Peter Charles, kutoka Shule ya Msingi Nyashimo, aliyeshika nafasi ya kwanza na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wavulana Mzumbe, nafasi ya pili ikishikwa na Ngulung’wa Selemani Zacharia kutoka Shule ya Msingi Mwamagulu na amechaguliwa kujiunga Shule ya Sekondari ya Wavulana Iliboru, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Johnson Goodluck John kutoka Shule ya Msingi Nasa, pia amechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Mzumbe. Kwa nafasi ya tano imeshikwa na Maria Paul Balekele kutoka Shule ya Msingi Nyaluhande na amechaguliwa kuijunga na Shule wasichana Msalato.
Pamoja na kushika nafasi za juu kwenye ngazi ya Wilaya, pia wanafunzi hao wnne (4) wameweza kuingia kwenye kumi (10) bora Kitaifa, na kuipeperusha vyema Wilaya ya Busega kitaaluma. Kwa upande mwingine wastani wa kwa ngazi ya mkoa ni sawa na 126.36% ikiwa na kiwango cha ufaulu 86.46% na kushika nafasi ya nane (8) Kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa