• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAZEE BUSEGA WAADHIMISHA SIKU YA WAZEE, WAISHUKURU SERIKALI KWA KUTOA USHIRIKIANO

Posted on: October 1st, 2020

“Familia na Jamii Tuwajibike Kuwatunza Wazee”, hii ndiyo kaulimbiu ya kilele cha siku ya Wazee mwaka huu. Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani hufanyika ifikapo tarehe 01 Oktoba kila mwaka. Wilaya ya Busega imeweza kuazimisha siku hiyo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu wazee katika ukumbi wa Silsos, Nyashimo.

Mgeni rasmi katika siku hiyo Wilayani Busega Mhe. Tano Mwera, Mkuu wa Wilaya ya Busega, ameeleza kwamba serikali inajali na kutambua mchango wa wazee nchini hivyo waondoe shaka kuhusu masuala yanayowahusu na kuongeza kwamba serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha wazee wanatunzwa na jamii kama kaulimbiu ya mwaka huu isemavyo.

Aidha Mhe. Mwera ameagiza kuwe na utaratibu wa ushiriki wa wazee katika shughuli za maendeleo kwa ngazi ya vijiji kwani wengi wao hawana uwezo, hivyo wasilazimishwe kushiriki katika shughuli za maendeleo. Kwa upande mwingine ametoa angalizo kwamba wazee wasitumie uzee kukwepa ushiriki wao kwenye shughuli za maendeleo, hasa kwa wale wanaojiweza.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Dismas Ijagala, amekiri kwamba wazee wana nafasi kubwa katika maendeleo na kwa kupitia mipango mbalimbali ya Kitaifa ikiwemo Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF. Mpango wa TASAF Wilayani Busega una jumla ya kaya lengwa 3,065 na kati ya hizo kaya za wazee zilizopo kwenye mpango ni 822, aliongeza Mratibu wa TASAF Wilaya ya Busega Bi. Wema Mmari.

Awali Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Godfrey Mbangali amewahakikishia kwamba matibabu ya wazee hayana malipo kama Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 inavyoagiza. Pia Dkt. Mbangali alianisha baadhi ya magonjwa yanayowasumbua zaidi wazee ikiwemo magonjwa ya moyo, mifupa, matatizo ya macho na saratani. Tunaendelea kuboresha zaidi huduma za afya kwa wazee. Tumeweza kuanzisha chumba cha wazee kwenye Hospitali yetu ya Wilaya na tunazo dawa asilimia 95.8% kwa magonjwa ya wazee, aliongeza Dkt. Mbangali.

Kwa upande wa Uongozi wa Baraza la Wazee Busega linaishukuru serikali kwa ushirikiano wao na kujali mchango wa wazee katika jamii. Tunaishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtandaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega kwa kushirikiana na kuwa kama mlezi wa Baraza la Wazee Busega kwani hata kodi ya Ofisi yetu inalipwa na Ofisi ya Mkurugenzi, na mambo mengine mengi ikiwemo kutuwezesha baiskeli mbili kwaajili ya Uongozi wa Baraza la Wazee, alisema Katibu wa Baraza la Wazee Busega Ndg. Kapeje Linti.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa