Watumishi kada ya Afya Wilayani Busega wamepewa Mafunzo ya Mfumo wa Kuhifadhi Taarifa na ukusanyaji Mapato ijulikanao kama GoT-HoMIS ambao hutumika kwa Ngazi ya Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili tarehe 29 hadi 30 Julai 2021 katika ukumbi mdodgo wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
Akifunga Mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria amesema hatowaonea aibu wote ambao watagundulika kutotumia mfumo wa GoT-HoMIS, na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Kabuko amesema Vituo vya Afya na Zahanati ambazo hazitumii mfumo wa GoT-HoMIS kumekuwa na makusanyo madogo ukilinganisha na Vituo vya Afya na Zahanati ambazo mfumo unatumika. Bw. Kabuko amesema baada ya Mafunzo hayo atafutilia kwa uaribu matumizi ya mfumo huo katika maeneo yote ya kutolea huduma za Afya.
Kwa upande mwingine, Mhe. Gabriel Zakaraia ametoa tahadhari kwa wote ambao wanajihusisha na wizi wa dawa katika maeneo ya kutolea huduma za Afya na kusisitiza kwamba, yeyote atakebainika kuiba dawa atachukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine.
Nao washiriki wamesema kwamba licha ya changamoto zilizpo ikiwemo changamoto ya miundombinu ya umeme, lakini wanaamini mfumo huo utarahisisha ukusanyaji wa mapato ambapo utasaidia vituo vya Afya na Zahanati kutumia mapato hayo kuboresha huduma za Afya.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa