Viongozi mbalimbali wa ngazi tofutti wa serikali ya vijiji na vitongoji wameapishwa wilayani Busega mnamo tarehe 27.11.2019. Viongozi hao wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji na Wajumbe wa halmashauri ya vijiji wamekula viapo vya uaminifu, na utii na uadilifu.
Jumla ya washindi 1431 kwa idadi ya Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji na Wajumbe wa halmashuari ya Vijiji; wakiwemo wenyeviti wa vijiji 59, wenyeviti wa vitongoji 361, wajumbe viti maalum 429 na wajumbe mchanganyiko 582. Viongozi waliopishwa wakitoka vijiji 59 na vitongoji 361 kati ya vitongoji 362 ambapo uapishaji huo ulifanyika katika kata zote 15 zilizopo wilayani humo.
Uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa na vijiji ulifanyika tarehe 24.11.2019 sehemu mbalimbali nchini na kushuhudia wagombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa kwa asilimia kubwa maeneo mbalimbali.
Kwa upande wa Wilaya ya Busega uchaguzi huo haukutofautina na maeneo mengine ya nchini, kwani asilimia 100% ya walioapishwa walitoka chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama washindi katika maeneo yao.
“Kwa ujumla hali ya uchaguzi ilikuwa na mchakato mzuri kuanzia mwanzo mpaka hitimisho lake na ushirikiano ulikuwa ni mkubwa mpaka kufikia leo siku ya kuapisha viongozi watakaokuwa viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji vilivyopo wilaya ya Busega”, Grace Ishengoma, Afisa Uchaguzi (W).
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa