Wananchi Jimbo la Busega wamejitokeza kwa wingi kupiga kura katika vituo mbalimbali vilivyopo jimboni humo. Mapema kuanzia saa moja kamili (1:00) Asubuhi vituo vilikuwa vimefunguliwa tayari kwa wapiga kura kuanza kuchagua viongozi wanaowataka.
Wapiga kura wapatao 124,316 ambao walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wataweza kupiga kura. Jumla ya vituo 325 vilivyopo katika kata zote 15 Jimbo la Busega vimefunguliwa na zoezi la kupiga kura linaendelea. Aidha, ulinzi umeimarishwa ili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kuchagua viongozi wanaowataka.
HABARI ZAIDI ZITAENDELEA KUTOLEWA..............
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa