Watumishi wa kada ya Ualimu Wilayani Busega wapewa mafunzo ya Mfumo wa Madeni ya Watumishi Serikalini ujulikanao kama MADENI MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM (MadeniMIS) wenye lengo la kuhakiki na kuthibitisha madeni ya Watumishi wa Serikali yasiyo ya mshahara.
Pichani ni Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu kutoka Wilaya ya Busega Wakiwa wanafuatilia kwa umakini Mafunzo ya MadeniMIS
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili ambapo washiriki wakiwa ni Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu, na Wasaidizi wao pamoja na Waratibu wa Elimu ngazi ya Kata, ambapo yameanza kutolewa kuanzia tarehe 02 hadi 03 Oktoba, 2020 katika ukumbi wa Silsos, Nyashimo.
Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha watumishi wa serikali kuweza kuanzisha uingizaji wa madai yao kwenye mfumo ili baadae Walimu Wakuu na Wakuu wa shule waweze kuhakiki na kupitisha madai kwa ajili hatua za kubaini madeni ya Watumishi wa Serikali.
Awali Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Mussa Mmbyana amewataka Walimu kuwa makini wakati wa mafunzo hayo ili kufanikisha lengo la mafunzo hayo. Mafunzo ya MadeniMIS yametolewa na Maafisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
Pichani ni Kaimu Afisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Chrispinus Christian akitoa Mafunzo ya Mfumo wa MadeniMIS kwa Washiriki.
Mfumo wa madeni ya Watumishi Serikalini, MadeniMIS una lengo la kuratibu madeni na madai ya Watumishi wa Serikali yasiyo ya mshahara nchi nzima lakini kwa kuanzia utaanza na madeni ya Walimu. Aidha mfumo huu utapunguza malalamiko ya madai na madeni ya Watumishi wa Serikali.
MWISHO.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa