• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VYAMA VYA SIASA WILAYANI BUSEGA VYATAKIWA KUFUATA MAADILI YA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2020

Posted on: August 5th, 2020

Vyama vya siasa wilayani Busega vyatakiwa kufuata maadili, taratibu na kanuni za uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya Kabuko wakati wa kikao na Viongozi wa Vyama vya Siasa wilayani Busega kilichofanyika tarehe 05/08/2020.

Ndugu Kabuko ambaye ni Msamizi wa Uchaguzi Jimbo la Busega, amevitaka vyama vya siasa vilivyopo wilayani Busega kuwa na utulivu na kufuata sheria na kanuni za uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu na kuwaasa kuteua wagombea watakaokuwa na mawazo chanya hivyo kukubalika na wananchi.

Utakapofika muda sahihi wa kufanya kampeni, tufanye vizuri kampeni kwa kuzuia taharuki, kuzuia mihemko na uchochezi ili kupita salama katika jambo hilo, na naomba Mwenyezi Mungu atusimamie tuweze kusimamia salama mpaka mwisho wa zoezi hili, aliongeza Ndugu Kabuko.

Kwa upande mwingine Kabuko amevitaka vyama vya siasa na wagombea wao kujikita hasa katika sera na sio vingenevyo, hii itasaidia kuwa na hoja ambazo hazitakuwa na uchochezi hivyo kuzuia vurugu na taharuki kwa wapiga kura.

Awali mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Busega, Ndugu Rutagumirwa Rutalemwa amesisitiza vyama vya siasa na wagombea watakaopata nafasi ya kugombea kuzingatia maagizo ya maadili yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili nchi yetu iweze kupita salama kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba. Ameongeza kwamba vyombo vya usalama na ulinzi wilyani Busega vitafanya kazi kwa muda wote ili kuhakikisha amani inatawala kwa kipindi chote cha uchaguzi. Tutumie lugha za ustarabu na staha ili kuepuka lugha za matusi na tuheshimu utu wa mtu, alisema Ndugu Rutalemwa.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Busega Bw. Hamad Mabula amewaomba wawakilishi hao wa vyama vya siasa kwamba TAKUKURU itakua macho muda wote na haitasita kuchukua hatua kwa mtu yoyote kutoka chama chochote atakayefanya vitendo vitakavyoashiria rushwa. Tutamkamata, kumhoji na kumfikisha mahakamani mtu yoyote wakati na baada ya uchaguzi kama tutakuwa na mashaka ya vitendo vyovyote vya kuashiria rushwa, aliongeza Bw. Mabula.

Jumla ya vyama vitano (5) vya siasa vilivyothibisha ushiriki wao katika uchaguzi mkuu wilayani Busega, vimeweza kushiriki katika kikao hicho ambacho kilimalizika kwa wawakilishi hao kufurahishwa na hatua mbalimbali zinazoendelea kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu. Vyama vilivyoshiriki ni pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Civic United Front (CUF), Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) na United Democratic Party (UDP).

Washiriki wote kutoka vyama vitano vya siasa wametolewa hofu juu ya  kutokuwepo na misongamano kwa wapiga kura kwenye vituo ili kutoa fursa kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura kutimiza haki ya kikatiba kwa kuchagua viongozi anaowataka, alisema hayo Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Busega Bi. Grace Ishengoma wakati akijibu swali la mwakilishi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Mkeshi Mhoja aliyekuwa na hoja kuhusu idadi ya wapiga kura kwa kila kituo. Kikao hicho pia kilihudhuliwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo na baadhi ya Watumishi wengine kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa