• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

UHAKIKI WA KAYA ZILIZOPO KWENYE MPANGO WA TASAF WAFANYIKA KWA UFANISI MKUBWA WILAYANI BUSEGA

Posted on: July 27th, 2020

Zoezi la uhakiki wa kaya zilizopo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kipindi cha kwanza awamu ya tatu limefanyika wilayani Busega huku kukiwa na muitikio mkubwa wa walengwa hivyo kuwezesha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi mkubwa. Zoezi hilo lililokuwa la siku tatu limeweza kufanyika kwa mafanikio makubwa huku kaya 3155 zikihakikiwa kati ya kaya 3826 zilizokusudiwa, huku baadhi ya kaya zikiwa zimehama makazi yao hivyo kukosa sifa ya kaya lengwa.

Nuru Mkomambo, mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF Taifa, alisisitiza ushirikiano wa viongozi kwa ngazi mbalimbali ni moja ya njia sahihi ya kufanikisha zoezi hilo la uhakiki wa kaya masikini. Aidha aliongeza kwa kuwataka wawezeshaji kuwa na uadilifu katika zoezi hilo ili kutimiza lengo la zoezi.

Uhakiki umefanyika katika vijiji 41 kati ya 59 vilivyopo kwenye mpango wa TASAF kipindi cha kwanza awamu ya tatu. Mpango wa TASAF ni miongoni mwa dhima kubwa na kipaumbele cha kupunguza umasikini kwa kaya masikini nchini Tanzania, huku kaya lengwa zikiwa na matumanini makubwa katika mpango huu.

Kufanyika kwa uhakiki huo kuna kuna dhima ya kujua uhai wa kaya lengwa kwaajili ya kutekeleza kipindi cha pili awamu ya tatu. Mpango wa TASAF ni chachu kubwa ya kuboresha maisha ya kaya na mtu binafsi huku kaya zikijikita kwenye shughuli za maendeleo ikiwemo ufugaji, biashara ndogondogo, kusomesha watoto na shughuli za kilimo. Baadhi ya walengwa wamekiri kwamba mpango huu wa TASAF ni mkombozi kwao kwakua umefanya maisha ya kaya nyingi kuinuka kiuchumi kwa kujishughulisha na ujasirilimali.

Awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Mussa Mbyana akifungua mafunzo kwaajili ya uhakiki kwa wawezeshaji, aliwataka wawezeshaji wa zoezi hilo kuwa na maadili na ufanisi na hakutakuwa na mzaha kwa atakaye vuruga zoezi hilo kwani lengo la serikali hali ya umaskini nchini chini ya mpango wa TASAF.

Mratibu wa mpango wa TASAF wilaya ya Busega Bi. Wema Mmari  amekiri kuwa kuna mwamko mkubwa kwa kaya lengwa katika zoezi la uhakiki. Kata zote 15 zilizopo wilayani Busega zimekuwa katika mpango wa TASAF kipindi cha kwanza awamu ya tatu. Jamii na kaya lengwa zimekuwa zikipata elimu ya kuhakikisha maisha yao yanaboreshwa kutoka katika utegemezi kwa kutumia fedha wanazopata kikamilifu kwa mambo yenye tija ya ushawishi wa maendeleo.

Kwa kuona umuhimu wa mpango wa TASAF, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, tarehe 17 Februari, 2020 alizindua TASAF kipindi cha pili awamu ya tatu. Mpango ambao unatarajia kugharimu tirioni 2 za kitanzania kwaajili ya kutoa ruzuku kwa kaya masikini nchni.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa