• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Kafulila Asikiliza Kero za Wananchi wa Kata ya Kiloleli; Awatoa Hofu ya Changamoto Zinazowakabili

Posted on: September 25th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amefanya ziara Kata ya Kiloleli Wilayani Busega kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi wa Kata hiyo siku ya tarehe 24 Septemba 2021, na kuwatoa hofu juu ya kero na changamoto zinazowakabili.

Mkutano huo uliochukua takribani masaa matatu umewapa fursa wananchi wa Kata ya Kiloleli kueleza kero na changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa kero zilizowasilishwa na wananchi hao ni pamoja na changamoto za upatikanaji wa maji baadhi ya maeneo, changamoto ya barabara, umeme, maji na uvamizi wa wanyama wakiwemo Viboko na Tembo.

Pamoja na wananchi hao kueleza kero zao mbele ya Mhe. Kafulila ambapo aliwataka wataalam alioambatana nao kutoka Wilayani Busega kutoa maelezo ya changamoto zilizowasilishwa na wananchi na zile ambazo hazikuwa na maelezo ya papo hapo aliwaeleza wananchi wa Kata hiyo kwamba ataendelea kuzifuatilia kwaajili ya kuzipatia utatuzi.

Mbali na hayo, Mhe. Kafulila amewatoa hofu wananchi wa Kiloleli kwa kuwaeleza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ina azma na malengo ya kuhakikisha inasimamia Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ili kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, Mhe. Kafulila amesema kwamba kwa kudhiirisha hilo, tayari Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kuleta fedha kwaajili ya Miradi mbalimbali ikiwemo Miradi ya Elimu, Afya, Maji na Barabara. “Mkoa wetu umepokea kiasi cha Tshs Bilioni 12 kwaajili ya ujenzi wa Barabara Vijijini, zaidi ya Tshs Bilioni 8.8 kwaajili ya Miradi ya Maji, na miardi mingine mingi”, aliongeza Kafulila.

Wananchi wa Kata hiyo pamoja na kueleza kero na changamoto zao pia wameiomba Serikali kujenga chuo cha ufundi Mkoa wa Simiyu na Wilayani Busega ili kuwawezesha vijana ambao hawapati nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari na elimu ya juu kujinga na masomo ya ufundi. Akieleza kwa kina juu ya suala hilo Mhe. Kafulila amesema katika Mkoa wa Simiyu hakuna vyuo vya ufundi ambavyo vipo chini ya VETA, lakini juhudi tayari zimeanza hivyo taratibu zote zikikamilika Mkoa utapata chuo cha ufundi VETA ili kuwawezesha vijana kupata fursa ya masomo ya ufundi, hivyo wananchi wawe na subira.

Mhe. Kafulila anaendelea na Utaratibu wake wa kusikiliza kero za wananchi maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu, na hii ni zaidi ya mara tatu kufanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi Wilayani Busega.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa