Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda, amewaagiza, wakuu wa Wilaya, Maafisa Tarafa na watendaji wa Kata mkoani humo, kushughulikia utatuzi migogoro ardhi katika maeneo yao, amesema hayo alipofanya ziara Wilayani Busega tarehe 15 Agosti 2022.
Katika ziara yake Wilayani Busega kujitambulisha kwa watumishi wa umma na makundi mbalimbali, ikiwemo wazee, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Nawanda, anasema utatuzi wa Migogoro ya ardhi ni miongoni mwa vipaumbele vyake, na kutoa maelekezo viongozi wa Wilaya, Tarafa na kata, kutenga muda wa kutatua migogoro
Aidha Dr. Nawanda amesisitiza suala la ukusanyaji mapato kwa Halmashauri zote Mkoani Simiyu ili kuweza kupata fedha za kuhudumia wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria, amemhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo mpya kwamba Wilaya ya Busega ipo tayari kushirikiana nae katika kutekeleza majukumu mbalimbali. Aidha Zakaria amewakumbusha wakazi wa Busega na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi Agosti 23, mwaka huu.
Akiwa Wilaya Busega mkuu huyu wa Mkoa pia amekagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya hii na Kituo Cha Afya Mkula, na baadae kuongea na Watumishi wa Umma wa Wilaya ya Busega.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa