• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RAIS SAMIA: Serikali Itajenga Stendi na Soko Lamadi

Posted on: February 4th, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itajenga kituo cha mabasi na soko katika mji wa Lamadi Wilayani Busega. Samia ameyasema hayo wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Mara leo tarehe 04/02/2022 ambako atakuwa na ziara ya siku nne.

Akiongea na wakazi hao wa Lamadi ambao walijitokeza asubuhi na mapema kwa wingi, Rais Samia amesema suala la stendi tumelichukua na Serikali itajenga kituo cha mabasi na soko. “Nimemsikia hapa Mkuu wa Mkoa amesema kiasi cha ujenzi wa stendi ni takribani TZS bilioni 1.6, kwa kiasi hicho cha fedha Serikali hainshindwi kujenga stendi, tutajenga hiyo stendi na soko hapa Lamadi” aliongeza Mhe. Samia.

Aidha, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha wanatatua kero za wananchi wa Lamadi ya kuvamiwa na wanyama ikiwemo tembo na viboko. “Pamoja na juhudi mnazoendelea kufanya lakini hakikisheni mnaweka kituo cha maliasili maeneo haya ili kupunguza adha ya wanyama hatarishi kwa wananchi”, alisema Rais Samia.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ameweza kueleza juhudi kubwa ambazo Serikali ya awamu ya sita inazifanya katika mkoa wa Simiyu, ikiwemo uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, shule na huduma za maji na kueleza baadhi ya kero na changamoto zinazowakabili wakazi wa Lamadi ikiwemo kutokuwepo kwa stendi na soko la uhakika ambavyo vimekuwa kero kwa wakazi hao. Kafulila amesema Simiyu imekuwa ikiendelea kwa kasi kutokana na juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. “Katika kipindi cha awamu ya sita mkoa wa Simiyu umepokea zaidi ya TZS bilioni 126 kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Simiyu, aliongeza Kafulila.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Busega Simon Songe amemshukuru sana Mhe. Rais kwa kazi anayoendelea kuifanya kwani mpaka sasa mambo makubwa yamefanyika katika Wilaya ya Busega, hivyo anashukuru sana kwa maendeleo yanayoendelea kufanyika chini ya Serikali sikivu ya awamu ya sita. “Tunashukuru sana kwa fedha nyingi ikiwemo fedha za ujenzi wa madarasa 95 ambayo yamesaidia upungufu wa madarasa katika jimbo la Busega, kwani watoto wote waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza wameanza masomo kwa pamoja, sisi wananchi wa Busega hatusemi tu kwamba unaupiga mwingi bali unaupiga mwingi sana”, aliongeza Songe.

Pamoja na hayo, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Busega Veronica Sayore kwa kusimamia vyema ujenzi wa vyumba vya madarasa 95 yaliyojengwa chini ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19. “Kituo nilichotoka nimetengua wakurugenzi wanne kutokana na ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha, kwako sijasikia kwahiyo endelea kuchapa kazi Mkurugenzi” aliongeza Rais Samia.

Akiongelea suala la ufanyaji wa biashara ndogondogo, Rais Samia amewataka wafanyabiashara wadogo maeneo ya Lamadi na Sehemu nyinginezo kuwa wavumilivu kwani Serikali ina mpango mzuri juu yao ya kutenga maeneo ya kufanya shughuli zao za biashara. “Serikali ina mpango mzuri, tukifanikiwa Tanzania itakuwa na maeneo mengi ya kufanyia biashara kwa muda wa masaa ishirini na nne” alisema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan anaeleka mkoani Mara kwa ziara ya siku nne, pamoja na mambo mengine atashiriki kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo kitaifa yanafanyika siku ya kesho tarehe 05/02/2022 mkoani humo.

MWISHO 

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa