Kutokana na tamko la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alilotoa tarehe 29, Desemba, 2019 kwa wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa vyumba vya madarasa vikamilike kwa wakati ili wanafunzi wote waliochagulia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 waanze masomo kwa pamoja.
Kauli hiyo imechukuliwa kwa uzito na utekelezaji wake umekuwa wa kuridhisha kwa Wilaya ya Busega. “Ujenzi wa madarasa ni chachu kubwa ya kuleta ubora wa elimu na kuwezesha kila aliyepata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari anapata fursa hiyo” amesema hayo Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera.
Mkuu wa wilaya ya Busega Mh. Tano Mwera ameendelea kufanya ziara sehemu mbalimbali wilayani humo ili kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na upatikanaji wa madawati kwaajili ya kufikia lengo la serikali kuruhusu wanafunzi waliokosa nafasi kuingia kidato cha kwanza wanaanza masomo yao mapema mwezi Machi.
Mhe. Tano Mwera ameendelea uhamasishaji wa ujenzi vyumba vya madarasa katika kata ya Lutubiga na kuelekeza viongozi wa kata kuhakikisha ujenzi wa madarasa ni kipaumbele kwa ajili ya kufikia lengo la serikali.
Pamoja na changamoto za elimu zilizopo wilayani humo, Mhe. Tano Mwera ameelekeza njia mbadala zitumike, ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaendelea na masomo mpaka hapo ujenzi wa vyumba vya madarasa utakapokamilika. Jumla ya wanafunzi 3220 wilayani Busega walichaguliwa kujiunga elimu ya sekondari kwenye shule mbalimbali za serikali.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa