Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega yamefanyika leo tarehe 09 Agosti 2021. Bi. Veronica Sayore ambae ni Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Anderson Kabuko.
Katika makabidhianao hayo Bi. Sayore amesema anategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Wilaya pamoja na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega na kusisitiza kwamba bila ushirikiano hakuna kitakachoweza kufanyika. Aidha Bi. Sayore ametoa pongezi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Anderson Kabuko kwa kipindi chote alichoweza kuhudumu kama Mkurugenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega na kwa hatua kubwa ya utendaji wake.
Kwa upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Anderson Kabuko amewashukuru Watumishi wote na kuahidi kwamba ataendelea kutoa ushirkiano pale watakapoona inafaa ili kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wa Busega. Mwenyeketi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mhe. Sundi Muniwe amesema anaamini watafanya kazi kwa ushrikiano na anamkaribisha sana Bi. Sayore katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria ametoa shukrani kwa Bw. Anderson Kabuko kwa kipindi walichoweza kufanya kazi pamoja na anaamini kwamba Mkurugenzi aliyekabidhiwa Ofisi ataendeleza ushirikiano wa utendaji kazi kati ya Ofisi ya Mkurugenzi na Ofisi yake. Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Kamati ya Ulizni na Usalama Wilaya ya Busega, baadhi ya Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo na baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa