Taasisi za kibenki zatakiwa kutoa mikopo Zaidi kwa wakulima ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya kilimo. Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane kitaifa tarehe 01/08/2020, yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu.
Maonesho ya Nanenane ya 28 Kitaifa kufanyika yameweza kufunguliwa huku taasisi za kifedha za Benki za CRDB, NMB na NBC zikiwa ni wadhamini wakuu wa maonesho. Katika hotuba yake Mhe. Makamu wa Rais Mhe. Samia amezitaka taasisi hizo za kifedha kuwekeza Zaidi kwenye sekta ya kilimo ili kuleta ubora wa wakulima kwa kutumia teknolojia ya kisasa Zaidi katika kilimo, uvuvi na ufugaji nchini, kutoka asilimia 9% tu ya mikopo inayotolewa hivi sasa kwenye sekta ya kilimo.
Uwekezaji wa mikopo kwenye sekta hii utasaidia kuboresha kilimo cha umwagiliaji hivyo kuwa na akiba kubwa ya chakula nchini. Kuwezehswa kwa wakulima kuna manufaa makubwa kwa nchi na uchumi wa wakulima wetu nchini aliongeza Mhe. Samia.
Aidaha Mhe. Samia amewataka wataalam wa tafiti za kilimo kutoa taarifa sahihi kwa maafisa Ugani ili kuwezesha kusambaza taarifa kwa wakulima katika maeneo yao. Ameongeza kwamba tafiti nyingi zinafanyika lakini haziwafikii walengwa hivyo kukosa taarifa sahihi jinsi ya kuboresha kilimo, uvuvi na ufugaji nchini.
Kwa upande mwingine Mhe. Samia suluhu amezindua jengo la Wizara ya Kilimo mkoa wa Simiyu ambapo linatarajiwa kutoa huduma za elimu na ushauri katika sekta ya kilimo kwa ujumla, na kutaka uwepo wa jengo hilo kuwa na malengo yaliyokusudiwa na sio vingenevyo. Kuwepo kwa jengo hili ni fursa kubwa ya kutoa dira kwenye sekta hii hasa kudhibiti uvuvi haram ambao miaka ya karibu umekuwa changamoto na kusababisha upotevu mkubwa wa samaki katika ziwa Viktoria, kuboresha ufugaji wa kisasa na kufanikisha kilimo cha umwagiliaji.
Maonesho ya Nanenane yanafanyika mara tatu mfululizo mkoani Simiyu yenye kauli mbiu isemayo Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020, yameacha alama kubwa kwa wakulima, wafugaji, na wavuvi. Kilimo, ufugaji na uvuvi ni moja ya shughuli kubwa zinazifanywa nchini Tanzania, huku mkoa wa Simiyu ukiwa miongoni mwa mikoa inayolima mazao ya biashara huku zao la pamba likiwa linazalishwa kwa wingi. Shughuli za uvuvi kupitia ziwa Viktoria na ufugaji wa mifugo mbambali ikiwemo Ng’ombe, Kondoo na Mbuzi.
Mhe. Samia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea viwanja vya maonesho hayo ili kujifunza shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kupata elimu Zaidi ili kuboresha shughuli zao hivyo kuifanya sekta hii kuwa na matokea chanya katika maendeleo ya uchumi wa nchi.
Awali Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ameeleza mikakati ya Wizara ikiwemo usajili wa wakulima ili kupata takwimu sahihi ya wakulima nchini, kufanikisha huduma ya bima ya mazao na utafiti wa kilimo hasa kwenye mbegu bora na teknolojia katika sekta ya kilimo. Huku akihamasisha ushiriki wa wananchi kushiriki ipasavyo maonesho ya Nanenane kwani mchango mkubwa kwa wakulima, wana ushirika na wadau wengine kujifunza mbinu mbalimbali ambazo zitaboresha
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa