Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, wameazimia kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la kukusanya Zaidi ya aasilimia 100 ya bajeti ya shillingi biloni 32.39 kwa mwaka wa fedha 2022/23 ili kuweza kupata fedha za kuhudumia wananchi. Wamesema hayo katika baraza la kufunga mwaka 2021/2022 lililofanyika tarehe 21/08/2022.
Kwa mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri ya Wilaya ya Busega imekusanya asilimia 99 ya mapato yake ikilinganishwa na asilimia 74 walizokusanya mwaka 2020/21.
Katika mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri imejiwekea malengo ya kukusanya zaidi ya asilimia 100 ya bajeti yake ya kukusanya na kutumia shilingi bilioni 32.39, ambapo ili kufikia azma hiyo, madiwani wanawataka watendaji wa Serikali kusimamia ipasavyo vyanzo vya mapato na ukusanyaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bi. Veronica Sayore amesema kwamba tayari mikakati zaidi imeimarishwa ili kufikia matarajio ya kuhakikisha makadirio ya bajeti yanafikiwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Busega Mhe. Sundi muniwe amesema kwamba upatikanaji wa mapato ya kutosha utasaidia Wilaya ya Busega kuendelea kwani fedha hizo zitatumika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.Wilaya ya Busega.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa