Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amuagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Busega kuwahamishia Maafisa Kilimo sita ambao walikuwa wakifanya kazi Makao makuu kwenda Katika Kata ambazo hazina Maafisa Kilimo ili kuweza kujikita zaidi katika masuala ya uzalishaji na kusaidia kutoa ushauri wa kitaalamu moja kwa moja kwa Wananchi waliopo katika maeneo ya Kazi, Pia Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alielekeza pikipiki zote zilizopo katika makao makuu ya Wilaya ukiachilia za Idara ya Afya na Elimu zipelekwe Katani na Vijijini ili kusaidia Maafisa Kilimo na Ugani wanaofanya kazi katika Kata na Vijiji. Aidha, kwa pikipiki zitakazobakia Makao makuu ziwekwe kwenye Pool na utaratibu uandaliwe kila atakae kuwa na uhitaji wa kutumia kwa utekelezaji wa Kazi za Serikali apatiwe.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa