• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kamati ya Siasa yaridhishwa na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

Posted on: February 13th, 2021

Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa. Kamati hiyo ilifanya ziara ya siku mbili kati ya tarehe 12 hadi 13 Februari 2021 ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa.

Picha: Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega ikiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha Wanawake kijulikanacho kama Umoja kilichopo kata ya Nyashimo, ambacho kinafaidika na mkopo zinazotokana na fedha za mapato ya ndani.

Kamati hiyo iliweza kutembelea miradi 8 na kujionea jinsi utekelezaji wake unavyoendelea. Pamoja na kujionea utekelezaji wa miradi hiyo kamati imetaka kutatuliwa haraka changamoto zinazoathiri ukamilikaji wa miradi kwa wakati.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Daudi Ng’hindi amesema kwamba anawashukuru watumishi wa Wilaya ya Busega kwani wanaofanya kazi kwa kujituma na anawataka waendelee kufanya kazi kwa kujitoa ili kufikia lengo la Serikali.

Picha: Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Burilo Deya akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega, kamati hiyo ilipotembelea Shule ya Msingi Irambo kujionea utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu shuleni hapo.

Aidha, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Burilo Deya amesema changamoto zote zillizojitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo zitafanyiwa kazi na ameitoa hofu kamati hiyo, huku akieleza kwamba utekezaji wa miradi mbalimbali unakwenda vizuri kama kamati ilivyoweza kutembelea licha ya changamoto ndogondogo.

Kamati hiyo iliweza kutembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu kwenye Shule ya Sekondari Antony Mtaka, ambapo kamati iliweza kujionea miundombinu ya ujenzi wa Bwalo, Maabara, Madarasa na Vyoo kwa thamani ya TZS Milioni 196.6.

Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Venance Mabeyo na kujionea ujenzi wa Maabara, Madarasa na Vyoo kwa thamani ya TZS Milioni 46.3, Shule ya msingi Irambo ambapo utekelezaji wa ujenzi wa madarasa na vyoo kwa thamani ya TZS Milioni 66.6, ujenzi Jengo la Utawala Wilaya ya Busega ambalo linagharamu zaidi ya TZS bilioni 4.9 ambapo limeanza kutumika huku vyumba 68 vikiwa vimekalika kati ya vyumba 97 na ujenzi wake unaendelea.

Picha: Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega ikiwa mbele ya Jengo la Uthibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Busega.

Aidha kamati hiyo iliweza kutembelea ujenzi wa Jengo la Uthibiti Ubora wa Shule, ambapo ujenzi wake unagharimu zaidi ya TZS Milioni181.1, upanuzi wa wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mwamagigisi na ujenzi wa Jengo la Rafiki kwa Vijana (Youth Friendly Corner) ambapo ujenzi wake ni TZS Milioni 33. Kwa upande mwingine kamati iliweza kutembelea miundombinu ya barabara kata ya Lamadi na kumpongeza meneja wa TARURA Mhandisi Mwita Muhochi kwa jitihada anazozifanya kuhakikisha barabara zinapitika lakini kamati imemtaka kuongeza nguvu ya ujenzi wa barabara maeneo mbalimbali wilayani Busega ikiwemo zilizomo kwenye kata hiyo. . Kamati pia iliweza kutembelea kikundi cha Wanawake kijulikanacho kama Umoja ambacho kimepatiwa mkopo wa TZS Milioni 3.5, fedha zinazotokana na mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya wilaya ya Busega. kikundi hicho kinachopatikana kata ya Nyashimo kinajuhusisha na ufugaji wa Mbuzi.

Picha: Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Busega wakiwa ndani ya Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Mhandisi wa Majengo Wilaya ya Busega Bw. Paul Tumbu (wa kwanza kulia) akiwaonesha wajumbe wa kamati hiyo alama mbalimbali zilizopo kwenye jengo hilo.

Awali Mhe. Ng’hindi amesisitiza kwamba utekelezaji wa miradi hasa wa ujenzi wa majengo unahitaji umakini ili kuwa na uimara wa majengo hayo. “Tunahitaji kuwa na majengo bora na sio bora majengo” aliongeza Mhe. Ng’hindi. Hata hivyo kamati hiyo imewataka watumishi wilayani Busega kufanya kazi kwa kujitoa, lakini imetoa pongeza kwa Mhandisi wa majengo Wilaya ya Busega Bw. Paul Tumbu kwa kusimamia vyema ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Picha: Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Busega ikiwa ndani ya Jengo la Maabara linalojengwa Shule ya Sekondari Antony Mtaka. Kamati hiyo ilifanya ziara shuleni hapo kujionea ujenzi wa miundombinu mbalimbali. 


Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa