Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwezi Oktoba 2020, jumla ya wagombea 37 wameteuliwa kugombea nafasi ya ubunge na nafasi za udiwani Jimbo la Busega.
Kuteuliwa kwa wagombea hao kumeenda sambamba na kubandikwa kwa majina ya wateuliwa kwenye Ofisi ya Msamizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo kwa nafasi ya wagombea Ubunge na Ofisi za wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kwa nafasi za Udiwani.
Zoezi la kuchukua fomu kwa nafasi hizo lilianza tarehe 12/08/2020 na kuhitimishwa tarehe 25/08/2020, ambapo wagombea wenye vigezo na sifa wameweza kuteuliwa kwa hatua inayofuata, ikiwemo zoezi la pingamizi kwa wagombea na baadae kuanza rasmi zoezi la kampeni kwa wateuliwa ambao hawatakuwa na pingamizi.
Kwa upande wa Ubunge jumla ya wagombea wanne (4) ambao ni Ndg. Simon Songe Lusengekile kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Adam Alphonce Komanya kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ndg. Laulensia Yahona Machanya kutoka Civic United Front (CUF), na Ndg. Selemani Misango kutoka chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) wameweza kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Busega.
Kwa upande wa ngazi ya udiwani jumla ya wagombea 43 walichukua fomu ambapo 35 kati yao walirudisha fomu huku idadi ya walioteuliwa ikiwa ni 33 kutoka vyama vya CCM, CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo.
Jimbo la Busega ni miongoni mwa majimbo saba (7) yaliyopo mkoa wa Simiyu. Jimbo la Busega linasimamiwa na msimamizi uchaguzi ngazi ya Jimbo, Ndg. Anderson Njiginya Kabuko. `
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa