Halmashauri ya wilaya ya Busega imeweza kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kuendelea kuleta tija na hamasa ya utendaji kwa viongozi na watumishi wa wilaya ya Busega. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Busega, Anderson N. Kabuko wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG).
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Busega kwa kupata hati safi na kwa utelezaji wa miradi mingi ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa serikali ya awamu ya tano. Ameongea hayo wakati wa kikao hicho cha Baraza la Madiwani la kujadili majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mtaka ametoa pongezi kwa viongozi wa wilaya hiyo kwa usamizi wao mzuri wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Busega ambao umekamilika. Ukamilikaji wa Hospitali hiyo ya wilaya umeenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Afya vinne katika kipindi hicho cha miaka mitano.
Kwa upande mwingine, miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, miradi ya maji, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara na usambazaji wa umeme katika vijiji, imeweza kutekelezwa kwa hatua nzuri kwakweli sina budi kuwapongeza kwa utendaji wenu wa pamoja, mafanikio hayo ni ya pamoja kama viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa kwa ujumla, alisema Mtaka.
Licha ya Mhe. Mtaka kutoa pongezi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano chini ya serikali ya awamu ya tano, pia ametoa wito kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busega kuendelea kufanya kazi kwa kujituma na kwa ubunifu unaoendana na fani zao, ikiwemo kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato ya halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa