HATUA MUHIMU ZA KUZINGATIA ILI KUJIUNGA NA BIMA YA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF Iliyoboreshwa):
Hakikisha kila mwanakaya amepatiwa kitambulisho cha uanachama.
KUMBUKA:
MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF ILIYOBORESHWA) NI NINI?
Ni mpango muhimu wa hiari ulioanzishwa kwa Sheria Na. 1 ya mwaka 2001 (Sura ya 409 ya Sheria za Tanzania Toleo la 2002) wa kaya, kikundi au familia au mtu binafsi kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua.
KAYA/FAMILIA NI NINI KWA MUJIBU WA CHF ILIYOBORESHWA?
Baba, mama n watoto/wategemezi ambao jumla yao ni watu sita (6). Kundi la watu sita (6) katika taasisi kama vile shule (wanafunzi), Ushirika (wanaushirika), ama Vikundi vya ujasiria mali (SACCOS, VICOBA, n.k). Uandikishaji wa Wanachama sita (6) kwa gharama ya TZS 30,000 kwa matumizi ya mwaka mzima.
FAIDA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII:
USHIRIKI WA MWANACHAMA KATIKA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA:
Mwanachama atashiriki katika kuboresha huduma za Afya kupitia mwakilishi wa jamii katika bodi ya Afya ya Wilaya na kamati za uendeshaji na usimamizi wa Kituo cha Afya na Zahanati.
Mwanachama atawasilisha mawazo/kero zake kwenye serikali ya kijiji, na kupelekwa kwenye kamati ya CHF ya kata na hatimaye kwenye bodi ya CHF ya wilaya ambayo itayajadili na kuyatolea maamuzi.
Pia, mwanachama ataweza kutoa maoni yake kuhusu maboresho ya CHF na huduma za Afya kupitia mkutano wa mwaka wa kijiji wa wanachama wa CHF.
Kwa Maelezo zaidi tembelea Ofisi ya Mratibu wa CHF Wilaya au Wasiliana na Ofisi ya Kijiji/Mtaa iliyokaribu nawe.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega
Sanduku la Posta: 157 BUSEGA
Simu ya Mezani: +255 282 981 193
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: info@busegadc.go.tz
Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa