• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
BUSEGA DISTRICT COUNCIL
BUSEGA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busega

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Dhamira
      • Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utawala na Utumishi
        • Mipango, Takwimu na Ushirika
        • Elimu Msingi
        • Afya
        • Maendeleo ya Jamii na ustawi wa jamii na Vijana
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maji
        • Elimu Sekondari
        • Ardhi na Maliasili
        • Fedha na Biashara
        • Ujenzi na Zimamoto
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Kitengo cha Sheria
        • Kitengo cha Ugavi
        • Uchaguzi
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Afya
    • Elimu
    • Maji
      • Kilimo
        • Kilimo
    • Kilimo
      • Kilimo
    • Mifugo
    • uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya, Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya W\heshimiwa Madiwani
        • Kuonana na Mwenyekitiwa Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali za Maombi
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Maendeleo
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RAS Mmbaga: Tuboreshe huduma za Afya ya Mama na Mtoto

Posted on: April 23rd, 2021

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Miriam Mmbaga ametaka suala la huduma za Afya kuwa ni mojawapo ya vipaumbele katika mkoa wa Simiyu, hasa Afya ya mama na mtoto. Ameyasema hayo alipofanya ziara Wilayani Busega na kukutana na watumishi wa idara ya Afya. Ziara hiyo iliyofanyika tarehe 22 Aprili, 2021 wilayani Busega ililenga kujadili hali ya vifo vya akina mama na watoto, kukagua ujenzi wa miundombinu katika hospitali ya Wilaya ya Busega na kituo cha Afya Lukungu.  

Mmbaga amesema suala la Afya ni muhimu sana kwa wananchi, kwani kukosekana kwa Afya iliyo bora hupunguza nguvu kazi, hivyo huathiri uchumi wa Taifa. “Ili kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto ni vyema viongozi kuacha mitazamo hasi, ambayo huathiri sekta ya Afya na kupelekea athari nyingi kwa wananchi ikiwemo vifo kwa wakina mama vinavyotokana na uzazi”, alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga ametaka uwepo wa uwazi na uwajibikaji ili kuboresha huduma za Afya Wilayani Busega. “Tuwe na utamaduni wa kuwa na uwazi na uwajibikaji, ili kuleta ufanisi mkubwa katika kutekeleza majukumu yetu, ikiwemo suala la mapato na matumizi ya fedha tunazokusanya, hii itasaidia wananchi kuelewa matumizi sahihi ya fedha zinazokusanywa”, aliongeza Mmbaga.

Awali, Mganga Mkuu Wilaya ya Busega Dkt. Godfrey Mbangali, amesema baadhi ya vifo vya akina mama vinavyosababishwa na uzazi, hutokana na imani potofu katika jamii zetu. “Wengi wanatumia uzoefu wa huduma za uzazi kwa kutumia wakunga, hujifungulia nyumbani na kusababisha vifo kutokea kwani hushindwa kuwa na ujuzi zaidi kuhusu Afya ya uzazi” alisema Dkt. Mbangali.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera, ametaka elimu ya Afya ya uzazi itolewe zaidi kwa wananchi ili kupunguza vifo vya akina mama. Mhe. Mwera ametaka elimu hiyo iwe ya kina ili kuleta uelewa zaidi kwa wananchi. Pia, Mhe. Mwera amewataka wahudumu wa Afya kuwa na msukumo na hali ya kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya utoaji wa huduma za Afya ulio bora Wilayani Busega.

Kwa upande mwingine, Mmbaga ametaka watumishi wa umma kupenda kazi zao kwani ni moja ya jambo muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku. “Lazima kuwe na tija ya motisha katika kutekeleza majukumu ya kila siku, motisha huanza na mtumishi mwenyewe, lakini pia watumishi watambuliwe na kuthaminiwa”, aliongeza Mmbaga. Katika ziara hiyo Mmbaga ameweza kukagua ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Busega na ujenzi wa jengo la upasuaji kituo cha afya Lukungu na kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu hiyo.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III ULIOFANYIKA TAREHE 05.10.2024 October 05, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi October 07, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Busega_2020 November 23, 2020
  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili December 01, 2020
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • TIJA YA KUONGEZA MAPATO; BUSEGA YATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA KUJIFUNZA MBINU

    April 18, 2024
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Yapongeza Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Busega

    February 24, 2023
  • Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega Wapitisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti Mwaka wa Fedha 2023/2024

    February 14, 2023
  • Mgogoro wa Shamba la Kijiji cha Nyamikoma A uliodumu zaidi ya miaka 15 Wamalizika

    January 11, 2023
  • Onyesha zote

Video za Shughuli za Kiofisi na kitaifa

Stili Picha Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Salary Slip - Salary Slip Portal
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Ajira Portal
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Nishati
  • Wizara ya Maji
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa -TFDA
  • Tovuti ya TRA

Tovuti Mashuhuli

  • Tovuti kuu ya Serikari
  • Tovuti ya menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria
  • Kanzidata, Masuala ya Uchumi na Jamii Tanzania
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Sekretarieti ya Ajira Tanzania
  • Tovuti ya Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya TCRA
  • Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Tovuti ya Uhamiaji
  • Tovuti ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini -RITA
  • Tovuti ya Brela
  • Tovuti ya NIDA
  • Tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao- eGA
  • Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Busega

    Sanduku la Posta: 157 BUSEGA

    Simu ya Mezani: +255 282 981 193

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@busegadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki @2019. Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Haki zote zimehifadhiwa